GE2025 Wakili Kulanga: Wananchi endeleeni kujitokeza kupiga kura

GE2025 Wakili Kulanga: Wananchi endeleeni kujitokeza kupiga kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Moshi Mjini, Wakili Sifaeli Kulanga, ametoa tathmini ya mwenendo wa zoezi la kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.Akizungumza Wakili Kulanga amesema, vituo vyote vimefunguliwa na kuwataka wananchi kufika kwenye vituo kwa lengo la kupiga kura na kutimiza haki yao ya kisheria.

Pia Wakili Kulanga pia aliwahimiza wananchi kuzingatia taratibu na masharti yaliyowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuendeleza uchaguzi huru, wa haki, na wa uwazi.Wananchi wa Moshi Mjini wameendelea kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura, wakionyesha mshikamano na kuheshimu taratibu zilizowekwa.
 
Back
Top Bottom