charles ndagulla
Senior Member
- Feb 18, 2016
- 168
- 110
IDARA ya Uhamiaji Mkoani Kilimanjaro,imeanza uchunguzi kuhusiana na madai kwamba Wakili wa Serikali ofisi ya Wakili Mfawidhi Mjini Moshi,Omari Kibwana si raia wa Tanzania.
Habari kutoka Uhamiaji Kilimanjaro zilizodhibitishwa na Mkuu wa Uhamiaji Mkoa(RIO),Albert Rwelamira,zinapasha kuwa tayari jalada la uchunguzi limeshafunguliwa na wakili huyo ameshahojiwa na maofisa wa Idara hiyo.
Rwelamira amesema jukumu lao ni kuchunguza na pale wanatakapobaini kuwa si raia wa Tanzania,wanamshauri mwajiri wake kuwa mtu waliyenaye si mtu sahihi hivyo mwajiri anakuwa na jukumu la kumwajibisha.
Hata hivyo Kibwana mwenyewe anayedai amezaliwa Mkoani Tanga,amekana kuwa Raia wa Kenya bali ni Mtanzania kwa kuzaliwa licha ya ukweli kwamba amekulia na kusomea nchini Kenya.
Habari kutoka kwa watu waliokaribu na Kibwana zinadai kuwa,hajawahi kuukana uraia wa Kenya