DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,674
FIKRA ZA KIONGOZI WA TAIFA LANGU TANZANIA DUNIA YA TATU
Kweli wakati mwingine kuna mawazo ambayo wakati mwingine ukiyasikia na kuyapima kuwa yametoka kwa kiongozi wa juu kiwango hicho cha kuomba mamlaka ya juu ya Taifa...napata muwasho wa fikra za kujifikirisha ilikuwaje mtu wa hadhi hiyo kuwaza kuwa Taifa sasa linawaza kuwa na Rais mwenye Ukwasi bila kujali ukwasi wake umepatikanaje, kinachtakiwa ni Rais huyo apewe nafasi ya kuwatumikia umma hivyo umma huo utapata baraka ya Utajiri wa Rais huyo.Kwa mujibu wa maneno hayo kuwa anachukia umaskini...imenifikirisha sana na kunipa maswali mengi ya kujiuliza na kuwaza papo kwa papo nikiwaza hili na lile kama hivi
1:Huyu Kiongozi mwenye nia mpaka akawaza hivi...Je alimaanisha hivyo kweli?
2: Akiwa na kusudi lipi?
3: Kwa manufaa ya nani?
4: Je fikra zake hizo zina ukweli au ni uongo wa mchana kweupe kwa Wanataifa na nafsi yake?
5: Na Wananchi wanayapokea na kuyazingatia kwa dhati kama kauli thabiti na ya manufaa kwa maisha yao?
6: Je madhara ya kauli za namna hiyo kwa Taifa ni yepi?
7: Je ni haki kwa viongozi wetu kuwaza hivyo na kujalibu kutuaminisha hivyo kiuhalisia?
8: Nani anawajibu wa kuhakikisha viongozi hawatoi sumu ya maneno yasiyotimizika na hivyo kulaghai umma kwa kuwapa matarajio makubwa isivyostahiki na kufanya fikra za umma kuwazia yasiyowezekanika?
9: Nini funzo kwa Taifa na Umma kwenye kukumbatia kauli Tatanishi kama za namna hiyo?
10: Yale ambayo kiuhalisia hayatekelezeki yanapoletwa kwa umma kama matamanio na kuwaaminisha umma nini sifa yake kimaadili juu ya viongozi dhidi ya umma?Kwa kuwa umma uaminishwa kupitia Kiongozi na kiongozi anayotamka ynapokuja kuwa kinyume na UKWELI kwa kiwango kikubwa kwa Umma basi matamanio yaliyojengwa unakuwa ni UONGO na jamii kama Taifa HAIPASWI kujengwa kwa kuaminishwa UONGO kwa kuwa Kiongozi AKIWAONGOPEA UMMA ni mwanzo wa fikra zenye sura ya UONGO kustawi na kumea ...Je tunakubali Taifa kumea na kujitanabaisha kama Taifa la WAONGO?
FIKRA ZA KIONGOZI WA DUNIA YA KWANZA
Waziri Mkuu wa Uholanzi Bw. Mark Mutte akirejea nyumbani kwake toka kazini kwa kutumia usafiri wa baiskeli huku akimiminiwa saluti na walinzi wake. Hii hapa kwetu vipi