Wakazi amlipua Diamond vikali

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
14,238
22,668
Kupitia account zake msanii wakazi amemlipua vikali msanii boss wa wasafi diamond..

NASIBU USIPOTOSHE WATU, KWA KUPINDISHA UKWELI NA KUONGEA UNAFIKI.

Nimeona clip ya interview yako. Maelezo yako sio sahihi kuhusu soko la muziki la nje, na nashangaa wewe kujidai unahubiri unity na kutokatishana tamaa baada ya wewe mwenyewe kusanda huko “international”… kabla ulikuwa kimya kama sio perpetrator mwenyewe.

Muziki wa Tanzania haujaanza kufanya vizuri sasa hivi, infact sasa hivi ndio unafanya vibaya zaidi historically, maana wewe ndio Number 1 artist, lakini hata kujaza watu elfu 6 ughaibuni kimbembe, Waafrika wanaweka Historia duniani wewe umerudi kupambana na Ally Kiba.

Mimi binafsi nilikuwa nakukubali kwa nidhamu yako ya kazi (work ethics) na uthubutu, ila sasa umekuwa miyeyusho. Tunaelewa na kuheshimu kwamba umekuwa mfanyabiashara… maybe ndio imekuathiri upande wa muziki na huo ushindani usio na tija ambao huko duniani hamuwezi upeleka umepelekea kutaka kutia huruma.

Ngoja nimalizane na maswala ya Chama (ACT Wazalendo) na pia ku post kazi za Wasanii ambao wanafanya Sanaa kwa Level ya juu kwanza, alafu nitarudi kudadavua nachomaanisha kwa kutumia hiyo clip yako and beyond.

Beberu
*********************

Anyway wakazi ameongea ukweli shida ya huyu bwana huwa ni untouchable kabisa ukimgusa , hasa chawa wake ..

Pia baada ya muda mfupi chawa wa diamond nao wakamjia Juu kama inavyoonekana
FB_IMG_16914938777571258.jpg
 
Ana address uhalali wa alichosema Diamond, angeanzisha jambo lake bila kutaja uhalali wa maoni ya mtu mwingine
Kiuhasilia topic Fulani ambayo ndiyo hayo maoni ya mtu tena maarufu kama diamond lazima yawe criticized tena na mtu wa industry kariba ya diamond kama wakazi ..

Why asikosoe maoni hayo ya diamond na aanzishe kitu kingine? Diamond ni nani?
 
Bado wanaongea kuhusu Diamond. hawajiulizi ni nani hasa atakaimu nafasi yake baada ya yeye kumaliza! au ndo kuwa tegemezi kiasi wanatamani ni Diamond tu ndo awawakilishe huko international.

Kwann wakazi yeye asisimame kuendeleza gurumu hili ambalo kwa mtizamo wake anaona Simba ameshidwa?

Ni ujinga nchi yenye wasanii zaidi ya 1000 lila sku ni msanii mmoja tu anafananishwa na Nigeria, south Africa, mpaka America.

Wamwache simba apumzike afanye kazi zake bila ya presha mana amepambana kwa nafasi yake..
 
Wakazi na Ostadh Juma Namusoma hawana tofauti.

Wote ni wash outs waliochoka kimaisha wanaotafuta relevance ya kuongelewa.
Sidhani wana tofauti kubwa
Ostadh juma alikuwa anawa manage wasanii ..while wakazi hajawahi

Wakazi ana exposure ameishi nje muda mrefu while ostadh juma hana.

Wakazi anaongea kwa fact na mifano while ostadh juma hawezi .

Wakazi anakosoa kwa staha tofauti na ostadh juma
 
Bado wanaongea kuhusu Diamond. hawajiulizi ni nani hasa atakaimu nafasi yake baada ya yeye kumaliza! au ndo kuwa tegemezi kiasi wanatamani ni Diamond tu ndo awawakilishe huko international....
Hilo ndio huwa tunakataa .
Yaani hii theory ya diamond ni forever ndo hatutaki ..

Why usiseme wasanii wengine nao wakaze washike mpini waendeleze gurudumu mbele kuliko huyo diamond ambaye ameishiwa kiuhalisi na amebakiza majungu na kujitapa ..

Kwani kabla ya diamond muziki haukwepo hapa bongo? Kina nature walishaleta tuzo kabla ya huyo diamond.

Hii Tabja ya kumfanya kama Mungu ife infact kwa sasa madogo kama rayvanny, marioo, harmonize, jux, chino Kidd wanakimbiza kuliko huyo diamond ..

Akiondoka wengine wataendeleza
 
Basi kama wanakimbiza wamfunike kwa kazi nzuri sio kwa kutaka kulinganishwa nae
Kila mtu ni Bora kwa nafasi yake Ronaldo amekuwa akijitapa kwa muda sana mpaka leo lakini kujitapa kwake hakufanyi vipaji vingine visionekane.

Ko wacha ajikuze ajimwambafai mana ni haki yake hajavunja sheria.

Hao madogo wakaze kazi zao zionekane duniani huko wapewe deal nono na waokote tuzo kumzidi..
 
Basi kama wanakimbiza wamfunike kwa kazi nzuri sio kwa kutaka kulinganishwa nae
Kila mtu ni Bora kwa nafasi yake Ronaldo amekuwa akijitapa kwa muda sana mpaka leo lakini kujitapa kwake hakufanyi vipaji vingine visionekane...
Ko wacha ajikuze ajimwambafai mana ni haki yake hajavunja sheria.
Hao madogo wakaze kazi zao zionekane duniani huko wapewe deal nono na waokote tuzo kumzidi..
Hicho ndio kinatakiwa ni swala la process tu nao watafika muwasapoti sio kwenda na mtu mmoja ambaye ameshafika prime yake .

Halafu sidhani kama kuna dogo ambaye amejifananisha na diamond ila ni mashabiki nyie ndio mnalinganisha acheni wafanye muziki kwa nafasi yake kila mtu mkuu
 
Diamond yuko juu kuliko hao wote uliowataja na wanajua hivyo.

Ikitokea ameishiwa, itaonekana tu kuwa Diamond kaishiwa lakini tukubali tukatae.

Diamond kaifikisha Bongofleva mbali zaidi, kimataifa kuliko msanii yeyote hapa nchini.

Ukienda nje ya nchi,Mond ndiye anajulikana kuliko wote hao iliowataja na si kwa kitu kingine, bali ni muziki.

Yeye Diamond, kaboresha muziki, hata video quality zake,ni yeye ndiye mtu wa kwanza kabisa kutoa video kali na za gharama hapa nchini,tofauti na quality zilizokuwepo hapo kabla yake.Diamond kaanzisha lebo ya WCB,ni moja ya lebo za mfano kabisa hapa nchini na nje ya mipaka yetu,kuwa na mafanikio makubwa.

Tufike mahali, tuache kujizima data,kwa kutaka kusema flani yuko juu kuliko Diamond, wakati kila mtu anaona hiki ni kipindi cha Mond na lebo yake hapa nchini,then na wengine ndiyo wanafuatia.

Diamond anapigwa vita na alipigwa vita sana,lakini anaendelea kukomaa.

Clouds walimpiga vita, leo hii Fiesta inasuasua, ila Wasafi festival ndo hiyo inaendelea,hivi punde wanaanzia Mtwara.

Akina Wakazi et al, wakomae.
 
Sidhani wana tofauti kubwa
Ostadh juma alikuwa anawa manage wasanii ..while wakazi hajawahi

Wakazi ana exposure ameishi nje muda mrefu while ostadh juma hana.

Wakazi anaongea kwa fact na mifano while ostadh juma hawezi .

Wakazi anakosoa kwa staha tofauti na ostadh juma
Ila mwisho wa siku msingi hasa wa ukosoaji wao una mrengo wa chuki binafsi kwa Diamond na sio kwa nia ya kumrekebisha.

Nadhani chachu hasa ya kukosoa (personal attacks) kwao ni uchungu wa walionao juu ya kile alichonacho Diamond (uwezo wa kifedha) ambacho wao hawana na wanahisi walipaswa kuwa nacho. kwa lugha nyepesi, WIVU.
 
Back
Top Bottom