Wakiristo Nchini Iraq Wanakaribia Kutoweka Kwa Kuuawa

Status
Not open for further replies.

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Askofu mkuu wa Irbil, mji mkuu wa jimbo la Iraq la Kurdistan, amewashutumu viongozi wa kikristo wa uingereza kwa kushindwa kufanya juhusi za kutosha kuilinda jamii ya inayotoweka ya Wakristo wa Iraq.
katika hojtuba aliyoitoa mjini London, Askofu Rev Bashar Warda alisema kuwa Wakristo wa Iraq sasa wanakabiliwa na hatari ya kutoweka baada ya miaka 1,400 ya kuuawa.
tangu majeshi ya marekani yalipovamia Iraq na kuuondoa madarakani utawala wa Saddam Hussein mnamo mwaka 2003, amesema, jamii ya Wakristo imepungua kwa 83%, kutoka watu milioni 1.5 hadi watu 250,000.
"Ukristo nchini Iraq," amesema , "ambao ni moja ya makanisa ya kale, kama si ya kale zaidi duniani, unakaribia kutoweka. Wengine wetu tuliobakia lazima tuwe tayari kukabiliana na kufia dini ."
Alikuwa anazungumzia tisho kubwa la hivi karibuni kutoka kwa wapiganaji wa jihadi wa Islamic State (IS) kuwa ni "vita vya mwisho vya wakristo", kufuatia mashambulizi ya awali ya kundi hilo mnamo mwaka 2014 yaliyowasambaratisha wakristo 125,000 kutoka makazi yao asilia.
"Wanaotutesa wanamaliza uwepo wetu ," alisema, "huku wakitaka kupangusa historia yetu na kuangamiza maisha yetu yajayo.
Nchini Iraq hakuna fidia kwa wale waliopoteza mali zao, nyumba wala biashara. maelfu kwa maelfu ya wakristo hawana la kuonyesha kuhusu maisha yao ya kazi, katika maeneo ambapo familia zao zimeishi, labda kwa miaka elfu moja.
Islamic State wanaofahamika katika ulimwengu wa kiarabu kama Daesh, walifukuzwa kutoka ngome yao ya mwisho ya Baghuz nchini Syria mwezi machi baada ya kushambuliwa na wanajeshi wengi wa mataifa mbali mbali na kusema kuwa ulikuwa ndio mweshi wa "mtawala wa kiislamu".
Kabla ya hapo, kundi la Islamc State lilikuwa limefukuzwa kutoka mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq wa Mosul mwezi wa Julai 2017.
Lakini makanisa , majengo ya kidini na nyumba za familia za Wakristo zimekuwa zikiangamizwa na maelfu ya familia hazijarejea tena.
Wiki hii Askofu mkuu ameonya juu ya kile alichosema kuwa ni ongezeko la makundi yenye itikadi kali yanayoamini kuwa mauaji ya Wakristo na Wayahudi yalisaidia kueneza Uislamu.
BBC
 
Kwanini usihame ?? Kwani lazima Uishi huko ?? Mbona Dunia ni likubwa

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
HUYO ASKOFU MKUU ANACHOPASWA KUFANYA NI KUWAHAMISHA HAO WAKRISTU WOTE AWALETE HUKU TANZANIA KUNA ENEO KUBWA SANA NA WATAISHI KWA AMANI NA UPENDO.
 
Wangefanya kuhama tu,wawaachie dini yao na nchi yao..

Wataanza kuuana wenyewe kwa wenyewe.
 
Walijaribu kuvaa kanzu na barakashia wakauliwa??
 
Ila Waisrael kuua waislamuPalestina ni halali?

Kila mmoja apambane na hali yake.
Wenyewe kwa wenyewe hampendani mnauana kama kuku tena kwa kutumia jina la huyo huyo mnayemuabudu halaf mnamsingizia Israel na Marekani.

Hapo Iraq mshia hawezi kukatiza mitaa ya Suni na Suni hawezi kufanya hivyo kwa Shia. Unaabisha?

Ndio maana MBS kawapa za uso wapalestina na Waislam wenzake acheni unafiki.

Nyie Watu wa ajabu sana. Pendaneni kwanza wenyewe kwa wenyewe na muache kuuana kama kuku kabla ya kuwachukia wengine kwasababu iyo dini yenu ni ya kweli na Mungu mmoja
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom