Wakristo na waislam tupendane

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,807
18,534
Ninawafahamu watu wema na wabaya wengine Wakristo na wengine Waislamu. Ninawajua watu wenye akili nyingi na nzuri sana kutoka dini hizi mbili. Wapo warembo na watanashati wenye mvuto, Wakristo kwa Waislamu. Binafsi nina marafiki wengi kutoka kila upande. Japo nimelelewa katika familia ya kikristo sana, mchumba wangu ni muislamu mzuri.

Nimetembea pande zote za nchi hii nimeona matajiri na maskini katika kila mkoa na kila wilaya, waislamu kwa wakristo. Nimesoma shule na vyuo mbalimbali Tanzania nimeona vijana wakristo kwa waislamu wakipasi ama wakifeli. Nimewaona wahuni, majambazi sugu, matapeli, wakware na ma-masters, waliobobea wakiitwa John na wengine Hamisi. Kati ya makahaba wakubwa wa nchi hii, wapo akina Asha na akina Joyce pia.

Nimechukizwa na mila na desturi mbaya za baadhi ya waislamu na wakristo vile vile. Nimefurahishwa na ukarimu na upendo wa waislamu na wakristo kila nilipopita. Ninavutiwa na viongozi shupavu wa nchi hii, kama Nyerere na Karume. Mafisadi wakubwa wa nchii yetu, wawe papa au nyangumi wengine ni Wakristo na wengine ni Waislamu. Wapo watu nchi hii hawafanyi kitu bila ushirikina ilhali wakidai kwamba wao ni wailslamu na wengine ni wakristo.

Nimeshuhudia viongozi wengi wa dini wakiwaongoza watu kwenye ukweli na wengine wakiwa kikwazo kwa waumini wao, makanisani na misikitini.

Nakumbuka nilipougua wakati fulani walikuja kunifariji waislamu na wakristo.

Kati ya mkristo na muislamu hakuna bora zaidi ya mwingine. Kama ni hali duni kimaisha hili ni tatizo kwa wote. Nimesaidia ombaomba wengi wakristo kwa waislamu. Kama ni kuporwa rasilimali zetu sote tunaibiwa bila kujali imani zetu. Kama ni kufa kwa magonjwa yanayotibika hili linawakumba wote. Malaria inaua Kaskazini Unguja, malaria inaua Kilimanjaro. Kama ni kudharauliwa na wageni tunaowamilikisha rasilimali zetu nimeona waislamu kwa wakristo wakidharauliwa na hata kuuwawa.

Sote tunahitaji kujinasua kutoka katika umaskini, ujinga na maradhi. Hawa ndio maadui zetu wakubwa. Waswahili wanasema usilaumu ulipoangukia laumu ulipojikwaa. Wengi wetu tumejikwaa katika ujinga tukaangukia kwenye umaskini na maradhi. Chanzo cha umaskini na maradhi yetu sio dini ya mwenzetu au hata si dini zetu wenyewe. Tatizo ni ujinga wetu.

Katika maisha yangu nimeona wakristo wajinga, nimeona waislamu wajinga.

Tuache fitina na majungu kati yetu, tuache kudharauliana na kuchukiana, kufanya hivyo tunampa adui yetu nguvu, badala yake tushirikiane bega kwa bega, tupendane na kusaidiana, na dini zetu zitusaidie kuona kwamba sisi ni watoto wa Baba Mmoja ambaye naamini hafurahii hata kuona tukijiita Wakristo ama Waislamu bali anapenda kutuona tukishirikiana kama ndugu!
 
Asante sana mkuu kwa mada hii ambayo naamini itasaidia kufuangua macho wakristo na waislam.
 
Asante sana mkuu kwa hi mada coz c waislamu wote 2nawaita wakristu makafiri mi binafsi sipendi kabisa kumwita m2 hivyo,coz km kumtafuta Mungu wote 2namwomba Mungu m1 ila njia za kuomba ndo tofauti, waislamu na wakristu 2pendane jamani,tofauti za kidini zisitujengee chuki baina yetu ila dini ndo zitusaidie kuungana katka maendeleo ya nchi ye2.
 
Waislamu wao mtu asiyekuwa muislamu wanamuita kafiri, so there is no compromise on this matter.
Kafiri ni neno la kiarabu lenye maana mtu anayepingana na kitu kingine, ni kweli mkiristo hupingana na Muislam kiimani lakini upendo ni muhimu kwa kila mtu.
 
tutapendana tutakapo balance capacity of understanding,different is too big!!!!!!
 
Asante sana mkuu kwa hi mada coz c waislamu wote 2nawaita wakristu makafiri mi binafsi sipendi kabisa kumwita m2 hivyo,coz km kumtafuta Mungu wote 2namwomba Mungu m1 ila njia za kuomba ndo tofauti, waislamu na wakristu 2pendane jamani,tofauti za kidini zisitujengee chuki baina yetu ila dini ndo zitusaidie kuungana katka maendeleo ya nchi ye2.

Hapo kwenye nyekundu inaashilia HATARI...si kweli kwamba Mungu wa Israel ndiye mungu alla ...ni uongo wa shetani huo!
Hoja ya msingi hapa ni kupendana sababu wote tu wanadamu na muumba wetu mmoja ila kila mtu anamuabudu mungu aliyeamua kumuabudu ama aliyedangamya kwamba huyo ndiye mungu (kazi ya shetani ni kudangamya). Yupo anayemuabudu aliyemuumba na yupo aliamua kuabudu kitu kingine. Mfano wengine wanaabudu jua, mwezi, mlima, mti nk Mtu anayeabudu mwezi hawezi sema mungu wake ni sawa na wa yule anayeabudu jua!!

Nikirudi kwenye swala la wakristu na waislam kuna totauti sana ya ideology, kwanza kwa wakristu amuri kuu ni upendo kwa binadamu mwenzake kwa waislamu ni upendo kwa muislamu mwenzake!! hapo ndo utaona neno kafri linatoka wapi!
 
kama watanzania tutasema tuache kuongea maswala ya dini,
dunia itaongea
leo hii nenda ubalozi wa marekani unataka visa na jina lako la kiislam kama utapewa

matatizo haya yalianza kipindi cha nyerere. alitupindisha sana waislam yule mzee,
rosemarie, umeolewa wewe ? maana mmhhh
 
Back
Top Bottom