Wakosa mke kisa mjinga mmoja hivi

Wakosa mke kisa mjinga mmoja hivi

mtamaushi2

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2015
Posts
403
Reaction score
391
Kuna binti hapa mtaani ni kama wiki tatu sasa namfukuzia anantolea nje kisa anasema hawaamini wanaume wote.

Anasema alikua na mwanaume na alimpenda sana but akaja kumuacha kwenye mataa kwa kumsaliti. Tokea hapo anasema anawaona wanaume wote ni waongo. Kila nikijaribu kutupua nyavu anakuwa mkali kama mbogo. daaaaahh inaniuma saanaa ukizingatia mtoto ni mzuri balaa. nilizidisha kumfuata baada ya kunambia yupo single.

Tatizo kubwa ni huyu mwanaume aliyekuwa nae alimsaliti na kumwambia hamtaki.

Ombi langu ni: sisi wanaume tuache kuwatendea mabaya wanawake.

Wanawake pia muache kuwa na mtazamo wa samaki mmoja akioza wote wanakuwa wameoza muda mwingine unaweza kukosa mtu mwenye mapenzi ya kweli na anaekupenda kwa dhati kisa tu unaamini wanaume wote ni wabaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi nimekuwa mvivu wa kusoma hizi threads sijui kwa nini....au nimerogwa?

Sent from my TV
 
penda unapopendwa usilazimishe kupendwa usipopendwa utakuja kutendwa .
 
Sipendi hii tabia wanawake wengi wananiletea hii sababu...mimi nimeacha KUTONGOZA SASA
 
Achana naye tafuta ambaye hajatendwa. Muda utakapofika huyo aliyetendwa atawatafuta kwa lazima na yote aliyotendewa atayasahau.

Ila nyie wanaume wabaya aisee. Khaaa.
 
Hata kama asingetendwa, usingempata tu. Kwa sababu angepata kisingizio kuwa Nina MTU wangu tayari.

Hiyo ni njia ya kukutupa nje ya box. Jisogeze pembeni Mzee.
 
Mwanamke hata ukimuacha kwa kumfumania ,usipokua makini bado atakwambia Hivyohivyo.

Mwanamke ni kiumbe waajabu sana.

Asipotongozwa anasema ninamkosi ,
Akitongozwa anadengua,

Ukionyesha kumpenda anakuonyesha vitimbi.

Anatembea nusu uchi ,akikaa kwenye kiti anajifanya kuziba sehemu nyeti.
Hovyo sana hasa wadada wa sikuhizi.
Shaulizako mkuu.
 
Hata kama asingetendwa, usingempata tu. Kwa sababu angepata kisingizio kuwa Nina MTU wangu tayari.

Hiyo ni njia ya kukutupa nje ya box. Jisogeze pembeni Mzee.
Ulikuwa kwenye akili yangu. alafu kitu nimegundua wanawake wengi wanatumia huo msemo ili waonekane kuwa wanajielewa, au hard to get kumbe sio. utakuta anaipigisha sana huko alafu anajiadai kuwa sitaki mtu. chezea dushee
 
Endelea kutupia nyavu ataelewa tu
Watu wametongoza mara 60 ya 61 ndio anakubaliwa.
 
Achana naye tafuta ambaye hajatendwa. Muda utakapofika huyo aliyetendwa atawatafuta kwa lazima na yote aliyotendewa atayasahau.

Ila nyie wanaume wabaya aisee. Khaaa.
Siyo wote hata nyie baadhi ni wabays pia.
Ushahidi ninao
 
Hujui kutongoza, nenda VETA kapate ujuzi kwanza utajua namna ya ku win vikwazo vidogo vidogo kama vya huyo mrembo!
 
Back
Top Bottom