Wakulima wa korosho wamwangukia Mbatia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakulima wa korosho wamwangukia Mbatia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waridi, Mar 12, 2012.

 1. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Chanzo: Tanzania Daima

  Wakulima wa korosho wamwangukia Mbatia


  na Mwandishi wetu, Masasi


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]BAADHI ya wakulima wa zao la korosho Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara, wameonyesha dalili za kukata tamaa juu ya zao hilo kutokana na kukosa soko na bei ya uhakika ya zao hilo.
  Wamesema kuwa, pamoja na kwamba wao wanaishi kwa kutegemea korosho, hawaoni dalili za kubadilika kimaisha kwa vile kila mwaka wanalilima kwa hasara.
  Wakulima hao waliyasema hayo juzi kwa nyakati tofauti walipokuwa wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
  Mbatia ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kuimarisha chama, alihutubia mkutano huo katika viwanja vya Yatima vilivyoko mjini hapa.
  Akizungumza katika mkutano huo, mkulima Rajabu Pazi, alisema kutokana na kutokuwa na soko la uhakika la zao hilo, baadhi ya wazazi wameshindwa kusomesha watoto wao sekondari kwa vile kila wanapovuna na kuziuza, wamekuwa wakizikopesha badala ya kulipwa fedha tasilimu.
  Kwa mujibu wa mkulima huyo, hata wanapouza zao hilo, wamekuwa wakiuza kwa bei ya chini ambayo haiendani na gharama za maisha.
  “Mheshimiwa Mwenyekiti, ni afadhali umekuja, sisi huku tuna hali mbaya sana kwa sababu kila wakati tunakopwa korosho zetu na pale tunapoziuza huwa tunauza kwa bei ya chini. Yaani hata wazazi wanashindwa kuwasomesha watoto wao sekondari,” alisema Pazi.
  Mkulima mwingine aliyejitambulisha kwa jina la David Maganga, naye alisema haridhishwi na jinsi Serikali inavyolichukulia zao hilo kwa kuwa wakulima hawana sauti.
  Kutokana na hali hiyo, alimtaka Mbatia afanye kila linalowezekana ili wakulima wa korosho wanufaike na zao hilo kwa kuwa hawana mazao mengine mbadala zaidi ya korosho, karanga na choroko.
  Akijibu hoja za wakulima hao, Mbatia alisema shida wanazozipata Watanzania wakiwamo wakulima hao, zimesababishwa na wao wenyewe kwa kuwa hawataki kuviunga mkono vyama vya upinzani badala yake wamekuwa na kawaida ya kuwachagua wagombea wa CCM.
  Naye Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali, alizidi kuwataka wananchi wa Mtwara wasiichague CCM kwa kuwa ndani ya miaka 50 imeshindwa kuonesha utu kwa Watanzania na kwamba kutokana na hali hiyo ndiyo maana wakulima wa korosho wamekuwa wakiishi maisha ya shida kila mwaka.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukiwauliza mbunge wao katoka chama gani utasikia ni ccm alafu na bado anaing'ang'ania huku wakilalamika
   
Loading...