PreGE2025 Wakuu kumbe kuna siku ya Samia na hatuambiani?

PreGE2025 Wakuu kumbe kuna siku ya Samia na hatuambiani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ametangaza kuwa maadhimisho ya Siku ya Samia mwaka huu yatakuwa ya kipekee na ya kitofauti.

Amesema kesho Juni 3, 2025, badala ya kukusanya watu wote ukumbini kama walivyokuwa wanafanya, kwa kesho siku hiyo itaadhimishwa kila kata katika Mkoa wa Dodoma kwa mtindo wao wenyewe.

Aidha, Senyamule amesema lengo kuu la kuadhimisha katika kila kata ni kuweza kuwafikia wananchi moja kwa moja na kuwaonyesha kwa vitendo kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo katika kila kata.

Senyamule amewahimiza wananchi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi, kusikiliza mafanikio, kutoa ushuhuda wa mabadiliko waliyoona, na kufurahia mafanikio ya uongozi wa Rais Samia.

“Kwa kufanya hivi, tunatenda haki kwa Serikali na kwa wananchi, kwani kila mtu anatamani kujua Serikali imefanya nini kwake,” amesema RC Senyamule wakati wa mahojiano kwenye Kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo June 2, 2025.
 
kuna siku nimezamia semina flani, katikati ya semina tukatangaziwa ugeni ni mkuu wa wilaya baada ya porojo zake si katuimbisha wimbo wa hbd samia
nkaona huyu mkuu nae umeme mdg kichwani
Hahaha, usingezamia, watu na mikutano yao.
 
Magufuli tulkua tunahs ataongeza mda madarakani,But Samia ndo atafanya hvyo mi nawaambien.
 
Hahaha, usingezamia, watu na mikutano yao.
mkuu kuna ubwege sana siku hizi, kuna siku pia tulikuwa na mkutano wa umoja wetu (kampuni uchwara flani) acha mkuu wa wilaya amuombe katibu amuorodheshee mafanikio ya kakampuni ketu

kaja pale kayaimba mafanikio yetu kwa kibwagizo cha mama kila kitu mama hadi mnabaki mnashangaa

hawa wakuu wamekua wajinga wajinga sana
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
maadhimisho ya Siku ya Samia mwaka huu yatakuwa ya kipekee na ya kitofauti.

Inatukumbusha historia ya koloni la Tanganyika chini ya King George ambapo raia katika mitaa na miji ya Tanganyika walisherehea kwa mashindano ya matamasha, utunzi wa mashairi n.k kumtukuza King George

Na moja ya kumbukumbu za raia kumsifu, kumtukuza King George:

IMEBAKI KUANZISHWA SHINDANO LA SHAIRI KUMUENZI RAIS MFALME

Hatuna tofauti na mababu zetu walivyokuwa wanashindana kuandika mashairi kumpongeza mfalme King George :

Wa-Shairi tusiwe nyuma tufanye hima nasi kuja na tungo kwa ajili ya siku hii ya kumbukumbu 2025, ni uzalendo kiongozi haji bali kwa mapenzi ya Mungu yaani ukiona mtawala ameukwaa uongozi juwa nyuma yake amekingiwa kifua na Mungu.

Tujikumbushe jinsi hali ilivyokuwa enzi za Tanganyika iliyokuwa koloni chini ya utawala wa Mwingereza

Toka maktaba :

Sisi raia inabidi tukae kutunga shairi , wimbo au tenzi kukumbuka siku hii adhimu ya kuzaliwa mtawala wetu Maulana King George V.

