tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,516
- 21,542
Napenda kutoa wito kwa Dr Makufuli awafute kazi wakurugenzi wote walioshirikiana na maofisa utumishi kuchomekea wafanyakazi hewa kwa manufaa yao binafsi.
Ni ukweli ulio wazi kwamba makada hawa wa CCM ambao huteuliwa na rais kusimamia maendeleo ya halmashauri, wamekuwa wakitumia madaraka yao kujilimbikizia mali isivyo halali. Kila siku tumekuwa tukilalamika kuhusu uwepo wa mchwa kwenye halmashauri unaofanywa na makada wa CCM lakini kuna watu hata humu JF wamekuwa wakipingpa kwa nguvu zao zote. Jana tumesikia kada mwingine kutoka halmashauri moja huko mkoani Simiyu naye kasimamishwa kazi kwa sababu ya wizi wa fedha za umma.
Aidha, kuna kesi mbalimbali katika hatua tofauti zinazowakabili makada wengine kama hawa kuhusu wizi wa rasilimali za umma.
Huku kusimamishana kazi hakuonyeshi kubadili hali ya ubadhirifu wa mali za umma katika nchi hii. Wakati umefika hawa mchwa wafutwe kazi moja kwa moja pasipo kuangaliana usoni. Huu mtindo wa kuteuana kikada ndio uliotufikisha hapa. Tusicheze na rasilimali za Taifa.