Wakulima wa Matikiti - Msaada

Wakulima wa Matikiti - Msaada

ASHA NGEDELE

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
784
Reaction score
327
Habari wakulima,

Kama kuna ambae huwa analima na kuuza tikiti masoko ya dar es salaam naomba aniunganishe na dalali wake ambae ni mwaminifu ili niwe namtumia kumpelekea mzigo wangu ukiiva.

Nina dalali huwa namtumia yuko soko la Buguruni lakini amekua mjanja mjanja sana na pesa siioni. Najua dalali wengi (kama sio wote) wana utapeli ndani yao lakini wanatofautiana wengine wana nafuu.

Kwahio naomba mwenye kunipatia msaada huu aje private.

Asante
 
Mkuu Pole madalali watajihami kabisa ukiwaachia mizigo sababu tu ya hilo jina. Asha ngedele.
Yaani ninakoment huku nikiwa nafikra na mtu gani huyu.
Ok Asha Ngedele nitakuunganishia kwa dalali moja yupo humu JF kwa jina Basha Wako. Mtafute au
Pm Basha Wako atakusaidia
 
Dah hilo jina mbona linatisha..Basha tena . Ila nashukuru mkuu, niunganishe nae nizungumze nae nkaone na soko analouzia.

Jina langu lisikutie sana mawazo
 
Dah hilo jina mbona linatisha..Basha tena . Ila nashukuru mkuu, niunganishe nae nizungumze nae nkaone na soko analouzia.

Jina langu lisikutie sana mawazo
Huyo Mkuu ukienda mzima mzima atakuwa Basha wako!
 
Wafanyabiashara wa aina 3 wenye roho ngumu duniani ni wanaodeal na:

1.Network Marketing
2.Wakulima wa matikiti
3.FX traders.
 
Wafanyabiashara wa aina 3 wenye roho ngumu duniani ni wanaodeal na:

1.Network Marketing
2.Wakulima wa matikiti
3.FX traders.
Haha nililima tikiti asee ukiwa mtu wa kugive up kirahisi unaweza pata ugonjwa wa moyo... tikiti lina stress nyie acheni tu
 
Kwa hayo maelezo yako yaelekea na wewe ume-give up mana umesema ulilima.
Msimu huu nimepumzika see niliponea chupuchupu kupata loss, nashukuru hela yangu tu imerudi, nibora nifanye Mambo mengine kuliko kutumia nguvu na muda mwingi alafu faida kiduchu
 
Habari wadau! Mimi nina taka kufanya biashara ya muhogo na nipo kivukoni Dar naomba mwenye kujua unapopatikana anijulishe tafadhal
 
Haha nililima tikiti asee ukiwa mtu wa kugive up kirahisi unaweza pata ugonjwa wa moyo... tikiti lina stress nyie acheni tu
Kuna jamaa yangu alilima zikatoka na shape ya tango.....

Alilia kama mtoto sasa najiuliza mpaka sasa alikosea wapi
 
Kuna jamaa yangu alilima zikatoka na shape ya tango.....

Alilia kama mtoto sasa najiuliza mpaka sasa alikosea wapi
Haha poleni, tikiti ni timing ya maji madawa na mbolea.
Pengine hakutumia zile dawa za kunenepeshea amazo unakuwa unapulizia
 
Back
Top Bottom