Wakili Alphonce Nachipyangu Ajitoa Kesi ya Wanafunzi wa KIU

Jan 3, 2017
11
38
WAKILI NACHIPYANGU AJITOA KESI YA WANAFUNZI WA 'KIU' WANAODAIWA KUMVISHA HIJABU RAIS JOHN MAGUFULI
_____________________________________________

Na #Mwenda ND,

Kesi ya Jinai Namba 65/2016, Kati ya Jamhuri dhidi ya Amenata Harold Konga na wenzake watatu (3) imeendelea Jumatatu ya wiki hii ya tarehe 6 Agosti 2019 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Ilala Mheshimiwa Kiyoja

Kesi hiyo ambayo imedumu kwa muda wa miaka mitatu ni ile ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), kilichopo Gombo la Mboto, Dar Es Salaam, ambapo Amenata Harold Konga na wenzake wote wanafunzi wa KIU wanatuhumiwa kumvisha Rais John Magufuli HIJABU, katika picha zinazodaiwa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji, Shahidi namba moja wa Jamhuri (PW 1) Afande Betrice aliendelea siku ya Jumanne kutoa ushahidi wake kwamba yeye pamoja na mwenzake Afande Telesphory walizikamata simu za washitakiwa wote wanne na aliomba simu ya mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo, Bi. Ameneta Konga iingizwe kama ushahidi Mahakamani!.

UTATA WA KISHERIA, Wakati Wakili wa Jamhuri akimuongoza Shahidi (Afande Beatrice) kuitoa simu hiyo kama ushahidi, Wakili wa Utetezi, Alphonce Nachipyangu alipinga vikali kwa hoja mbili juu ya hatua hiyo!

Hoja ya Kwanza, Wakili Alphonce Nachipyangu aliiambia Mahakama kwamba hakukubaliani na uamuzi wa simu hiyo iwe sehemu ya ushahidi, kwani Mahakama hiyo hiyo siku ya tarehe 23 Novemba 2017 ilikubali pingamizi la Wakili Peter Kibatala kwamba Jamhuri ilipaswa kumuongoza Shahidi wao Afande Betrice kutoa kwanza nyaraka ya kushikilia (Certificate of Seizure) simu hiyo ndipo baadae upande wa Jamhuri uilete simu hiyo kama ushahidi na iombe ipokelewe lakini hawakufanya hivyo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Kiyoja alikubaliana na pingamizi hilo na akakataa kwani hawakufuata utaratibu (Procedure) upande wa mashitaka. Hivyo tangu awali simu za watuhumiwa hazikuwa sehemu ya ushahidi kwneue kesi hiyo.

Wakili Alphonce Nachipyangu aliikumbusha Mahakama kuwa, Kanuni ya kisheria iitwayo "FUNCTUS OFFICIO " ikiwa na maana 'Mahakama haiwezi kubadili ilichokiamua yenyewe'. Hivyo akatoa suluhu kuwa, suluhisho la utata huo, upande wa Jamhuri ulipaswa kukata rufaa Mahakama Kuu katika jambo hilo kama haikuridhika na sio kuzunguka upande mwingine na kulete tena simu hizo ambazo hapo awali ziliwekewa pingamizi na watu wale wale, Mahakama ileile , Hakimu yule yule jambo ambalo lilikuwa haliwezekani!

Akijibu hoja hiyo Wakili wa Serikali, Anne Chimpa alidai kwamba Mahakama haiwezi kataa kwani ilichokitaka wametekeleza. Hata hivyo Wakili wa upande wa utetezi, Wakili Alphonce Nachipyangu aliongeza hoja ya pili kuwa, Mahakama Kuu ambayo ikitoa uamuzi basi Mahakama hiyo (Mahakama ya Wilaya na Mahakama zote zilizo chini) haina namna zaidi ya kuufuata maamuzi hayo.

Mahakama Kuu ilitoa uamuzi katika 'Kesi Namba 6/2015' ambayo ni ya Bw. Emmanuel Godfrey Masonga dhidi ya Edward Franz Mwalongo na wengine wawili kesi iliyoamuliwa na Jaji Mwambegele (Mahakama Kuu Kanda ya Iringa) alifafanua kwamba ushahidi wowote wa kielekitroniki lazima uambatane na hati ya kiapo (AFFIDAVIT) ambayo itaeleza mambo mbalimbali juu ya kifaa husika kama vile, aina ya kifaa hicho, utumiaje wake, aliyetumia na namna mbalimbali zilivyofanyika kabla haijaletwa Mahakamani.

Pia Wakili Nachipyangu aliongeza kuwa, kukosekana kwa hati hiyo kunafanya kielelezo (simu za watuhumiwa) hicho kisiwe na sifa ya kupokelewa kama ushahidi Mahakamani hapo.

