GE2025 Wakili Patrick Malogoi arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Geita kupitia CCM

GE2025 Wakili Patrick Malogoi arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Geita kupitia CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Wakili Msomi kutoka ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali, Patrick Stephen Malogoi amerejesha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Geita kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hii ni mara ya pili kwa wakili Malogoi kuomba ridhaa ya CCM ambapo katika kura za maoni za mwaka 2020 na kushika nafasi ya pili akimfuata Joseph Kasheku (Musukuma) aliyeshika nafasi ya kwanza na baadaye akapitishwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo hilo na kushinda uchaguzi.

Wakili Malogoi ameweka wazi kuwa zoezi la uchukuaji fomu kwa wilaya ya Geita linaendelea vizuri na yupo tayari kuchuana na watia nia wengine wa jimbo la Geita (Geita vijijini) akiwemo mbunge anayemaliza muda wake, Joseph Kasheku (Msukuma).

 
Ni mbunge anaemaliza muda wake au ni mbunge aliyemaliza muda wake,
tuwekane sawa
 
Mropokaji wa darasa la saba muda wake wa kukaa bungeni umeisha.
 
Kashenku aangalie biashara zake kwa sasa jimbo linaenda kupata mbunge mpya
 
Back
Top Bottom