PostGE2025 Wakili Mwasipu: Ombi la kufungua maombi ya msingi yamekubaliwa, maombi ya tume ya uchunguzi kusitisha shughuli zake yamekataliwa

PostGE2025 Wakili Mwasipu: Ombi la kufungua maombi ya msingi yamekubaliwa, maombi ya tume ya uchunguzi kusitisha shughuli zake yamekataliwa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

ChekoFagia

Senior Member
Joined
Sep 20, 2025
Posts
115
Reaction score
339
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam imewaruhusu waleta maombi kufungua kesi ya msingi, katika shauri namba 30210/2025 linalohusu kupinga uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteua Tume Huru ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani nchini yaliyotokea Oktoba 29 mwaka huu na siku zilizofuata

Hata hivyo, licha ya Mahakama kuruhusu waleta maombi kufungua kesi msingi ndani ya siku 14 kuanzia leo, lakini imekataa ombi la kuzuia kwa muda shughuli za Tume hiyo hadi pale kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi

Katika uamuzi wake uliosomwa leo, Alhamisi Desemba 18.2025 na Naibu Msajili wa Mahakama Hussein Mushi kwa niaba ya Jaji Hussein Salum Mtembwa aliyekuwa anasikiliza maombi hayo, Mahakama imesema imesema kila upande utabeba gharama zake

Katika shauri hilo lililoendeshwa leo kwa njia ya mtandao, upande wa Jamhuri ukihuhusisha wajibu maombi wa kwanza ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Wajumbe wote Nane wa Tume hiyo wakiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman ulikuwa unakilishwa na Wakili wa Serikali Waandamizi Daniel Nyakia na Wakili wa Serikali Erigh Rumisha, mjibu maombi wa 10 ambaye ni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimewakilishwa na Wakili Ferdinand Makore, wakati waleta maombi ambao ni Rosemary Mwakitwange, Edward Heche na Deogratias Mahinyila wamewakilishwa na Wakili Hekima Mwasipu

Akizungumza na Jambo TV, muda mfupi baada ya uamuzi huo Wakili Hekima Mwasipu amesema kwa niaba ya wateja wao wamepokea uamuzi huo kwa moyo mkunjufu, na kwamba watatekeleza maagizo ya Mahakama ndani ya muda waliopewa

Hata hivyo, Wakili Mwasipu amesema watafungua kesi hiyo kwa hati ya dharura, na kwamba watawasilisha tena maombi Mahakamani hapo kuomba Tume hiyo izuiliwe kwa muda kufanya kazi hadi hapo kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi

Akizungumza kwa niaba ya TLS, Wakili Ferdinand Makore amesema wao wamepokea uamuzi huo kwa mikono miwili, na kwamba katika maombi hayo wamehakikisha wanasimama upande wa waleta maombi, lakini pia amesema haoni tatizo lolote litakalosababisha kesi hiyo 'ivurugike' licha ya kwamba Tume husika inaendelea na kazi.

Pia Soma: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025
 
Ile tume haina tofauti na necccm, lengo kuu ni kumsafisha samuya dhidi ya mauaji aliyofanya!.
 
Sijawahi kuona Tume iliyopuuzwa karma hii, Hivi Ndugu Othman Chande ile Tume ya Haki Jinai iliishia Wapi?
Ni vyema sana kukusoma tena.
Nilifikiri umechomewa utambi na yule Mnyarwanda 'Imhotep' maana mambo yake yalibadilika sana; na sasa kapotea tena, bila shaka kapewa kidawati mahali fulani kwenye hii HARAMU.

Sasa nina hofu kubwa ya Mzee pekee aliyebaki na heshima, mzee Warioba naye kutengenezewa nafasi ya kusafisha uchafu wa hawa mashetani.
 
Muhimu tu hao washtaki na wakili wao msomi kuanzia sasa waishi kwa tahadhari kubwa. Maana wahuni siyo watu wazuri hata kidogo. Ukiingia tu kwenye 18 zao, wanakupoteza kwa njia yoyote ile.
 
Back
Top Bottom