Hamjambo wana JF. Mie ni mwananchi wa Kenya na nina nia ya kuchangia mabadiliko kwenye sekta ya elimu nchini Kenya. Jambo la kwanza ambalo ningependa kuangazia ni lugha inayotumika kuwafundishia watoto.
Naamini kuwa ni vyema mtoto afundishwe kwa lugha anayoielewa vyema. Kwa maoni yangu, lugha Kamilifu (ideal,) ni ile ya mama; lakini ile inayowezekana (practical) ni lugha ya Kiswahili. Ingawa sera ya Wizara ya elimu ni kuwa lugha ya mama itumike vijijini na ile ya Kiswahili au kiingera vitumike mijini hadi darasa la tatu, hakuna vitabu vyovyote ambavy vimeandikwa kwenye lugha hizi. Jambo la ajabu ni kuwa hata yale makampuni ya kuchapisha vitabu ambavyo vinamilikiwa na serikali, Kama vile the Kenya Literature Bureau, na The Jomo Kenyatta Foundation, vinatoa vitabu ambavyo vimeandikwa kwa kiingeraza, isipokuwa vile vitabu vinavyo fundisha lugha hiyo kama somo.
Kwa hivyo, ninataka niandike vitabu vya darasa la kwanza vya Sayansi, Somo la Jamii, Somo La Dini (Christian Religious Education,) na Hesabu. Niko na changamoto kadhaa;
1. Mara nyingi mie nimehusiana na watoto na hao huniambia kuwa wana shida kusoma katika lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu Kiswahili, ingawa ni 100% phonetic, ni lugha amalgamated na kwa hivyo huwa na maneno marefu sana. Je, wale wantanzania ambao mlisomea lugha ya Kiswahili katika shule za msingi, kati ya kusoma kiingereza ambacho si 100% phonetic lakini sio amalgamated na kusoma Kiswahili ambacho ni 100% phonetic lakini ni amalgamated; ni gani heri?
2. Kwa watanzania waliotumia Kiswahili katika shule ya msingi, mlipoenda katika shule za upili, mlipata shida yoyote kuelewa vitabu vya kiingereza? Je, ikiwa ulipata shida hii, utailaumu medium of instruction ama utailaumu shule yako/mwalimu wako?
3. Kuna shida ya rote memorization katika shule nyingi za Kenya; naamini hii ni kwasababu ya kutumia lugha ya kiingeraza. Huko Tanzania, shida hii imekithiri? Na wale wlioelewa wakiwa shule ya msingi, walipofika shule za upili, walizidi kuelewa au walianza kukariri wasioelewa (intellectual vomit?)
4. Shule zinazotumia kiingereza (English medium) hao hufanya mtihani wa darasa la saba kwa kiingereza au Kiswahili?
5. Kuna software gani ya bure inayotumika kuhadhiri maandishi katika lugha ya Kiswahili?
6. Kwa mkenya ulio hapa, reaction yako itakuwa ipi ukiambiwa kuwa medium of instruction imebadilishwa hadi Kiswahili?
Asanteni sana kwa maoni yenyu.
P.S. Nitapachika hapa kijitabu ambacho natayari na nitaomba maoni yenyu