Wakazi wa maeneo ya IPOIPO kuelekea Kihonda Sekondari tunaendelea kupata adha kubwa kutokana na hali mbaya ya barabara hii.
Mvua ikinyesha hali inakuwa mbaya zaidi — magari, bajaji na pikipiki hupata shida kupita, na wakati mwingine usafiri husimama kabisa.
Wananchi tunapata mateso kila siku wakati wa kwenda kazini, shuleni na kwenye shughuli zetu za maisha.
Tunaomba viongozi na mamlaka husika muisikie sauti ya wananchi na mtusaidie kurekebisha barabara hii ili kurahisisha usafiri na kuondoa mateso yasiyo ya lazima.
Barabara imekua mbovu kwa muda hata kabla ya uchaguzi. Kuna kipindi magreda yalikuja kama geresha then yaliondolewa bila kazi yoyote kufanyika. Barabara hii ni kubwa inaunganisha barabara ya kwenda iringa na dodoma
Na imekua kimbilio kwa watu wanaokwepa barabara ya msamvu kwa kuwa inakua na foleni ya malori na magari
Ni kipande kidogo tu ila ni kimya. Barabara haina taa za barabarani na usiku ni giza.
Source: Habari Morogoro