Wakili wa kujitegemea Tumsifu Kweka, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, leo amejitokeza rasmi kuchukua fomu za kuwania ubunge katika Jimbo la Siha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kweka alifika katika Ofisi za CCM wilaya ya Siha asubuhi ya leo akiwa ameongozana na mkewe, katika tukio lililoshuhudiwa na wanachama na wafuasi wa chama hicho, huku akipokelewa kwa shangwe na matumaini kutoka kwa baadhi ya wananchi waliohudhuria
Hatua ya Kweka kuingia katika kinyang’anyiro hicho inaongeza ushindani ndani ya CCM katika safari ya kutafuta mgombea atakayebeba bendera ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025
Soma pia:
www.jamiiforums.com
Akizungumza kwa kifupi baada ya kuchukua fomu, Wakili Kweka alieleza kuwa amesukumwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Siha kwa kutumia weledi wake katika sheria na uzoefu wa kisiasa alionao ndani ya chama.
“Ni wakati wa kuunganisha nguvu za kijamii, kiuchumi na kisheria kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Siha,” alisema Kweka
Zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu linaendelea katika ofisi za CCM wilayani humo, huku wanachama na wafuasi wakifuatilia kwa karibu majina ya watia nia wanaojitokeza kutaka kuwania nafasi ya ubunge kupitia chama hicho tawala

PreGE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Habari Wakuu, Ili kuzifikia nyuzi hizi kirahisi, hapa utapata orodha yote ya mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kwenye ushiriki wa Uchaguzi Mkuu 2025, ambamo ndani yake utapata links za matukio yote yanayojiri katika mikoa husika mpaka kufikia kwenye uchaguzi wenyewe, matokeo ya uchaguzi huo...