Wako wapi mashujaa wa maadili UVCCM? (Raia mwema 30/11/2011) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wako wapi mashujaa wa maadili UVCCM? (Raia mwema 30/11/2011)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joseph Peter, Nov 30, 2011.

 1. J

  Joseph Peter Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wako wapi mashujaa wa maadili UVCCM?
  Na Godfrey Dilunga
  KAMA kuna vijana wenye maadili ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) bila kujali wingi wao bali uzito wa hoja, basi wanahitaji kufanya jambo moja kati ya mawili au hata yote mawili.

  Mosi, kuwakana wenzao walioko kwenye mkondo wa kifisadi ambao Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amewahoji kwenye kikao cha Halmashauri Kuu (NEC); wamepata wapi fedha (kuhonga wenzao).

  Wanaweza kuwakana kwa kutumia njia sahihi kinidhamu kwa mujibu wa mfumo wa UVCCM au CCM (taasisi mama). Wanaweza kuwashitaki rasmi kwenye kamati za maadili. Hili la kwanza.

  Pili, wanaweza kuanzisha mapinduzi ‘matakatifu’ ndani ya umoja huo ili kuwapindua vijana hao ambao tayari ni sawa na mbegu mbaya kimaadili. Ndiyo, ni mbegu mbaya inayowakilisha ‘viongozi’ wanaoweza kununuliwa ili kutimiza ajenda binafsi za mtu au genge fulani.

  Katika hili la pili, vijana wenye maadili bila kujali idadi yao bali kwa kujali nguvu ya hoja kwa mujibu wa matakwa ya kimaadili, wajipange kuratibu na kutengeneza mpasuko rasmi na maalumu.

  Mpasuko wenye uhalali wa kisiasa na kimaadili mbele ya umma wa vijana wa Tanzania na wananchi wote kwa ujumla. Mgogoro au mpasuko huu ni wenye tija kwa sababu unalenga kutenganisha kati ya uadilifu na uozo miongoni mwa kundi kubwa la vijana.

  Kutengeneza mpasuko au mgogoro huu wenye uhalali wa kisiasa na kimaadili ni hatua ya kishujaa, tena inayohitaji mashujaa wa kweli kimaadili. Hakuna ubabaishaji hapa.

  Swali la Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwenye vikao vya NEC-CCM, kati ya Novemba 24 na 25, wiki iliyopita linatoa fursa kufanya haya mawili kama nilivyoyaeleza.

  Lengo ni kutaka UVCCM ibebe msimamo wa uadilifu mbele ya vijana wa Tanzania, ambayo vijana hao wametia doa. Tahadhari ni kwamba, kitendo cha vijana wote UVCCM (wakiwamo wenye maadili kama wapo) kukaa kimya kama vile hakuna kilichotokea ni sawa na kuridhia kuwa umoja huo si kielelezo tena cha taswira ya vijana wa Tanzania.

  Kikwete amenukuliwa akimhoji Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa na baadhi ya wenzake; wamepata wapi fedha za kununua (kuwahonga) wenzao? Hapa, mjadala si kwamba wamepata fedha au la, mjadala ni kwamba fedha wanazo isipokuwa wamezipata wapi?

  Kwa lugha inayoeleweka tena pengine kwa kuzingatia mantiki ya maneno ya Mwalimu Nyerere; “Mtanzania wa leo ili amnunue mwenzake naye kwanza ni lazima kanunuliwa: Rais anahoji; nani amewatia mfukoni vijana hawa? Kwamba vijana hawa wanatumikia mtu au genge fulani linaloendesha siasa za rushwa.

  Kipato cha vijana hao hakitoshi kusafirisha, kulipa posho na kugharimia malazi kundi kubwa la wenzao. Imeelezwa pia fedha zilizotumika (kununua akili, nguvu ya maarifa ya vijana hao) hazikutokana na mfumo wa fedha za chama hicho. Ni fedha nje ya mfumo rasmi ambazo Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema; “fedha za wauza bangi”.

  Ndiyo, Mwalimu aliwahi kuonya tusipoangalia ipo siku tutapata Rais anayetokana na fedha za bangi. Pengine hizi ni dalili, tumeanza kupata vijana wanaolipwa fedha za bangi na bila shaka, tusipokuwa makini hawa watatuletea mgombea anayetokana na fedha hizi ambazo lazima azirejeshe atakapopata madaraka.

  Kwa mantiki hiyo, vijana hawa wamenunuliwa kwa fedha za bangi. Wamesafirishwa, kulipwa posho na kugharimiwa malazi kwa “fedha za bangi.” Kwa vyovyote, mawazo, vitendo na mwekeleo wao utafanana na hao “wauzaji bangi.”

  Hapa, wenye akili lazima wafikiri na kuhoji zaidi. Je, Malisa na wenzake wote walionufaika kwa “fedha za bangi” bado wanayo hadhi kimaadili kubaki madarakani?

  Je, vijana wenzao (mashujaa wa maadili kama wapo) watachukua hatua gani? Je, watawasilisha malalamiko rasmi ili wenzao wachunguzwe na kushughulikiwa?

  Je, watakaa kimya na kwa hiyo, UVCCM kama taasisi kubeba taswira ya kutiwa mfukoni na genge la siasa za kihuni na rushwa? Je, bado vijana hawa wana uhalali wa kisiasa na hata kimaadili, kubaki kwenye taasisi zinazopaswa kubeba taswira ya vijana wa Tanzania?

