Wakati wabunge wa CCM wakitetea posho za vikao na kutokatwa kodi kwenye kiinua mgongo

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,235
16,205
Wabunge wa ccm nawashauri tu wakubali kulipa kodi kama watu wengine wanavyolipa
Wakati walimu wakikatwa kodi kwrnye mishaara yao wabunge wa ccm hawako tayari pesa zao za viinua mgongo zikatwe kodi
Wakati wananchi wakiwa hawana wa kuwatetea kuhusu mzigo unaoweza kuwaangukia wa kodi kutokana na kutoa hela kwenye ATM M pesa Airtel money Tigo pesa hawana mtu wa kuwatetea bali wabunge wa ccm wanatetea maslahi yao tu
Wakati wapinzani wakikubali posho ya vikao iondolewe na kupeleka kwa jamii ya wasio na maji safi
Wabunge wa ccm hawataki kusikia hizo habari
Wakati wabunge wa upinzani wakikubali viinua mgongo vyao vikatwe kodi wabunge wa ccm hawako tayari viinua mgongo vyao kukatwa kodi
Wabunge wa upinzani wakiwa hawapo bungeni sisi wananchi tunakosa hata wa kutusemea
Mungu ndio anajua yale tunayoyapitia tu
Na nyie wabunge wa upinzani kwa nini msirudi bungeni tu kama mnaona mnaonewa mwachieni mungu tu
Ona sasa tunakosa hata mtetezi
Wabunge wa ccm kweli mnajiona nyie tu sisi hamtuoni tuteteeni basi jamani
Kiukweli nianze kutafuta kibubu cha kuhifadhia pesa zangu tu maana huenda kufikia mwezi wa saba benk na mitandao ya simu patakua si salama kuweka hela
 
All of a sudden, ishu ya posho imekuwa ni ya wabunge wa sisiemu, chadema kwisha kabisa!!
 
wabunge wa ccm sio wabunge wote,au hukumsikia mbatia alivojitetea juu ya hoja ya hiyo kodi??
 
Back
Top Bottom