Wakili: DOWANS itadhoofisha nchi

Angalia wanasheria wa Tanzania walivyo. Huyu Fungamtama alikuwa akijidai kuzungumzia shauri hili kama raia wa kawaida aliyejua lolote kuhusu kesi hiyo. Akajifanya kutoa ushuri kuwa ni lazima serikali ilipe pesa hizo kwa sababu makosa yalifanywa na watu walioitetea TANESCO, leo hii ndiye anayepeleka nakala ya hukumu hiyo mahakamani kusajiliwa ili apate mshiko wake:

 
Fungamtama ana maslahi binafsi katika kesi hii wakati Sitta anatetea maslahi ya watanzania wote! Watu kama Fungamtama hawatakiwi kwenye jamii kabisa. ICC haiwezi kupuuza kuhusu mmiliki wa Dowans hizo ni propaganda za Fungamtama tu! Pamoja na kwamba company ni legal person lazima wamiliki wake wajulikane pia! Issue iliyopo hapa ni kwanini Dowans iwe na uhalali wa ku-contract wakati ilii-rith Company hewa ya Richmond? Kama kamati ya bunge iliona Richmond ni company hewa, inawezekanaje Dowans iwe halali? Zote Richmond na Dowans ni company hewa!! Wabaya wetu wakubwa ni akina Fungamtama wanaoweka maslahi yao binafsi mbele na inabidi washughulikie!
 
Mimi ninapendekeza, hata kabla ya kuwatafuta wamiliki wa Dowans, kwanza tuambiwe washiriki wote kwa upande wa serikali na tanesco walio ridhia madudu yote haya yaliyo tokea. tujue majina yao na walishiriki vipi ! tuwafunge kwanza hawa na kuwafilisi mali zao zote na kisha tumjue mmiliki wa hiyo Dowans, manake hawa tutakao wafilisi na kuwafunga lazima watakuwa wanamjua mmiliki. haiwezekani nchi iingie kwenye utata wa kiasi hiki na kusiwe muwajibikaji wa kuadhibiwa !! au wahusika walio liingiza taifa hili kwenye utata huu nao hawajulikani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…