Wakorea kujenga hospitali ya meli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakorea kujenga hospitali ya meli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Aug 5, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMAPILI, AGOSTI 05, 2012 07:26 NA JOHN MADUHU, MWANZA

  HALMASHAURI ya Wilaya ya Sengerema kwa kushirikiana na wafadhili kutoka Korea Kusini wanatarajia kujenga hospitali ya meli kwa ajili ya kutoa matibabu kwa wananchi wanaoishi katika visiwa vilivyopo katika ziwa Victoria.

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mathew Lubongeja ameieleza Mtanzania kuwa meli hiyo itajengwa maalumu kwa ajili ya kutumika kama hospitali inayotembea.

  Lubongeja alisema tayari vifaa vya kujenga meli hiyo vimekwisha kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam kutoka Korea Kusini na vinatarajiwa kusafirishwa wakati wowote kupelekwa Mwanza kwa ajili ya kuunganishwa na kuwa meli kamili.

  Alisema hospitali hiyo inayotembea itakuwa ikitoa huduma za matibabu kwa wananchi wanaoishi katika visiwa na itakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa na kutoa huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na upasuaji.

  "Meli hiyo ni ya aina yake, wananchi wanaoishi katika visiwa katika ziwa Victoria walikuwa na tatizo la kupata huduma ya hospitali kutokana na mazingira yao, tumejitahidi kutafuta wafadhili na ndoto yetu imetimia wananchi hao watapata hospitali ya uhakika inayotembea," alisema.

  Lubongeja alisema kazi ya kuiunganisha meli hiyo itakayotumika kama hospitali inatarajiwa kuchukua muda mfupi na kuwapongeza wafadhili hao kwa msaada huo.

  Wilaya ya Sengerema inaongoza kwa kuwa na visiwa vingi katika ziwa Victoria. kwa kuwa na visiwa 37 hali ambayo imekuwa ikisababisha wananchi wengi kukosa huduma za matibabu kutokana na kutokuwapo usafiri wa uhakika.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145

  Sasa hapo ndio Maendeleo tunayoyataka kwenye Mwambao wa ZIWA VICTORIA...

  Yeah hapo ndio naona faida ya kuwapa ka-ardhi chetu... sioni faida ya kuwapa wa-Iran zaidi ya kutuongezea

  Matatizo, Misaada yao Wanapeleka Zanzibar Ardhi tumewapa Bara...
   
 3. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  M2 wangu me cdhani mambo ya kweny maji co kabisa.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Itapiga nanga haitatembea... na itakuwa Meli ya Uhakika
   
 5. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  This is very heartening. All the best
   
 6. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Bac 2kumbuke kulifanyia marekebisho maana likikaa sana kwenye maji litaharibika 2 hata kama litakuwa stationary.
   
 7. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Itakidhi mambo mawili. Kutibu wagonjwa na kuvua sangara pia!
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Nina Maana itasafiri kando kando mwa ziwa kwenye Mwambao na kupaki kusubiri Wagonjwa Mfano itakwenda Ukerewe

  na kukaa kusubiri wagonjwa; Itakwenda Ukara na kufanya hivyo hivyo wakati inatibu itakuwa stationary
   
Loading...