Heshima ya King George V ( “Respect for King George V”)16 Kaniki Nguo ya Kale, Dar es Salaam Mambo Leo (c.1923-36)

(1) Leo siku ya tatu katika mwezi wa Juni(1) Today is the third day in the month of June
Kazaliwa Bwana wetu King
George Sultani
When was born our lord and sultan King George
Jamii ya wote shime andameni
Mkongeni
Everyone hurry up and proceed to Mkongeni
Tukatazame heshima ya maulana
King George.
So we see respect paid to His
Highness King George
(2) King George ni mwana wa King
Edward
(2) King George is the son of King
Edward
Amezaliwa Ulaya nchi ya upande wa kaskaziHe was born in Europe in a country to the north
Kama tujuavyo yeye ni pekee asadi17As we know he is a special lion
Tukatazame heshima ya maulana
King George.
So we see respect paid to His
Highness King George
(3) Watakutana mabwana wakubwa na wadogo(3) The noble and the lowly will participate
Hapazuiwi kijana akuambiaye ni mrongoNo youth will not be denied; whoever tells you otherwise is a liar
Wala fujo hapatakuwa ya mafimbo na magongoNor will there be disturbances with sticks or clubs
Tukatazame heshima ya maulana
King George.
So we see respect paid to His
Highness King George
(4) Siku hiyo ni siku ya furija na anasa18(4) This day is a day of celebration and entertainment
Atakayejaliwa kwenda furaha hatakosaWhoever attends will certainly be happy
Kwani ni siku ya idi bashasha yatupasaFor it is a holiday and we are expected to be joyful
Tukatazame heshima ya maulana
King George.
So we see respect paid to His
Highness King George
(5) Atahudhuria Gavana bwana wa
Tanganyika
(5) His Lord the Governor of
Tanganyika will attend
Siku hiyo mwenye nishani itampasa kupachikaOn this day whoever has medals should wear them
Asiyekuwa na mwana hata jiwe ataeleka19The one without children should carry a stone
Tukatazame heshima ya maulana
King George.
So we see respect paid to His
Highness King George
(6) Akina Bwana Askari hupanda wao farasi(6) The soldiers will mount their horses
Mwendo wao taratibu kama mwendo wa papasiThey will pass slowly by, at the speed of a tick
Kuwaonyesha raia mambo yasiyo kiasiTo show the citizens extraordinary things
Tukatazame heshima ya maulana
King George.
So we see respect paid to His
Highness King George
(7) Tazameni ibura ya Mfalme kuwa
Ulaya
(7) Look at this extraordinary celebration for a king who is in
Europe
Huko mambo mbayana kama amehudhuria20There [at Mkongomeni] things will be celebrated as though he were attending
Jamaa ukaidi wani mbona mtaangamia21What’s the point of being stubborn lest you be destroyed?22
Tukatazame heshima ya maulana King George.So we see respect paid to His
Highness King George
(8) Kuna wingi wa Polisi wazuiao hatari(8) There are many police to prevent danger
Wapitisha kwa kiasi zote pia motakariThey only allow selected motorcars to pass
Hiyo ndiyo dunia wala nyingine haiwiThat is indeed how the world is.
It cannot be otherwise
Tukatazame heshima ya maulana
King George.
So we see respect paid to His
Highness King George
(9) Mfalme King George wote mnamjua(9) Sovereign King George all of you know him
Kwa alama za mataji mara utamjuaBy the symbol of his crowns you’ll immediately recognize him
Na utakapo ya zaidi soma utajuaAnd if you want to know more, read about him
Tukatazame heshima ya maulana
King George.
So we see respect paid to His
Highness King George
(10) King George ana sifa kupenda wake raia(10) King George is known for liking his subjects
Walio bora na hafifu wote twamfurahiaThe upper and lower classes we all are happy for him
Tumwombee Rabuka huruma amzidishieLet us pray to God will show more mercy to him
Tukatazame heshima ya maulana
King George.
So we see respect paid to His
Highness King George
(11) Sifa hapa zimekoma mwaka huu najaribu(11) The praises end here, this year I am trying
Labda nitapata yangu huwa bahati nasibuPerhaps I will have my luck
Sikukaa nasimama nangoja yangu matulubu23I am not sitting, I stand, waiting to get what I expect
Tukatazame heshima ya maulana King George.So we see respect paid to His
Highness King George
15The following example of another birthday poem for King George composed by a poet with the pen name “Komagi bin Sansa
 
Back
Top Bottom