VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
UKAWA msidhani hatuwaoni. Tunawaona ila tunawapa nafasi ya kutamba kwa namba. Kuonesha watu kuwa mna mafuriko popote apitapo mgombea wenu Lowassa. Huu ni wakati wenu kucheza scene yenu halafu nasi CCM tuanze scenes zetu. Kalikali. Za kiushindi. Tayari muda unakaribia. Muda wetu umepiga hodi na tunainuka kuufungulia. Muda umeshafika. Subirini muone.
Malizeni kuteua wagombea wenu wa Ubunge na Udiwani halafu tuwaoneshe mchezo. Tutawashawishi wagombea wenu ili wafanye 'mambo' na wetu wapite bila KUPINGWA. Mbele ya rupia,wapo watakaojaza hovyo fomu zao ili wawekewe mapingamizi na mwishoni kuondolewa. Wapo watakaochelewa makusudi kurudisha fomu na hivyo kujifuta kwenye kugombea. Wapo watakaotengeneza wenyewe filamu za kupotea.
Muda umefika huku ukiwa unahitajika. Wakati wa kupiga na kuhesabu kura pia hatuna wasiwasi. Tutafanya 'mambo' hata bila ya kuwatumia mgambo. Kitaeleweka tu mwaka huu. CCM itashinda kwa kishindo kikubwa kwakuwa ina nia na maarifa ya kufanya hivyo kama alivyodokeza Mwenyekti wetu alipohutubia hapa Lumumba siku Dr. Magufuli alipochukua fomu ya kugombea Urais. Tumejipanga.
CCM, mbele kwa mbele!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam