[SIZE=-1][/SIZE]Shirika la Habari la B.B.C. Jumanne Aprili 6, 1999 asubuhi (B.B.C. World Service) lilielezea taarifa ya shirika moja la Haki za Binadamu juu ya Mauaji ya Rwanda. Taarifa hiyo imeonyesha mchango wa Kanisa Katoliki katika mauaji na jinsi baadhi ya Maaskofu walivyohusika.
[SIZE=-1]Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kiongozi mmoja wa Kanisa Katoliki aliyehusika sana na mauaji ya kuangamiza huko Rwanda amehamishwa na kufichwa huko Paris.[/SIZE]
[SIZE=-1]Taarifa ya shirika hilo la Haki za Binadamu ikasema kwamba huko ni kuwalinda wauaji na kulivunjia heshima Kanisa Katoliki na kulitaka lijisafishe angalau kwa kuwatoa wauaji washitakiwe.[/SIZE]
[SIZE=-1]Waislamu tuna uchungu na nchi yetu; tunaipenda na tunatamani idumu katika hali ya amani na utulivu. Waislamu tunathamini uhai, heshima na haki ya kila Mtanzania na kila binadamu. Lakini tunajua vile vile kwamba penye dhulma amani haidumu. Amani haiwezi kudumishwa kwa kuwalinda wachochezi na wauwaji huku shutuma kubwa ikielekezwa kwa wadhulumiwa.[/SIZE]
[SIZE=-1]Tunatamani kudumu na Tanzania yetu yenye amani na utulivu ambapo kila raia anapata haki yake na haonewi kwa namna yoyote ile. Ni kwa ajili hiyo basi tunaisihi serikali ijisafishe angalau kwa kuwatoa wauaji washitakiwe.[/SIZE]
[SIZE=-1]Kauli za kuhimiza amani, amani na kuwatisha watu na matukio ya Rwanda hayatusaidii na pengine zimepitwa na wakati. Litakalotusaidia ni kuyafanyia kazi yale ya Waraka wa Abu Aziz, Waraka wa Ponda, Kamati ya kupigania haki za Waislamu, Kamati ya akina mama na yale aliyozungumza Mh. Kitwana Kondo Bungeni.[/SIZE]
[SIZE=-1]Kuwaita Waislamu wachochezi kwa kudai hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wauaji ni kuiweka rehani amani ya nchi yetu. Amani ya kweli ni ile yenye haki kwa wote. Tusiwe weledi wa kutoa mifano ya Rwanda, Burundi, Lebanon na sasa Indonesia huku tunaendekeza yaleyale yaliyozitosa nchi hizo katika janga.[/SIZE]
[SIZE=-1]Hofu ya kupungukiwa na manufaa yanayotokana na kuhodhi nafasi zinazowapa fursa baadhi ya watu kufanya wawezavyo dhidi ya Waislamu isituangamizie nchi. Wala isidhaniwe yupo Mtanzania wa kukubali kuendelea kuona anadhulumiwa na kuonewa daima dumu. Vinginevyo tusingekuwa na akina Mkwawa, Mirambo, Chifu Kimweri, Mashujaa wa Majimaji n.k.[/SIZE]
[SIZE=-1]Tuitambue haki, tuitende na kuidumisha kwa wote ili tudumishe amani. Sote tupo ndani ya jahazi moja; tusipomkemea anayetaka kulitoboa tutaangamia sote. Ni jukumu letu sote wananchi kuikemea dhulma na kuhimiza haki na uadilifu. Na kwa muktadha huu kama Kanisa Katoliki lilivyopewa nasaha kuwa liwatoe washiriki wa mauaji ya Rwanda washitakiwe, tunainasihi serikali yetu tukufu iwafikishe mahakamani walioitikia na kutoa amri ya "Piga shaba", "piga yule".[/SIZE]