Wakuu kwanini Uhonge mwanamke Mpaka uishiwe?

CHIBA One

JF-Expert Member
Nov 16, 2018
560
2,087
Maisha yamebadilika sana...tulizoea kuwapa zawadi za pipi, chupi, saa, wapenzi wetu lakini sasa hivi wanataka i phone 15, gari kali, kulipiwa kodi etc

Vijana wana stress za maisha, lakini wakati huo huo wana stress za kumantain mahusiano yao, wako tayari wasile ili kuwafurahisha mademu zao ambao nao wana wanaume wengine wawili watatu wa kuwaweka mjini...

Kijana akinunua gari cha kwanza anawaza kubeba mademu, akili zimejaa mawazo ya mademu hakuna FOCUS.

Wanawake utasikia wanasema "Tafuta hela utaishia kutuita shemeji" Maneno yanayojenga stress ndani mioyo ya vijana wengi wa sasa kwa maana hiyo kwa sasa Ni biashara ya Ngono inafanywa hadharani watu wanauziana mapenzi.

Kijana una ndoto, una mipango ya kimaisha, bado unajitafuta, kwa nini uwekeze kwenye kuhonga mpaka unaishiwa ili kufurahisha hawa binadamu? Toka umeanza kupata ngono umegundua kuna jipya gani kwa hao mabinti? Kwa nini usitimize ndoto zako kwanza ama ukawa na mmoja ambaye angalau dishi lake halijayumba kama hawa maslay queen wa mjini wanaowaza kugongea hennesy na kujitia filter mitandaoni?

Vijana wengi wamepeta pesa za ghafla wakawekeza kwa mademu na matokeo hayakuwahi kuwa ya kufurahisha, cha msingi jenga territory yako, uwe na financial freedom, ukishakuwa na hela huna haja hata ya kuhonga, utawahonga harufu yako nzuri ya perfume, kiyoyozi cha magari yako, na wala hutakuwa na papara nao. Utachagua kama nyanya sokoni unavyotaka.

#Fatilia kwa nini Masikini wanapenda sana kuzaa, kila mwaka ana mtoto!!
 
_20240216_192131.JPG
 
Kijana una ndoto, una mipango ya kimaisha, bado unajitafuta, kwa nini uwekeze kwenye kuhonga mpaka unaishiwa ili kufurahisha hawa binadamu?
Mkuu wakati unastaajabu wanaohonga hadi wanaishiwa.

Kuna MALOFA leo hii wapo wanapambana namna ya kulipa madeni waliyokopa ili wawanunulie zawadi mademu zao siku ya Valentine.

Focus yao iko katikati ya mapaja ya wanawake. Na mwisho wake ni MATESO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom