Wakina mama na watoto wao wa Kiume! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakina mama na watoto wao wa Kiume!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sumba-Wanga, May 6, 2011.

 1. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ni kawaida sana kwa wakina mama kutimbana na wakwe zao. Hii nimeiona live wakati nasoma sekondari, niliwahi kukaa kwa dada yangu ambaye mama mkwe wake alikuwa ni moto, na bahati mbaya shemeji alikuwa hana msimamo!

  mambo ya mama mke ni magumu sana. Mara utasikia wewe mwanamke gani hujui kumtunza mwanangu, mara hujafundwa kwenu. basi ni shida tu kati wanawake hawa wawili muhimu sana na kila mmoja ana umuhimu wake wa kipekee katika maisha ya kijana (mama na mke)! Achague wapi?

  Hapo bado hatujawagusa mawifi, hasa wale kula kulala wasio na kazi, hawajaolewa na ambao ndoa zao zimewashinda! Kaka ndio mkombozi, basi wifi yupo kikaangoni! Utasikia mwanamke mbaya sana huyu, ana roho mbaya! Anakula tu pesa ya kaka yetu, toka aolewe hatuna amani kabisa humu ndani? Jamani! Nilikuwa najiuliza sana wakati nikiaa kwa dada yangu, Si ni kwake? Mnataka kulala na kaka yetu!! Nikawa sipati picha na mimi nikiolewa mambo ni haya haya!

  Msumali wa mwisho kwenye jeneza ni pale mke asipojaliwa kupata mtoto, utasikia mwanamke gani huyo anatujazia choo tu hapa!

  Habari nzuri, baba mkwe mara nyingi anakuwa hana taabu kabisa na mwali wake, lakini mama mkwe, ni chungu!

  Jamani, hili jambo limefanya ndoa nyingi sana kuvunjia, mapenzi kupata machungu makubwa sana, watoto kuhangaika!

  Ni nini hasa jamani? tufanye nini kuwasaidia walio kwenye huo moto? Wanandoa wanawezaje kukabiriana na hali hiyo? NIna wasi wasi kuwa wengine hata kabla ya kuletewa mkwe wameshagombana nae wanamsubiri kwa hamu! Kuna mtaalamu mmoja wa saikolojia aliwahi kusema kuwa chanzo kikubwa ni mapenzi ya mama kwa mwanae wa kiume, ambayo anaona kama mwanamke mwingine anaingilia kati......? Sina hakika.

  Wa JF tuwasaidie wale waliopo kwenye janga hili. Kwa nini African families, upande wa mume wanakuwa wakorofi sana?
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Jipendekeze kwa mama mkwe na mawifi...
  Omba Mungu mume awe na msimamo....
  Wapotezeee...
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kutimbana ???? Nipe maana ya hilo neno kabla sijaanza kuchangia.
   
 4. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kulumbana, kusemana, kunangana, na kila aina ya nneo linalotumika kwenye ugomvi!
   
 5. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Hizi kesi zimekua nyingi...nadhani suluhisho ni kutafuta bwana asiye na mama na dada wakati wa engagement...na ikiwezekana mkaishi porini kuepuka kero za majirani.,..nadhani ndilo suluhisho la pekee!
   
 6. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Tehe tehe tehe, Horseshoe, Are you trying to run away from the reality????? Give us your experience!
   
 7. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Okada kuna watu hata uwatende vipi wao wana negative altitude tu...fikiria binti anaamua kuolewa kwa hiari yake,wakati huo huo kichwani ana ile mentality kwamba wakwe esp kina mama ni wakorofi na mawifi ni wafitini huyu hata apewe somo gani bado kumchange state yake ya kufikiri itakua kazi sana....nadhani hili suala la fulani ni mbaya ni suala la hisia tu binafsi of which hata km ni kweli,tumia usemi wa kale kua adui mpende,maisha yataendelea!
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ni kweli, kwenye last sentence, You have made a point!
   
 9. HekimaMoyoni

  HekimaMoyoni Member

  #9
  May 6, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio rahisi kiasi hicho..kuna mtu hata umpende, umheshimu kwa kila hali bado haachi chokochoko na kukuandama.
   
 10. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  H M hali ikifikia hapo hata aliye kando ataona...wewe una ushauri gani kwa anayeogopa kufanya commitment leo kwa kua ana dhana kua atanyanyaswa/andamwa na mama mkwe na kufitiniwa na mawifi!
   
