Wakazi wa dar si muhame jiji hili kha! Ndo maana utendaji kazi unakua mdogo

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,352
3,533
Habarini,

Yaaani sikuamini,

Mi nimkazi wa Dar sawa, lakini nature ya kazi yangu na mahala nikaaapo huwa sikutani sana na haya niliyoyaona leo.

Nilikwenda mbezi ya kimara kulala huko na leo asubuhi nikasema "nirauke" asubuhi na mapemaaa ili niwahi nyumbani kwangu nikalale maana huko mbezi kulikua na shughuli flani.

Saa 11 asubuhi naingia barabarani kuelekea maeneo ya ubungo. Nimekutana na foleni ndefu sana.

Nikajiuliza hawa watu wanawahi makazini sawa. Lakini kazini unatakiwa uripoti labda saa mbili. Wewe unaamka kwako say saa10 alfajiri ili by saa 11 alfajir uwe barabarani.

Mwili wako unakua unafikiria na kufanya kazi jumla yamasaa 13. Yaani kuanzia saa 10 alfajir mpaka 11 Jioni.

Je, utendaji wa kazi hapa kweli utakua wa ufanisi? Akili itakua active kweli kwa massaa yote haya? Adha yote ya nini hii? Dah!
 
We rudi shamba tu. Tuliozoea tunaenjoy.
If u can live n make it here.. u can make it anywhere
 
* Viongozi wa serikali hii ya kichovu ndiyo wa kulaumiwa kwa foleni ya Dar....Wangeweza kutoa malori yote katika njia ya Mandela...wangeweza kutengeneza barabara mpya ya Tegeta-kimara-Tabata-Gongo la Mboto/pugu- Mbagala, na mengine mengi...lakini akili zimelalala zinawaza namna ya kupiga madili.....
 
Unatoka Saa 10 asubuhi Unaenda kazini Unarudi saa 5 usiku unakuta watoto wamesha lala, unadhani nini kitaendelea? Maisha ya Dar uwenazo usiwenazo ni tabu tupu.
 
Daah sio salama tena kwa kuishi.

Watu kibao shida tupu .

Nipo lushoto huku nafurahia maisha .

Shuruba na rabsha za dar nimeshazisahau .

Tanzania sio dar tu
 
Back
Top Bottom