  Kama chama (taasisi mama) kupitia kwa Mwenyekiti wake kinakiri hakijui vijana hawa wamepata wapi fedha za kununuana ambazo Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuonya kuna siku tutapa Rais anayetokana na “fedha za wauza bangi”, hakika UVCCM inahitaji kutumbukia katika mgogoro kati ya waadilifu na watumiaji fedha za bangi.

  Hoja na maswali haya yanatusogeza katika busara za mwandishi wa habari na mshindi wa tuzo ya Nobel katika fasihi mwaka 1957, Albert Camus, aliyewahi kusema; mtu mwerevu ni yule ambaye akili yake inajisimamia (An intellectual is someone whose mind watches itself).

  Je, katika mtanziko wa namna hii unaochafua taswira ya UVCCM wangapi watakaojipambua kuwamo kwenye kundi la vijana werevu, wenye akili inayojisimamia?

  Kuna ukweli kwamba UVCCM kwa miaka kadhaa sasa imekuwa haina tija ya kutosha kwa CCM, sababu mbalimbali zikitajwa. Kutokana na ukweli huo, Baraza Kuu la UVCCM liliwahi kuitisha kikao na kuteua Kamati ya kupendekeza namna ya kurejesha upya mvuto wa umoja huu.

  Hata hivyo, juhudi hizo sasa zimekwishaingia dosari. Wanaopaswa kusimamia mchakato huo wa mageuzi katika UVCCM ndiyo hao ambao Mwenyekiti, Rais Kikwete amehoji; nani kawanunua?

  Hili linaweza kuwa suala jepesi kwa vijana wasiotambua umuhimu wao katika kujenga taifa lenye maadili, lakini ni suala zito na muhimu kwa wale wanaotambua umuhimu wa kujenga taifa lenye maadili.

  Nakumbuka katika kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwenye mdahalo uliosimamiwa na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, wapo vijana (akiwamo Hussein Bashe) waliohoji wazee wako wapi wakati taifa linaangamia kwa kukosa maadili.

  Inashangaza, vijana waliohoji hayo tena kwa kuwataja akina Jaji Joseph Warioba, Dk. Salim Ahmed Salim na wengine ndiyo hao walionunuliwa na kisha kuendelea kuwanunua wenzao kwa “fedha za bangi.”

  Hawa waliohoji ukimya wa wazee katika masuala ya msingi kwenye nchi leo hii licha ya ujana wao, ndiyo vinara na makuwadi wa rushwa na magenge yasiyo na maadili. Nitashangaa UVCCM kama taasisi ikivumilia makuwadi hawa, angalau kama si kuwafuta uanachama basi hata kuwaonya.

  Nape Nnauye aliwahi kutaka kunyang’anywa uanachama wa UVCCM kwa sababu tu alifichua uozo katika mkataba wa ujenzi wa jengo makao makuu ya UVCCM Dar es Salaam alipomtaja aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kuhusika. Leo hii waliohusika katika rushwa kwa nini wasichukuliwe hatua na Baraza Kuu la UVCCM?

  Vijana wa Tanzania watazame suala hili kwa umakini, aliyefichua uozo kwa kutetea uadilifu aliandamwa hata kutaka kufukuzwa, waliohusika katika rushwa watalindwa au kushughulikiwa?

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
   
 2. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Ifike wakati 'maadili' iwe ni kati ya vigezo vya kiongozi. Kuanzia ngazi ya uenyekiti wa kijiji hadi ubunge, uwaziri, ukatibu mkuu wa wizara na rais.
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nchi iko ktk mazingira magumu sana,lakini yote hii ni kuwa na mfumo wa kisiasa wenye kuzalisha viongozi mafisadi. Kwa sasa kigezo cha kwanza na muhimu cha kupata uongozi ni fedha na si kwa maana ya kutumia fedha hizo kwa maendeleo bali kwa ajili ya kununua uongozi. Hadi sasa hakuna dalili za kubadili mfumo huu na matokeo yake ni jinsi nguvu za kifisadi zinavyozidi nguvu ndogo ya uadilifu.

  Kwa sasa waadilifu wanapigana vita ya "majimaji" na mafisadi wanatumia "silaha" kali. Mafisadi wanatumia fedha (silaha) nyingi wakati wapiganaji wengi ni masikini wakitegemea 'risasi' (fedha) zigeuke maji, lakini zinawaua kama zilivyomuua Kikwete na kundi lake Dodoma. Walitegemea risasi za rashasha (fedha) zigeuke 'majimaji' wakashangaa jamaa wanawatwanga za kichwa, chali. Jambo la msingi na zito ambalo lazima tulitambue ni kwamba, sasa Taifa litaingia katika ukurasa mpya wa wakata tamaa ambao watakua hawana cha kupoteza ila njaa na dhiki katika familia zao na hivyo kufanya lolote. Hali hii si afya kwa Usalama wa Taifa letu. Mungu tunusuru.
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  huyu dilunga anajichanganya sana siku hizi,ccm imeoza yote,kikwete alisomewa risala na lowasa akawa bubu.
  ndie alikuwa anaratibu shughuli yote ya richmond lowasa akiwa chini yake,kama uvccm imenunuliwa inonyesha ndio mtiondo wa ccm siku hizi.
  unanunua kuanzia mwenyekiti mpaka mjumbe wa shina,
  kwa nini dilunga anashauri tutafute kitu kisafi jalalani?
  au anaandika kwa sababu ni kazi?
   
Loading...