Wakulima wa korosho tukutane hapa

Wakulima wa korosho tukutane hapa

Nascoba

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2012
Posts
310
Reaction score
160
Wakulima wa korosho ktk nchi hii inayowajali na kuwasimamia wanyonge wananyanyasika ktk kupokea malipo ya korosho zao walizouza kiasi ambacho iko wazi mazingira ya dhuluma dhidi yao yanaandaliwa kwa ustadi mkubwa na serikali yao.mfano ktk halmashauri ya Wilaya ya Tunduru baadhi ya wakulima korosho zao zilichukukiwa tangu mwezi wa kumi lakini wengi wao hawajalipwa hadi leo huku wakivurugwa ktk malengo yao ya kuandaa watoto waende shule pamoja na msimu mpya wa kilimo
Ambapo mvua zimekwisha anza na mbaya zaidi wako ambao walishajenga majumba wakitarajia watamalizia kuezeka baada ya kupokea pesa
Zao lakini kwa masikitiko makubwa majumba hayo yameanza kubomoka na mvua zilizoanza
Na bado ktk hali hiyo si mkuu wa mkoa wa Ruvuma wala mkuu wa Wilaya ya Tunduru wala Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya wanaoguswa na hali hii kiasi cha kujitokeza kuwaeleza wananchi kinachoendelea.
Tunamuomba Rais magufuli apitie upya teuzi alizozifanya ktk mkoa huu na hasa Wilaya ya Tunduru.wakulime wameambiwa malipo yao lazima yapitie bank lakini kuna urasimu mkubwa ktk ufunguaji wa hizo account kiasi ambacho Mkulima anatoka kijijini kwenda Wilayani kufungua account na inamchukua hadi wiki akiwa ktk foleni huku hana pesa ya kula wala ndugu yeyote mwisho wengine wanakatata tamaa na kuamua kuachana na zoezi hilo bila kujua hatma ya pesa zake itakuwaje.
Tunaomba sana mheshimiwa Rais amulike hali za wananchi wa Tunduru na hatma yao juu ya malipo ya korosho walizouza.
 
Back
Top Bottom