Wakati umefika wa CCM kugawanyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakati umefika wa CCM kugawanyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Raia Fulani, Aug 19, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna mambo mengi yanaendelea hapa nchini ambayo tunaweza kuyachambua na mengine kuonekana kwa wachache ambayo yote haya yanaumiza nafsi za watanzania wengi. Nikitaja madudu hapa sitamaliza ila wenzangu mnajua, tena zaidi kuliko mimi. Nimewahi kusema wakati flani kuwa mzalendo wa kweli ni yule mwenye sifa kuu mbili. kwanza uwezo wa kujibainisha, pili awe na dhamira iliyo hai. vingine ni mbembwe tu. sasa basi, haya yote yamefika hapa kwa uongozi 'imara' wa CCM. ndani ya chama kuna waadilifu wachache kama Sitta na kundi lake. Ili usemi wa baba wa Taifa utimie, LAZIMA hawa watu wajitoe ndani ya chama na kuangalia mistakabali wa taifa kwa mapana na uzalendo zaidi. kuendelea kubaki na kukubali kunyamazishwa huku ukijifanya unaumia ni unafiki tu! Mbona hawa viongozi wetu wanaogopa changamoto? Au siasa ndio ajira? Bila siasa mtu hawzi ishi? Bila CCM hakuna maisha? Obama alisema YES WE CAN! Na wao wanaweza kujiengua na kufanya mambo ya maana zaidi. Tunataka Tanzania mpya 2010 na kuendelea. Naomba kuwasilisha hoja!
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  God Help it should not such long...!
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi kipi,o cha uadilifu nini bwana mziwanda?
   
 4. Dogo Tundu

  Dogo Tundu JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 441
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  kaka mi nakubaliana na wewe 100%
  kila kitu kinamwisho, nahisi huu unaweza ukawa mwisho wa ccm.
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kipimo cha uadilifu bwana ni matendo yako mkuu. dhamira iliyo hai inayokusuta pale unapotenda kinyume. uwe na uwezo wa kuvaa hali ya mtu mwingine na kujiuliza itakuwaje kama nikiwa yeye? ukishajijibu maswali hayo kisahihi, basi huo ni uadilifu
   
 6. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  SITTA hana lolote bado anahofuu kubwa ya maisha yake bila kuwa CCM..Ni unafiki usiokuwa na KIPIMOOOOO...
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  thats y nikasema ni unafiki kuendelea kulamba miguu ya wakubwa kwa kuogopa changamoto
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Akina Seif na wenzake waliachana na ufuasi wa Sultani CCM walipotakiwa kufanya hivyo na Mwalimu Nyerere ili kama wanapingana na maamuzi ya chama basi wapinge wakiwa nje ya CCM na hadi leo wapo nje ya CCM na mambo yao si mabaya tatizo kuna watu wanaiabudu CCM na kuona bila ya CCM hawana wa kuwapa riziki.

  Watu kama hao huna la kuwambia wakaachana na CCM ,kwa wanavyoiabudu CCM hata wakiambiwa wavue watavua.
   
 9. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuanguka kwa ukomunisti uko Urusi(USSR) miaka ya 1990 na hatimaye kumeguka kwa nchi hiyo kulitoka na kile kitu kinaitwa "contradictions" katika mfumo wa kisoshalisti uliokuwa umetawala tangu mapinduzi ya 1919 (kama sikosei) chini ya Lenin. Utaona kwamba huu ni muda mrefu ni kama miaka 70 na ushee.

  CCM ilianza kuwa na contradictions za ndani hasa pale ilipoamua kulitosa azimio la Arusha kule Zanzibar chini ya uongozi wa mzee Ruksa. Kwenye msafara wa Mamba pekee Kenge wakaanza kujipenyeza na matokeo yake ni tabaka kuanza ndani ya chama na hatimaye ndani ya nchi.

  Contradictions hizo zilijitokeza zaidi katika mchakato wa urais ndani ya CCM 2005 ambapo kwa mara ya kwanza kulikuwa na ushindani mkubwa uliogubikwa na matumizi makubwa ya pesa, rushwa, ubaguzi wa rangi na hila mbali mbali. Mchakato ule wa ndani ya CCM uliacha ufa mkubwa. Kwa vile uongozi wa CCM haukujali kuziba "ufa" ule matokeo yake ukuta sasa unaanza kubomoka!

  Kilichofanywa na NEC juzi ni "blunder" moja kubwa sana kama Bunge lilivyomfukuza Zitto Kabwe mwaka jana. Nafasi ya Usipika ni kubwa sana na Bunge ni moja ya muhimili wa dola. NEC haikumdhalilisha Sitta pekee lakini ndani ya mitima yao (deep down) wanajua wamewadhalilisha wabunge kwa ujumla kwa kisa ambacho kiiini chake hasa ( hata kama hili halisemwi) ni Richmond! Ndio maana NEC imeunda tume ya Rais Mstaafu Mwinyi kujaribu kuweka mambo sawa. Tusibiri tuone lakini CCM haiwezi kuwa kama zamani tena (CCM will never be the same).

  Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu ya utandawazi hata wana CCM hususani wabunge wakizibwa midomo nje ya vikao hakuna siri tena kama tunavyoona kwenye JamiiForums. Wakifanya usiku, asubui mambo yanakuwa hadharani! Kwa hali hii hata kama CCM haitaki kutambua na kukubali kwamba inameguka taratibu lakini pole pole inaelekea uzeeni huku ikiandamwa na "magonjwa" lukuki (ufisadi, mahakama ya kadhi na IOC, waraka wa kanisa, mamlaka ya Zanzibar, Muafaka wa Zanzibar na sasa mvutano katika Bunge) na wote tunajua matokeo ya uzee: KIFO
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,606
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Mwingine huyu wa kambi ya ufisadi kaajiriwa ili kuwapaka wote wale ambao wanajaribu kupambana na mafsadi ndani ya chama na serikali. Wewe unafiki wako wa kuwapigia debe mafisadi huoni!!!
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Aug 20, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Ni wakati mzuri kwa akina Mwakyembe kuonyesha rangi zao halisi sasa!
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Haya yalitabiriwa na marehemu Kolimba (Mungu amrehemu) kipindi hicho. CCM ingekuwa macho ingezinduka na kufanya mambo yake kwa mtazamo mpya lakini wapi! Sio kwamba tunaichukia CCM bali yale yanayotendwa na wale walio chamani. Watu hamsini waadilifu ndani ya chama hicho hawawezi kutushawishi tukakipenda. Vuguvugu la kweli linahitajika hapa badala ya kung'ang'ania hii hali tete itakayotupeleka pabaya wakati fulani mbeleni. Tusidanganyike kuwa mataifa mengine yanaitamani hii hali ya 'utulivu' tuliyo nayo. wanajua dhahiri kuwa ni kiini macho tu na ni sawa na moto wa pumba. ili tusifike huko, CCM aidha ijipange KIZALENDO ama wale wazalendo wajitoe tu. mtaona watu watakavyotapatapa
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ccj walishindwa vipi kukigawa ccm?
   
 14. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,162
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Wana Great Thinker,
  Kwa maoni yangu na ushauri wangu kutokana na hii mada/topic, mimi naona tatizo lipo kwenye Katiba ya Nchi, naona Katiba inampa Nguvu na Madaraka makubwa Rais ambaye ndie Mwenyekiti wa Chama ambacho kinatawala.
  Tunapaswa kuwa na Katiba ambayo inawapa wananchi nguvu ya kuwawajibisha Viongozi, hata Rais asipo/wasipo fanya kazi au kutimiza wajibu wao. Bado tuna kazi kubwa ya kubadilisha Katiba kutoka Mfumo wa chama kimoja kwenda Vyama vingi ingawa Katiba yetu tunaiwekea viraka hapa na pale.
  Uoga wa viongozi wetu wa kutoa maoni, ushauri kwa kuhofia Usalama wao na familia zao na biashara zao na mali zao, na kufanya Siasa kama ni njia ya kutafuta ulaji, ili mradi mkono uende kinywaji.
   
 15. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mimi naamini udhaifu, udini na visasi vya JK ndio vinaiua CCM!
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  mkuu unadhani kwa mchakato wa katiba unaoendelea kuna jambo jema lolote mbele?
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,606
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Magamba igawanyike mara ngapi bana!!!? we husikii Lowassa ana kundi lake, Membe ana kundi lake, Mkapa ana kundi lake, Sitta ana kundi lake. Magamba imeshagawanyika miaka mingi iliyopita.
   
 18. m

  mharakati JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  siyo unafiki, wale wazuri wachache waliopo CCM wanafikiri muda bado wana matumaini ya kuibadilisha CCM ambayo bado ni chama makini kiitikadi na kinadharia. Haya matumaini bado ni makubwa kiasi fulani, lakini yakianza kufifia kabisa katika miaka miwili ijayo maamuzi mazito yatachukuliwa...kinachoiunganisha CCM sasa hivi ni matumaini kama haya waliyonayo makundi yote ndani ya CCM. Nyerere alisema wapinzani wa kweli watatoka CCM..tukae tusubiri
   
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo tusubiri kusambaratika sio?
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Red
  Miaka 50 bado unasema tuamini katika nadharia za ccm na itikadi zake? Hapo umechemsha. Au una tafsiri nyingine ya nadharia?

  Black
  Hata kina Dr Slaa Wametokea ccm, hivyo tayari kuna upinzani wa kweli ambao chimbuko lake ni ccm
   
Loading...