Wako wapi watetezi wa Spika Sitta!

M-bongo

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
338
71
Ni muda mrefu sasa tangu spika wa bunge letu tukufu alipoanza kuhusishwa na tuhuma mbali mbali, wana Jf wengi walijitokeza bila kusahau vyombo mbali mbali vya habari kumtetea SS! sakata linaloendelea mjini Dodoma kwa sasa katika Bunge ni kielelezo tosha kuwa SS si muadilifu kiasi ambacho wengi tungependa tuamini.

kamati ya maridhiano ambayo imekuwa ikiongozwa na Mzee Mwinyi mambo mengi yameibuka ikiwa ni pamoja na SS kuhusishwa moja kwa moja na ujio wa kampuni tata ya Richmond!

taarifa ambazo zimepatikana siku chache zilizopita ni kuwa Mh SS akiwa TIC ndiye aliyebariki ujio na kutoa maelekezo anuai ili wahusika wa Rich mond waweze kupewa msaada pindi ambapo wangehitaji, hiyo haitoshi lakini SS amethibitika kutembelea ofisi za Richmond oversees na hata kupiga picha ya pamoja na mohamed Gire mtuhumiwa mkuu wa Richmond lakini kama hayo haya toshi ni siku chache zilizopita TAKUKURU ilianza kuwahoji baadhi ya wabunge kwa tuhuma za posho mbili! SS kama mpambanaji wa ufisadi kama ambavyo angependa tudanganyike hivyo, akaja juu na kuwa mithili ya Nyati alijeruhiwa kwa risasi kwa ku tetea eti wabunge wasihojiwe NOSENSE! wengine wakadiriki kusema kuwa wanao wahoji wabunge lengo lao ni kuwa ziba midomo wapambanaji bandia wa ufisadi, hoja hii haina mashiko kabisa.

Nimalizie kwa kuwaomba wote waliokuwa mstari wa mbele kumtetea mnafiki, mwenye wivu wa kukosa Uwaziri mkuu SS waje hapa jamvini na watueleze kwa kiasi gani wamekuwa wafuasi wa SS, na kwa kiwango wamekuwa wakimtetea Sita pasipo kuwa na ushadi yakinifu zaidi ya upambe na ulipyoto!

Tunawaomba jamvini hapa na kama ni waungwana mkiri kuwa mlipotoka kumtetea Sita mimi na wengine wengi tupo tayari kuwasamehe endapo nafsi zitawaagiza kufanya hivyo
 
kamati ya maridhiano ambayo imekuwa ikiongozwa na Mzee Mwinyi mambo mengi yameibuka ikiwa ni pamoja na SS kuhusishwa moja kwa moja na ujio wa kampuni tata ya Richmond!

Ukileta topic njoo na ushahidi, wewe kwenye hicho kikao ulikuwepo?
 
Kibaya zaidi SS alitaka kila mtu amuamini kuwa yeye na wenzake ni watetezi wakubwa wa watanzania ikiwa ni pamoja na kupambana na ufisadi jambo ambalo limegundulika kuwa silo, wameshikwa pabaya, wameinama, wanaona aibu!
 
K4jolly! huna mawasilino na vyombo vya habari? au unaishi Dunia gani ambayo hadi sasa huelewi yanayotokea Tanzania, au umeuguwa ugonjwa wa Macho ambao wataalamu huuita UMOFIA? ambao humfanya mtu asiweze kuona mbali yaani short sighted?
 
Samwel Sitta ni fisadi mwandamizi, alipokuwa TIC madudu aliyoyafanya yataendelea kuli gahrimu taifa hili kwa miaka mingi ijayo.

Huko bungeni ndio hatari zaidi, kajipangishia jumba la milioni 10 kwa mwezi, kaagiza Mercedes ya Uspika ilhali ile ya mwanza haina hata miaka miwili kwa mamilioni ya pesa. Mtu mzima anafoji mpaka risiti za matatibu kwa mamilioni ya pesa. Anatumia magari ya serikali kuhudumia vimada, I can go on and on huyu mzee hafai no wonder anatetea posho mbili wizi wa waziwazi.
 
Kibaya zaidi SS alitaka kila mtu amuamini kuwa yeye na wenzake ni watetezi wakubwa wa watanzania ikiwa ni pamoja na kupambana na ufisadi jambo ambalo limegundulika kuwa silo, wameshikwa pabaya, wameinama, wanaona aibu!


Richmond kamam walikuja kamam wawekezaji huo mwakak 2001 si ajabu kufanya mawasiliano na kituo cha uwekezaji ambacho Sita alikuwa kiongozi wake... suala ni Mkataba walioingia wa umeme sio walikuja vipi... hivi watu wengine mkoje?
 
Back
Top Bottom