mkafrend
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 3,047
- 1,503
Ndugu Watanzania, salaam!
Kwa namna yeyote ile binadamu apendaye maendeleo lazima asikiapo habari au tetesi za watumishi hewa machozi yatamlenga lenga kwa kuwa tunaziba nafasi za watanzania wenzetu ambao wangeajiriwa kwa nafasi hizo tusingekuwa na uhaba wa madaktari, walimu, watendaji, wagavi n.k
Hata hivyo bila kuwa mwanasiasa ingawa chembe chembe za siasa ninazo, kwa muda mrefu wakulima walioko kwenye mikoa inayopata ruzuku za pembejeo (mbolea) mwaka kwa mwaka wamekuwa wakidhurumiwa mbolea zao toka kwa mawakala na kusababisha hasara nyingi zisizoelezeka ambazo ni pamoja na:
Tusifanye kazi kwa matukio na maagizo ya RAIS tu bali tusaidie kuibua issues na kuzifanyia kazi hata kabla rais hajazifahamu. Ni aibu viongozi mkiwa katika maeneo yenu kutoibua issues ambazo ni kero kwa wananchi. - MSAIDIENI RAIS MAJANGA NI MENGI HUKU

- Kuvuna nafaka kidogo sana;
- Kupungua kwa kipato cha mwananchi (per capita income);
- Kuendelea kuwa maskini na mkulima atumiaye jembe la mkono n.k
- Kuingiza mbolea kipindi kisichoendana na wakati (kuchelewesha mbolea) za kupandia huletwa kipindi cha palizi au mavuno;
- Mbolea za kukuzia vile vile huletwa kipindi cha mavuno n.k
- Mawakala kupoka mifuko ya mbolea kwa kuwarubuni wakulima na vijifedha kidogo kisha vocha zikishajazwa mawakala huondoka nazo as if tayari mkulima amepata mbolea kumbe imerudishwa kwenye gari na kuuzwa nje ya nchi