Wakulima wamzuia waziri kuingia ukumbini Mbozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakulima wamzuia waziri kuingia ukumbini Mbozi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Jan 18, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Godfrey Kahango,Mbozi
  WAKULIMA wa Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya wamemzuia Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe kuingia ndani ya ukumbi ili azungumze nao badala ya wafanyabiashara waliokuwa wameandaliwa.

  Tukio hilo lilitokea jana baada ya uongozi wa Halmashauri ya Mbeya kuwazuia wakulima hao wasiingie kwenye ukumbi huo kwa lengo la kutoa kero zao kwa waziri huyo.

  Wakulima hao walichukua uamuzi huo wa kumzuia kwa madai kwamba viongozi wa wilaya hiyo wamewaingiza wafanyabiashara ili wazungumze na waziri huyo huku wakipachikwa jina la wakulima maalumu. Mvutano huo uliodumu kwa takribani dakika 10

  huku wakulima wakimtaka waziri huyo kuzungumza nao nje ya ukumbi uliokuwa umeandaliwa na uongozi wa halmashauri hiyo ulitulizwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.

  Hali hiyo ilionekana kumshangaza waziri huyo na Mkuu wa Mkoa Mbeya Abbas Kandoro baada ya kuona viongozi wa wilaya wakitumia nguvu kuwaondoa wakulima hao bila utaratibu na kutowasikiliza.

  Mkuu wa mkoa huo Abbas Kandoro baada ya kuona mvutano huo unaendelea, aliingilia kati sakata hilo na kuwaruhusu wakulima 10, kati ya zaidi ya 400 kuzungumza na waziri huyo.

  Kandoro alipowapatia fursa, wakulima hao walisema wamezuiliwa kuingia ndani ya ukumbi na viongozi hao na kwamba waliowaingiza ndani ni wafanyabiashara wa kahawa na siyo wakulima wa zao hilo.

  “Sisi wakulima wa zao la kahawa wametukatalia kuingia ndani kuzungumza na waziri na walioingia humo ndani ni wafanyabiashara ambao ndio wanaotunyonya wakati wa kununua kahawa zetu, wananunua kwa bei ya chini na wanaikataza kampuni ya Lima Ltd kununua kahawa mbivu wakati inatulipa bei nzuri na inatupa na pembejeo,”alisema mkulima mmoja.

  Baada ya uongozi wa halmashauri hiyo kuona hivyo, ulijaribu tena kuwaondoa wakulima hao lakini walikataa na kusema kwamba wangeendelea kusikiliza mjadala kupitia madirishani kwenye jengo la ukumbi huo.
  Ndani ya ukumbi huo kulitokea malumbano kati ya wakulima na uongozi wa Halmashauri hiyo kwamba imekuwa ikikumbatia walanguzi wakati haiwasaidii kutunza kahawa yao huku ikiikataza Kampuni ambayo inaonekana kuwa msaada kwa wakulima wa zao hilo.

  Mkulima Malaba Mwasenga kutoka Kijiji cha Itegula, Kata ya Igamba alisema uongozi wa halmashauri hiyo unaipiga vita kampuni ya Lima Ltd huku ikitambua ni msaada mkubwa kwa wakulima wa zao la kahawa wilayani humo.

  “Sisi wakulima wa kahawa tunakombolewa kwa kuuza kahawa yetu kwa bei nzuri kupitia Lima na sio kutoka kwa walanguzi ambao wamekuwa wakitunyonya kwa kununua kahawa kwa bei ndogo,”alisema Mwasenga.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa, Adolph Kumburu alisema kanuni za wizara ya Kilimo zinaruhusu kununua kahawa mbivu kwa ajili ya kutafuta ubora wa zao hilo katika soko la kimataifa.

  Alisema kwamba mkulima anaruhusiwa kuuza kahawa mbivu kwa mujibu wa kanuni hizo na sheria namba 23 ya mwaka 2003 ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2011 inaruhusu ununuzi wa kahawa hiyo.

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Kandoro alisema uamuzi wa mkoa huo katika vikao vyake vilivyoketi mwaka jana, hayatatenguliwa na yatabaki kwamba kahawa hiyo isiuzwe katika kampuni hiyo.Profesa Maghembe alisema uamuzi wa uliotolewa na uongozi wa mkoa na wilaya wa kutoruhusu kampuni ya Lima kununua kahawa mbivu (Cherry) unauacha kama ulivyo.

  Alisema katika msimamo wake, viongozi wa mkoa na wilaya wanapaswa kusimamia bei nzuri kwa mkulima badala ya kuishia kupiga marufuku uuzaji na ununuzi wa kahawa hiyo.
   
Loading...