Wakili wa upande wa Jamhuri Anne Chimpa wakati anajibu hoja hiyo aliieleza Mahakama kuwa, hajasoma vizuri uamuzi huo lakini kwa maoni yake simu sio kifaa cha kielekitroniki, vifaa vya kielekitroniki ni kama vile CD na VCD.

Hata hivyo baada ya malumbano hayo ya kisheria, Hakimu Mkazi alitoa uamuzi kuwa ameyakataa mapingamizi (ya upande wa utetezi ya kuzuia simu isiingie kama ushahidi) hayo hivyo kesi iendelee ambapo Wakili wa utetezi hakukubaliana na uamuzi wa Hakimu.

Baada ya Hakimu kudai kesi iendelee, Wakili wa utetezi Alphonce Nachipyangu alimwambia Hakimu kuwa hakubaliani na maamuzi hayo hivyo anatoa notisi ya rufaa na anaiomba Mahakama isubiri jambo hilo liamuliwe na kutolewa tafsiri na Mahakama Kuu.

Hata hivyo Hakimu alimweleza Wakili wa utetezi (Wakili Nachipyangu) afuate utaratibu ila yeye ataendelea na kesi. Ndipo Wakili Alphonce Nachipyangu akaieleza Mahakama kuwa anaona anaweka rehani HAKI ZA WATEJA WAKE hivyo anajitoa katika kesi hiyo.

Nao washitakiwa walipoulizwa kama wataweza kuendelea na kesi hiyo walidai hawawezi kuendelea bila Wakili na hivyo wakaomba watafute Wakili mwingine wa kuwatetea. Kesi hiyo iliahairishwa tena mpaka tarehe 20 Agosti 2019 kwaajili ya kuendelea na usikilizaji!
IMG_20190808_114332_018.jpeg
 
Mh. Kiyoja ni mweupe sana kichwani. Hana analolijua. Na ni hakimu ambaye anaongoza kwa kutoa hukumu ambazo hazina misingi ya haki hata kidogo kwa sababu hajui Sheria waka she doesn't take any effort kufuatilia marekebisho ya Sheria na precedents.
 
Wakili wa upande wa Jamhuri Anne Chimpa wakati anajibu hoja hiyo aliieleza Mahakama kuwa, hajasoma vizuri uamuzi huo lakini kwa maoni yake simu sio kifaa cha kielekitroniki, vifaa vya kielekitroniki ni kama vile CD na VCD

Wakili wa Jamhuri huyu
 
Hata huyo chimpae si yule state attorney mweusi sura mbovu...ni mtupu kichwani yani hamna kitu!
Nilishawai kumburuzaga kwenye kesi moja nikawachanganya yeye na huyo hakimu
Mh. Kiyoja ni mweupe sana kichwani. Hana analolijua. Na ni hakimu ambaye anaongoza kwa kutoa hukumu ambazo hazina misingi ya haki hata kidogo kwa sababu hajui Sheria waka she doesn't take any effort kufuatilia marekebisho ya Sheria na precedents.
 
WAKILI NACHIPYANGU AJITOA KESI YA WANAFUNZI WA 'KIU' WANAODAIWA KUMVISHA HIJABU RAIS JOHN MAGUFULI
_____________________________________________

Na #Mwenda ND,

Kesi ya Jinai Namba 65/2016, Kati ya Jamhuri dhidi ya Amenata Harold Konga na wenzake watatu (3) imeendelea Jumatatu ya wiki hii ya tarehe 6 Agosti 2019 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Ilala Mheshimiwa Kiyoja

Kesi hiyo ambayo imedumu kwa muda wa miaka mitatu ni ile ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), kilichopo Gombo la Mboto, Dar Es Salaam, ambapo Amenata Harold Konga na wenzake wote wanafunzi wa KIU wanatuhumiwa kumvisha Rais John Magufuli HIJABU, katika picha zinazodaiwa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji, Shahidi namba moja wa Jamhuri (PW 1) Afande Betrice aliendelea siku ya Jumanne kutoa ushahidi wake kwamba yeye pamoja na mwenzake Afande Telesphory walizikamata simu za washitakiwa wote wanne na aliomba simu ya mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo, Bi. Ameneta Konga iingizwe kama ushahidi Mahakamani!.

UTATA WA KISHERIA, Wakati Wakili wa Jamhuri akimuongoza Shahidi (Afande Beatrice) kuitoa simu hiyo kama ushahidi, Wakili wa Utetezi, Alphonce Nachipyangu alipinga vikali kwa hoja mbili juu ya hatua hiyo!

