Wakuu naomba msaada kwa hili tatizo

Wakuu naomba msaada kwa hili tatizo

proxy

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
1,481
Reaction score
1,356
Nina jirani yangu kaajiliwa wilaya ya Tunduru ,huyu jilani kwao wamezaliwa yeye na mdogo wake ambae sasa yupo chuo ,baba yao alishafariki wakiwa bado wangali wadogo sana kwa sasa wamebakiwa na mzazi mmoja (Mama), kabda hajaajiliwa mama naye akaaza kuugua na ninavyozungumza sasa hivi kalazwa hospital ya Rufaa Peramiho kwa matatizo aliyokuwanayo ameshauliwa akae karibu na hospital kubwa .Rafiki yangu kajaribu kuomba uhamisho ili akae karibu na mama yake na apate kumuuguza lakini jitihada hazijazaa matunda na pia inamlazimu kusafiri kwa mwezi Mara 3 kwa ajili ya kwenda kumuuguza mama yake,na kafatilia uhamisho kwa hali na mali lakini wapi anazungushwa tu Mara njoo kesho Mara faili sijui lipo wapi Mara palienda pakarudi ,yani imekuwa ni mlolongo wa story zisizo kuwa na tija kwa mhusika .Na ukiangalia kwa undani mama anakaa peke yake kwenye nyumba na akizidiwa inamlazimu kuomba msada kutoka kwa majilani ili wamsaidie ili aweze wahishwa hospital,sasa swali langu ni hili kwa watu wanaomyumbisha huyu mtumishi hivi wanapata nini hasa ? Au wanataka mpaka mtu apoteza mzazi ndipo wamsikilize shida yake? Please kwa yeyote mwenye mchango nakaribisha ndugu zangu.
 
Achukue barua ya daktari inayothibitisha mama ni mgonjwa kisha aiambatanishe na maombi kuanzia kwa bosi wake hadi wilayani. Kuna ndugu yangu kafanikiwa toka Shinyanga hadi dar yeye ni mwalimu
 
Ameshafanya hivyo ila bado ni mizungushano tu ,barua ipo kwa DEO ,lakini kuisaini ndio imekuwa shughuri.
Tatizo la walimu ni kukosa confidence!!! Waogawaoga. Unakuta mwalimu ana degree but anamwogopa PS wa DEO mwenye certificate!!!

Mwambie huyo mwalimu anaweza kumpoteza mzazi wake kwa ujinga wa kumwogopa DEO
 
hapo mlipo nyie hamna hospitali nyingine kubwa karibu ata ya private?, kama ipo amuhamishie hapo.
 
DEO anam treat according to his/her appearance!!! Mwambie akaze vilivyo then utanipa mrejesho. Akishindwa akaonane na MAYOR/M/KITI wa Halmashauri na Mkurugenzi. DEO ni mtu Mdogo saaana
Mkuu mtu kwenye position yake ni shida sana kashaenda kuongea naye Mara kadhaa lakini story ni nyingi ,Mara nitakuruhusu mwezi wa sita Mara oho subiri wa kumi na mbili ,yani suala linaenda miaka 2 sasa.
 
mwambie aende tamisemi kuna mtu atamsaidia! afike chumba namba 12!
 
Ila tukumbuke uhamisho umesitishwa kwa muda , maboresho yanafanyika ila muda si mrefu hali itarudi
 
Back
Top Bottom