Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Wakili msomi Joseph Kinango amesema tamko la Waziri Mwakyembe kuwa ataifuta TLS ni batili na halina mashiko kisheria. Kwa lugha ya kisheria "Its null and void abinitio" yani ni tamko batili hata kabla Mwakyembe hajalitamka. Yani wakati Mwakyembe anafikiria kutamka tayari lilikua batili.
Hii ni kwa sababu ili ufute TLS inabidi ufute sheria inayoanzisha TLS (The Tanganyika Law Society Act). Na sheria hiyo haiwezi kufutwa kienyeji. Inabidi ipelekwe bungeni na bunge liifute. Ikitokea hivyo athari zake ni kama ifuatavyo:
1. Mawakili wote nchini wanapoteza uhalali wa kuwa mawakili, maana sifa mojawapo ya kuwa wakili ni kuwa member wa TLS.
2. Sheria takribani 200 zinazotaja au kutambua uwepo wa mawakili inabidi zifutwe au zifanyiwe marekebisho ili kuondoa application ya mawakili katika sheria hizo.
3. Bodi za taasisi kadhaa nchini inabidi zifanyiwe marekebisho maana kuna bodi ambazo Rais wa TLS ni mjumbe.
4. Sifa za kumpata Gavana wa BOT inabidi zibadilishwe maana moja ya watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Gavana ni pamoja na Wakili wa mahakama kuu.
5. Sifa za kuwapata majaji nchini inabidi ziwe reviewed maana mojawapo ya sifa ni kuwa wakili wa mahakama kuu (na mahakama zilizopo chini yake).
6. Chuo cha mafunzo ya sheria (School of Law) kinachofunza na kuandaa mawakili inabidi kifungwe maana hakitakuwa na tija tena kwa nchi.
[HASHTAG]#NiniKifanyike[/HASHTAG]:
1. Tamko la Waziri Mwakyembe linafaa kupuuzwa. Halina mantiki.
2. Waziri Mwakyembe avuliwe ujumbe wa TLS. Haiwezekani aendelee kuwa mjumbe wa Taasisi ambayo anafikiria kuifuta.
So jambo la kwanza kwa mawakili wakifika Arusha tar 17 March, kabla ya kupiga kura ya kumchagua Lissu kuwa Rais wao, wanapaswa wapige kura ya kumfuta uanachama wa TLS Mwakyembe.