Hoja ya Kwanza, Wakili Alphonce Nachipyangu aliiambia Mahakama kwamba hakukubaliani na uamuzi wa simu hiyo iwe sehemu ya ushahidi, kwani Mahakama hiyo hiyo siku ya tarehe 23 Novemba 2017 ilikubali pingamizi la Wakili Peter Kibatala kwamba Jamhuri ilipaswa kumuongoza Shahidi wao Afande Betrice kutoa kwanza nyaraka ya kushikilia (Certificate of Seizure) simu hiyo ndipo baadae upande wa Jamhuri uilete simu hiyo kama ushahidi na iombe ipokelewe lakini hawakufanya hivyo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Kiyoja alikubaliana na pingamizi hilo na akakataa kwani hawakufuata utaratibu (Procedure) upande wa mashitaka. Hivyo tangu awali simu za watuhumiwa hazikuwa sehemu ya ushahidi kwneue kesi hiyo.

Wakili Alphonce Nachipyangu aliikumbusha Mahakama kuwa, Kanuni ya kisheria iitwayo "FUNCTUS OFFICIO " ikiwa na maana 'Mahakama haiwezi kubadili ilichokiamua yenyewe'. Hivyo akatoa suluhu kuwa, suluhisho la utata huo, upande wa Jamhuri ulipaswa kukata rufaa Mahakama Kuu katika jambo hilo kama haikuridhika na sio kuzunguka upande mwingine na kulete tena simu hizo ambazo hapo awali ziliwekewa pingamizi na watu wale wale, Mahakama ileile , Hakimu yule yule jambo ambalo lilikuwa haliwezekani!

Akijibu hoja hiyo Wakili wa Serikali, Anne Chimpa alidai kwamba Mahakama haiwezi kataa kwani ilichokitaka wametekeleza. Hata hivyo Wakili wa upande wa utetezi, Wakili Alphonce Nachipyangu aliongeza hoja ya pili kuwa, Mahakama Kuu ambayo ikitoa uamuzi basi Mahakama hiyo (Mahakama ya Wilaya na Mahakama zote zilizo chini) haina namna zaidi ya kuufuata maamuzi hayo.

Mahakama Kuu ilitoa uamuzi katika 'Kesi Namba 6/2015' ambayo ni ya Bw. Emmanuel Godfrey Masonga dhidi ya Edward Franz Mwalongo na wengine wawili kesi iliyoamuliwa na Jaji Mwambegele (Mahakama Kuu Kanda ya Iringa) alifafanua kwamba ushahidi wowote wa kielekitroniki lazima uambatane na hati ya kiapo (AFFIDAVIT) ambayo itaeleza mambo mbalimbali juu ya kifaa husika kama vile, aina ya kifaa hicho, utumiaje wake, aliyetumia na namna mbalimbali zilivyofanyika kabla haijaletwa Mahakamani.

Pia Wakili Nachipyangu aliongeza kuwa, kukosekana kwa hati hiyo kunafanya kielelezo (simu za watuhumiwa) hicho kisiwe na sifa ya kupokelewa kama ushahidi Mahakamani hapo.

Wakili wa upande wa Jamhuri Anne Chimpa wakati anajibu hoja hiyo aliieleza Mahakama kuwa, hajasoma vizuri uamuzi huo lakini kwa maoni yake simu sio kifaa cha kielekitroniki, vifaa vya kielekitroniki ni kama vile CD na VCD.

Hata hivyo baada ya malumbano hayo ya kisheria, Hakimu Mkazi alitoa uamuzi kuwa ameyakataa mapingamizi (ya upande wa utetezi ya kuzuia simu isiingie kama ushahidi) hayo hivyo kesi iendelee ambapo Wakili wa utetezi hakukubaliana na uamuzi wa Hakimu.

Baada ya Hakimu kudai kesi iendelee, Wakili wa utetezi Alphonce Nachipyangu alimwambia Hakimu kuwa hakubaliani na maamuzi hayo hivyo anatoa notisi ya rufaa na anaiomba Mahakama isubiri jambo hilo liamuliwe na kutolewa tafsiri na Mahakama Kuu.

Hata hivyo Hakimu alimweleza Wakili wa utetezi (Wakili Nachipyangu) afuate utaratibu ila yeye ataendelea na kesi. Ndipo Wakili Alphonce Nachipyangu akaieleza Mahakama kuwa anaona anaweka rehani HAKI ZA WATEJA WAKE hivyo anajitoa katika kesi hiyo.

Nao washitakiwa walipoulizwa kama wataweza kuendelea na kesi hiyo walidai hawawezi kuendelea bila Wakili na hivyo wakaomba watafute Wakili mwingine wa kuwatetea. Kesi hiyo iliahairishwa tena mpaka tarehe 20 Agosti 2019 kwaajili ya kuendelea na usikilizaji!View attachment 1175366
Ukiweza kuweka na hiyo picha ya muheshimiwa kavaa ijabu itapendeza zaidi
 
Back
Top Bottom