Wakati ufaao ni sasa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,213
22,277
WAKATI UFAAO NI SASA

Leo nimeona nitumie haki yangu ya uhuru wa mawazo kwa mujibu wa ibara ya 18(i) ya katiba ya JMT. Nitatamka jambo kuhusiana na maisha tunayoishi. Kilio ni kikubwa kwamba maisha ni magumu na wengi tunaishi chini ya matarajio yetu. Kwa ufupi wengi tunaishi kwenye umaskini. Nakubaliana na alieyesema kwamba kama kipato chako ni chini ya USD 10,000 (Tsh 23,000,000/=) kwa mwaka basi wewe ni maskini.

Kimsingi lazima tukubali kwamba haukuwa mpango wa Mungu kwamba binadamu aishi maisha magumu. Mungu alipanga binadamu aje kuwa mtawala wa kila kitu na aishi maisha bora (Mwanzo 1:26 -27). Lakini pamoja na kuingia dhambini bado Mungu ameendelea kutupenda na kutupa miongozo mbalimbali kupitia biblia ili kufikia malengo ya kuondokana na umaskini.

Mhubiri 9:10 "Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe". Kama ambavyo mhubiri kaandika basi kila mmoja wetu popote ulipo fanya unachoweza kufanya kwa nguvu na maarifa yako yote bila kuvunja sheria za Mungu na za Jamhuri.

Anza sasa kujikomboa kutoka hapo ulipo. Usisubiri baadae maana hata biblia inasema wakati ufaao kwa ukombozi ni sasa, 2 Wakorintho 6:2. Ulicho nacho mkononi kwa wakati huu ndo kitakachokuvusha kwenda kwenye Caanan yako. Inaweza kuwa vyeti, kipaji au chochote kile unachoweza kukitumia. Kumbuka Musa aliwavusha wana wa Israel kwa fimbo aliyokuwa nayo mkononi. Hata wewe una kitu mkononi mwako usijidharau.

Mwisho kabisa kwa pamoja tuendelee kuwa watiifu kwa ibara ya 25 ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania isemayo;

25.-(1) Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa mali katika jamii, ndilo chimbuko la ustawi wa wananchi na kipimo cha utu. Na kila mtu anao wajibu wa-

(a) Kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifu katika kazi halali na ya uzalishaji mali; na
(b) Kutimiza nidhamu ya kazi na kujitahidi kufikia malengo ya uzalishaji ya binafsi na yale ya pamoja yanayotakiwa au yaliyowekwa kisheria.
 
"Wakati ni sasa"

Ujumbe wako umeamsha hali ya kujituma zaidi.

Binafsi nahitaji kubadilika. Baadhi ya fursa zinanipita kwa kukosa uthubutu.

Ikishapita inaanza mambo ya ningejua, ningejua.

Ila Mungu ni mwema mapambano inaendelea.
 
Ubar
"Wakati ni sasa"
Ujumbe wako umeamsha hali ya kujituma zaidi.

Binafsi nahitaji kubadilika. Baadhi ya fursa zinanipita kwa kukosa uthubutu.

Ikishapita inaanza mambo ya ningejua ...ningejua.

Ila Mungu ni mwema mapambano inaendelea.
Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom