Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mahakama ya Hakimu Mkazi iliyopo Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetoa hukumu katika shauri la madai ya kashfa lililofunguliwa na msanii na Mbunge Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo) dhidi ya Webiro Wasira maarufu kama Wakazi.
Katika hukumu iliyotolewa tarehe 13 Machi 2026, mahakama imebaini kuwa taarifa zilizosambazwa na Wakazi dhidi ya mlalamikaji zilikuwa za uongo na zenye kumdhalilisha, na zimeathiri sifa yake katika biashara pamoja na tasnia ya muziki ndani na nje ya Tanzania.
Mahakama imeamuru mshtakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya shilingi milioni 100 (Tsh 100,000,000) kutokana na madhara yaliyosababishwa na taarifa hizo za kashfa.
Aidha, mahakama imeagiza mambo yafuatayo:

- Mshtakiwa aombe radhi hadharani kwa taarifa za uongo alizosambaza.
- Aondoe na kukanusha taarifa hizo katika tovuti, mitandao ya kijamii, blogu, magazeti na hata kwenye chaneli za YouTube.
- Amezuiwa kuendelea kusambaza taarifa zozote za kashfa dhidi ya mlalamikaji katika siku zijazo.
- Kiasi hicho cha fedha kitalipwa pamoja na riba ya asilimia 7 kwa mwaka kuanzia tarehe ya hukumu hadi kitakapolipwa kikamilifu.
- Pia gharama za kesi zimelipwa na upande wa mshtakiwa.