Wakiona hivi wanajisikiaje rohoni mwao?

Wakiona hivi wanajisikiaje rohoni mwao?

tafadhali msaada. kwani wakati mwalimu nyerere akiondoka madarakani tulikuwa wangapi?

attachment.php


Halafu The same country:

1. Ina madini ya kila aina (uranium,dhahabu,almasi,copper,makaa ya mawe)
2. Imezungukwa na maziwa matatu (victoria,tanganyika na nyasa)
3.ina bandari 3 (dar es salaam,mtwara na bagamoyo)
4. ina eneo la nchi (mita za mraba) kubwa
5.ina vivutio vya kitalii (kilimanjaro,serengeti,olduvai etc)
6. n.k

Nchi hii bado iko kwenye lindi la umaskini...(Haina barabara,haina maji safi,elimu mbovu etc)

Haijalishi wewe kama raia unakula nini..unaendesha gari gani..unalala wapi...kwa nje unahesabika unatoka tanzania. (LDC)

kwanini haya yote:

1. Kukosa viongozi wazalendo..kukosa viongozi wenye uchungu na nchi yao. kua na viongozi walio tayari kuuza rasilimali za nchi ili wafaidike wao..wasio na utayari wa kutimiza majukumu yao kwa uadilifu kama walivyo apa wakiwa wameshika bibilia au msaafu.

kwanini mtu ajilimbikizie mabilioni ya pesa za wananchi..ilihali tumbo lake haliwezi kumaliza hata mkate wa mia elfu moja? kwanini akaziweke fedha hizi nje ya nchi...hata asijenge hoteli basi ndani ya nchi aajiri watanzania wenzake??
hizi laana watazibebaje??

NB: Nimeona mtu akiwa karibia anakufa kwa njaa.....tanzania hii hii..ambayo wabunge wanalalamika laki 2 haiwatoshi kwa posho kwa siku..nje ya mshahara..
 
tafadhali msaada. kwani wakati mwalimu nyerere akiondoka madarakani tulikuwa wangapi?
hii list haijaekwa kwa namba kaka....imeandikwa kwa kufuata alphabet...and whether tulikua wa mwanzo..katikati au mwisho...the fact is..with all the natural resources we have..all the gifts mother nature blessed us with...bado hadi leo after 50 years of being independent....50! years bado tuko listed kwenye nchi fukara duniani
 
CCM hawakawii kuzitafsiri wanavyojua wenyewe na kusema kuwa hizo data zinaanzia kusomwa chini kupanda juu....
 
Back
Top Bottom