Wakenya Wanae James Orengo Watanzania Tunae Tundu Lissu !!

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Wakati kenya Wanahangaika Kujenga Taasisi Imara Tanzania Tunahangaika Kumjenga Mtu Imara, Maendeleo Tutayasikia Kwa Jirani Tu!!

uamuzi wa Supreme Court ya Kenya ni ushindi mkubwa kwa wapigania demokrasia kila mahali duniani na kwetu pia.

Uamuzi huo umetokana na Kenya kuwa na Mahakama iliyo huru na isiyokuwa na hofu, woga wala upendeleo katika utendaji wake wa haki.

Mahakama hiyo huru imetokana na Kenya kuwa na Katiba Mpya ya kidemokrasia ya mwaka 2010.

Katiba hiyo ilipunguza na au kudhibiti mamlaka ya Rais wa Kenya, na ilimaliza utawala wa kiimla uliodumu Kenya kwa karibu nusu karne.

Kwetu sisi uamuzi huu ni fundisho kubwa sana.

Tunahitaji demokrasia itakayoondoa utawala wa kidikteta katika Tanzania pia.

Tunahitaji Katiba Mpya itakayolinda haki za binadamu, kuleta utawala wa sheria na kuondoa utawala wa amri za majukwaani na bomoa bomoa.

Ili kupatikana kwa demokrasia hiyo, tunahitaji Katiba Mpya.

Katiba Mpya itakayopunguza na kudhibiti Urais wa Kifalme ambao umekuwa 'organizing principle' ya Katiba yetu tangu mwaka 1962.

Katiba Mpya itakayoiweka huru Mahakama ya Tanzania, ambayo leo haina hata Jaji Mkuu, na kuwatoa hofu majaji wetu.

Katiba Mpya itakayowawezesha watawaliwa kuwadhibiti na kuwaadabisha watawala, wanaojigeuza miungu watu mara wakishaingia madarakani.

Kwa hiyo, pamoja na kuwa urais uliotenguliwa ni wa mgombea tuliyemuunga mkono, hatuna budi kushangilia ushindi huu wa utawala wa sheria na uhuru wa mahakama.

Na, bora zaidi, hatuna budi kuyafanyia kazi mafundisho ya demokrasia ya Kenya: Katiba Mpya na ya kidemokrasia.

Katiba Mpya ya Kenya haikujileta. Ililetwa kwa jitihada, jasho na damu ya waKenya. Katiba Mpya ilipiganiwa, ilidaiwa na, baada ya kupatikana, imelindwa.

Na kwetu lazima iwe hivyo hivyo. Haitapatikana kwa kuombewa makanisani au misikitini tu. Itapatikana kwa kudaiwa mitaani na barabarani na Mahakamani na kila mahali.

Haitapatikana kwa vigelegele na vicheko. Itapatikana kwa vilio vya wanaodai haki na wanaokandamizwa.

Hebu na tujielekeze katika kazi ngumu na muhimu iliyoko mbele yetu. Kazi ya kudai Katiba Mpya.
-----------------------------------------------------------------------
Tanzania na Kenyat wote tu-nchi masikini, lakini umasikini wetu ni wa akili zaidi kuliko mali. Tusipobadilika Kenya wataendelea kutuacha sana.

mr mkiki.
 
Je unakubaliana na maneno ya Uhuru, juu ya kile atafanya baada ya uchaguzi kwisha hapo 1 Novemba, 2017 ikiwa atashinda hasa kwa majaji na wanasheria waliohusika na maamuzi hayo?
 
Tudsu lisu unaye wewe na Babako usitake kutuhusisha Watanzania wote na huo mkosi!
 
Manyumbu utayajua tu kutokuwa na dira. Juzi tu bwana yenu Lowasa alipiga kampeni na kusema chadema IPO nyuma ya Rais Kenyatta mkasema uchaguzi ni Wa kidemokrasia. Leo upepo umegeuka mnapongeza kutenguliwa uchaguzi wakati mlisifia ni Wa kidemokrasia. Shame on you!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada nimesoma kichwa cha habari tu unamkosea sana Orengo kumfananisha na huyu jamaa aliyekataa kupimwa mkojo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mawakili wengi Tanzania akiwemo lisu hawana viwango vya orengo. Orengo Hana mihemuko Kama lisu au wengi wa mawakili wetu yuko composed halazimishi hoja kwa kuitisha maandamano na migomo Kama lisu na mawakili uchwara WA upinzani anajikiita kwenye hoja za kisheria tu. Hahangaiki na kuuza sura kwenye press Kama Lisu and company anapambana kortini tu huwezi linganisha na wauza sura kwenye press Kama Lisu. Tuombe samahani kumfananisha lisu na orengo. Please
 
Hivi jaman wazee wakudai demokrasia bongo tushike kipi ambacho tunapambana nacho mbona mnatuyumbisha 1.kupambana na udictetor
2 katiba
3 mikutano huru
4maandamano
N.K mbona hatueleweki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una
Manyumbu utayajua tu kutokuwa na dira. Juzi tu bwana yenu Lowasa alipiga kampeni na kusema chadema IPO nyuma ya Rais Kenyatta mkasema uchaguzi ni Wa kidemokrasia. Leo upepo umegeuka mnapongeza kutenguliwa uchaguzi wakati mlisifia ni Wa kidemokrasia. Shame on you!

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajaribu kitu kigumu sana. Kuwauliza Nyumbu wetu wapendwa, kwao wapi? Serengeti au Masai Mara halafu unategemea jibu.
 
Back
Top Bottom