 11. HekimaMoyoni

  HekimaMoyoni Member

  #11
  May 6, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Horseshoe, kama kuna uwezekano usiishi nao sehemu moja, hiyo ni nia ya kwanza ya kuepuka hilo tatizo..
  Jambo la msingi ni mwamamme mwenyewe kuvunja ukimya na kusema wazi lilipo tatizo ( kutoa karipia) bila kujali huyu ni mke, mama, au dada. Ukweli ni msumeno kama ilivyo sheria.
  Ndio maana kuna haja ya mwanamme kua na msimamo..
   
 12. g

  gnasha Member

  #12
  May 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachotokea ni kwamba wamama huwa wanawapenda sana watoto wao wa kiume. Na siku zote mtoto kwa mama hakui. Sasa labda kabla yule kijana hajaoa alikuwa anapeleka msaada mkubwa kwa familia yake (wazazi na ndugu zake) lakini tangu ameoa na yeye anatengeneza kwake matumizi kwa wazazi yatapungua ili aweze kujiendeleza yeye na mkewe. Wengi hapo ndipo wanapoanzia matatizo.

  Na ikitokea kijana akamchukua mama yake ili aishi naye basi huwa tabu, maana yule mama mtu anaona maisha anayoishi mwanaye sivyo, anatumia pesa vibaya na huyu mke wake, kama mama alizoea kuwa anamtengenezea mwanaye chakula vizuri lakini mke hana muda wa kupika yuko busy chakula kinapikwa na housegirl anaona pia mwanaye hatendewi haki. Anakuwa anatamani mambo yote mazuri aliyokuwa anamfanyia mwanaye akiwa mdogo aendelee kufanyiwa lakini amesahau kuwa huyu kijana ameshakuwa mtu mzima hahitaji kudekezwa kama mama alivyokuwa anamdekeza.

  Sasa na mke naye anaona anaingiliwa nyumbani kwake, mama mkwe anavyokuwa anataka kutawala nyumba. Waume wanatakiwa wawe na msimamo asisikilize upande mmoja kwasababu mke na mama wote ni muhimu kwake.
   
 13. HekimaMoyoni

  HekimaMoyoni Member

  #13
  May 6, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaudhi sana wanaume wanakua wameoa lakini mipango yote huko ndani inapangwa na mama Mkwe/Baba Mkwe na ndugu zake. Wewe unakua unapewa taarifa tu. Mengine utayasikia kwa ndugu zake kabla hata yeye hajakuambia....
   
 14. w

  warea JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wakristu wanatakiwa wawe wanajua kuwa inampasa:
  1. Mwanamme kuwaawacha baba na mama yake na kuambatana na mkewe
  2. Mwanamme ampende mkeo
  3. Mwanamke amtii mmeo
  Efeso 1-6 (Usianzie efeso 5:22, soma kuanzia sura ya 1 had ya 6)
  Kwa wale ambao bado hawajamua Yesu Kristo wanakaribishwa wampokee kwanza
   
 15. g

  gnasha Member

  #15
  May 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaudhi kweli ila uvumilivu na busara ndio vinatakiwa hapo la sivyo ndoa haitadumu
   
 16. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  aiseee, hii kwangu ni mwiko kabisa na Mungu anisaidie, kila mtu kwenye nafasi yake anatakiwa awe na mipaka yake
   
 17. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #17
  May 6, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Mie siwapendi wote wifi plus mama mkwe bahati nzuri sina
   
 18. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hehehe!
   
 19. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kwani bado kunawanao lazimishwa??
   
 20. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2011
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kujipendekeza!!!! Hapana Lizzy, kama hawakupendi, hawakupendi tu hata ujipendekezeje? bado watakuona mbaya, Ni sawa kabisa kumuomba Mungu mume awe na msimamo, na kuwapotezea ndio poa, maana utawapotezea kwa kuwatazama tu hata wafanye nini? wewe ndo mke wa kaka/mtoto wao. Ila sasa tatizo linakuja pale ambapo mama mkwe/mawifi watakapo mtafuta mtu mwingine mbadala. Hii nimewahi shuhudia, dada mmoja alikuwa anamsuka mama mkwe wa shoga yangu, sasa hivi yeye ndo kaolewa hapo, jamaa amemwacha mke wake kabisa amemuoa huyu msusi. Jamani maisha!!!! Hapana!!!!!
   
Loading...