Wakazi wa eneo la Iloganzila Kibamba wabomolewa nyumba zao zaidi ya 400

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
IMG_0006-620x308.jpg

Wakazi waliojenga eneo la Iloganzila Jimbo la Kibamba Dar es salaam leo wamebomolewa nyumba zao ambazo ni zaidi ya nyumba 400, zoezi hilo limekuja baada ya amri iliyotolewa na Mahakama Kuu juzi.

Taarifa zinasema eneo hilo lenye ukubwa wa heka 33, mali ya Henry Kashangaki lilikuwa na mgogoro tangu 1997 baada ya kundi la watu 11 kuvamia na kuanza kujenga nyumba na kuwauzia wananchi wengine.

Baada ya eneo hilo kuvamiwa mmiliki wake aliamua kwenda mahakamani na kuwashtaki Shaha Matibwa na wenzake kumi, kesi hiyo iliendeshwa kwa muda wa miaka mitano na mwaka 2010 hukumu ilitolewa na Kashangaki na Matibwa walionekana wana haki ya kumiliki hivyo walitakiwa kugawana.

Hata hivyo, Kashangaki hakuridhika na hukumu hiyo na kukata rufaa na kwenda Mahakama Kuu, January 2016 kesi hiyo ilitolewa hukumu na Kashangaki alishinda, hivyo juzi Mahakama hiyo ilitoa amri nyumba zivunjwe ili kumpisha mwenye eneo lake.
 
Sawa kabisa hiyo inaitwa UTII WA SHERIA BILA SHURUTI, kwa nini uvamie eneo sio lako kisa wewe huna uwezo.
 
Duuh, makazi 400! Kwani haya mambo hayawezekani kuamuliwa nje ya mahakama, Mwenye eneo akapata pesa nzuri kwa sababu ana bargaining chip na wavamizi wakaondokana na vilio vya nyumba.
 
Kwani sheria inasema ukikaa muda gani bila kuendeleza eneo unanyang'anywa pia kwanini wasimtafutie eneo lingine huyo mmoja aanze moja kuliko kuondoa watu wote hao
Kumnyang'anya mtu eneo kwa sababu halijaendelezwa kuna itifaki zake. Hao wavamizi ni wezi tu pamoja na aliyewauzia, wingi wao hauwahalalishii eneo hilo.
 
View attachment 344112

Wakazi waliojenga eneo la Iloganzila Jimbo la Kibamba Dar es salaam leo wamebomolewa nyumba zao ambazo ni zaidi ya nyumba 400, zoezi hilo limekuja baada ya amri iliyotolewa na Mahakama Kuu juzi.

Taarifa zinasema eneo hilo lenye ukubwa wa heka 33, mali ya Henry Kashangaki lilikuwa na mgogoro tangu 1997 baada ya kundi la watu 11 kuvamia na kuanza kujenga nyumba na kuwauzia wananchi wengine.

Baada ya eneo hilo kuvamiwa mmiliki wake aliamua kwenda mahakamani na kuwashtaki Shaha Matibwa na wenzake kumi, kesi hiyo iliendeshwa kwa muda wa miaka mitano na mwaka 2010 hukumu ilitolewa na Kashangaki na Matibwa walionekana wana haki ya kumiliki hivyo walitakiwa kugawana.

Hata hivyo, Kashangaki hakuridhika na hukumu hiyo na kukata rufaa na kwenda Mahakama Kuu, January 2016 kesi hiyo ilitolewa hukumu na Kashangaki alishinda, hivyo juzi Mahakama hiyo ilitoa amri nyumba zivunjwe ili kumpisha mwenye eneo lake.
Hapa kazi tu. Tafuteni pa kwenda
 
Back
Top Bottom