GE2025 Wakili wa Mahakama Kuu, Tumsifu Kweka achukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Siha

GE2025 Wakili wa Mahakama Kuu, Tumsifu Kweka achukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Siha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM kutoka mkoa wa Kilimanjaro na Wakili wa Mahakama kuu Bw. Tumsifu Kweka, leo Jumanne Julai Mosi, 2025, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya uteuzi wa kugombea ubunge katika Jimbo la Siha, akiahidi kuendeleza maendeleo ya wananchi na kusimamia itikadi ya chama endapo Chama chake kitampitisha.

Wakili Kweka amesema ametimiza haki yake yakidemokrasia ndani ya chama kwa kuchukua fomu ya kuwania ubunge katika Jimbo hilo, akiwaomba wananchi wa Siha kumpatia fursa ya kuwawakilisha na kushirikiana nao ili kuleta maendeleo katika jimbo la Siha.

Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha amebainisha kuwa anatosha katika nafasi hiyo kutokana na uzoefu alionao pamoja na kuzijua fursa na changamoto za Jimbo hilo,akieleza kuwa amepata fursa ya kuisoma ilani ya CCM ya mwaka 2025/30 na hivyo inahitaji mtu ambae anaweza kukimbizana na maendeleo ya nchi lakini pia yeye sio muumini wa siasa za maneno bali yeye ni muumini wa siasa za vitendo.

Screenshot 2025-07-01 232419.png
 
Back
Top Bottom