Wakati Tanzania imezama katika mawazo mgando ya mwaka 47 kuwakatalia raia zake uraia pacha, nchi nyingine sasa zinatoa uraia kukaribisha wawekezaji!

Wakati Tanzania imezama katika mawazo mgando ya mwaka 47 kuwakatalia raia zake uraia pacha, nchi nyingine sasa zinatoa uraia kukaribisha wawekezaji!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
14,176
Reaction score
25,919
Ni jambo mojawapo linaoonyesha kwamba viongozi na watu wengi nchini Tanzania wamezama katika mawazo ya mwaka 47 ya zama za ujima pale wanapokuwa na msimamo mkali dhidi ya uraia pacha kwa watanzania ambao eidha wamechukua au wana nia ya kuchukua uraia katika mataifa mengine kwa ajili ya kurahisisha uwekezaji wao, ajira au masuala mengine yenye maslahi ya maendeleo ya kiuchumi kwao, ndugu zao na taifa kwa ujumla.

Sababu kubwa inayotolewa na wengi wanaopinga uraia pacha kwa watanzania wenzao eti ni kukosa uzaledo au masuala ya usalama, wakiashiria kwamba mafisadi wengi tulionao nchini ni wazalendo zaidi ya hao Watanzania wanaoomba Tanzania iwaruhusu kuwa na uraia pacha, angalau kwa watu wenye asili ya Tanzania kwa kuzaliwa au kurithi. wengine wanapinga kwa sababu za wivu tu usio na maana, daima hawataki kuona wenzao wakiedelea au kufaidika na jambo ambalo wao sio rahisi kupata.

Na ikumbukwe kwamba suala la uraia pacha sio geni. Jirani zetu Kenya, Uganda na Burundi wanaruhusu, vile vile nchi kama Afrika Kusini, Marekani, Botswana, Misri, Japan, Sierra Leone, Germany, Ghana, India, Uingereza, Sweden, Zimbabwe, Australia, Nigeria, Singapore, Namibia, Morocco nk, pamoja na hata taifa la United Arab Emirates!

Mara nyingine hata unajiuliza, hivi suala la usalama kwa Tanzania ni kubwa kuliko nchi zinazoruhusu uraia pacha, kama zilizotajwa hapo juu? Ni tishio gani la usalama lipo dhidi ya watu wenye asili ya Tanzania ambao wangependa kuwa na uraia pacha?

Wakati Tanzania tunaendeleza mawazo mgondo ya kupinga uraia pacha, ambayo mara nyingi n yanatolewa na watu ambao huenda hawajawahi hata kuishi nje ya Tanzania, nchi kama Mauritius, Dominica, Malta, Grenada, Cyprus nk zimeenda hatua mbele zaidi katika suala la uraia pacha, kwamba sio lazima uwe umeishi nchini mwao kupata uraia, bali ukiwekeza nchini kwa kiwango cha zaidi ya dola 200,000 basi unaweza kupata uraia wa nchi hizo.

Watanzania tuondokane na mawazo mgando ya mwaka 47!
 
Mkuu mbona Mimi Nina uraia pacha, vitu vingine ni kufanya kibabe na kuachana na mambo ya kimakuzi
 
Mkuu mbona Mimi Nina uraia pacha, vitu vingine ni kufanya kibabe na kuachana na mambo ya kimakuzi
Mkuu, kuna nchi ambazo ili kupata uraia pacha lazima wapeleke barua ubalozi wa nchi yako. Balozi zetu wakipata hizo barua hawakawii kupiga simu uhamiaji Dar es Salaam na Ikulu!
 
Ukiangalia nchi ambazo raia wake wamesambaa sehemu mbalimbali Duniani ambazo kama zingekubali Dual citizenship zingefaidika sana kama Uraia pacha unafaida kubwa ni INDIA na CHINA lakini nchi hz zimekataa uraia pacha kwa nini au sababu gani wanajua wenyewe

Uraia pacha umekuwa ni hoja inayojadiriwa sana ktk nchi nying hii ni kutokana na faida ya moja kwa moja na kumbuka faida wanazozipata wazungu nchi za ulaya na America hazitokuwa sawa na faida wanazizipata nchi za ulimwengu wa 3 kuhusu hii dual citizenship na si kila nchi iliyokubali uraia pacha wamekubali kwa kila nchi mfano

Pakistan hawa wamekubali kwa nchi za
1. United Kingdom
2. Italy
3. France
4. Belgium
5. Iceland
6. Australia
7. New Zealand
8. Sweden
9. United States
10. Ireland
11. Netherlands
12. Switzerland
13. Canada
14. Egypt
15. Jordan
16. Syria
Angalia nchi hzo je umeona nchi gani ya ulimwengu wa tatu je Tanganyika hakuna wapakistani wenye asili ya huko wanaopenda kuwa na uraia wa Pakistan pia?

Haya angalia Spain yeye amechagua makoloni yake tu na baadhi ya nchi ndo unaweza kuwa na Dual citizenship
Latin-American countries Argentina, Bolivia, Chile, Colombia, Costa Rica, Dominican Republic, Ecuador, Guatemala, Honduras, Nicaragua, Paraguay, Peru na Uruguay, Andorra, Portugal, Philippines na Equatorial Guinea.

Umesema Japan na UAE na Singapore nchi hzo hawaruhusu hata kidogo kitu kinachoitwa Uraia pacha wanasababu zao so kila nchi ambayo imekubali Uraia pacha wanazo sababu sawa na nchi zilizokataa pia zipo sababu

Mfano India hawaruhusu uraia pacha lakini watu wenye asili ya kihindi waliopo sehemu mbalimbali Duniani wanatuma kiasi cha dola billion 69 kwa mwaka kutoka kwa watu waliopo sehemu mbalimbali Duniani wenye asili ya India tu na kufanya India kuongoza Duniani kwa watu wa asili ya nchi hyo kutuma fedha nyumbani

Ukiangalia kigezo kikubwa Duniani cha watu kutaka Uraia pacha ni uwekezaji wa wale wanaoitwa Diaspora pia kila nchi inasababu zake lakini nchi za Ulaya na America si uwekezaji bali ni kupata wataalamu kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwani wanajua kila mtu atatamani kwenda huko leo hata wachina wanatamani kwenda Ulaya na US pamoja na nchi yao kuwa na maendeleo itakuwa nchi zingine?

Kingine kama swala la walio nje kusaidia ndugu zao mbona linawezekana sema waafrica si watu wakusaidiana au kutuma hela nyumbani kwao ilo ni swala la kiasili kabisa so mtu wa aina hii hata umpe uraia za Dunia nzima hawezi kubadilika hata kdg
 
Last edited:
Wakati mwingine kuna mambo ya kuchekesha yanayoendelea. Tulipinga apartheid ya kina Botha tukiita ubaguzi halafu wakaiti huo huo tunawakataa watanzania wenzetu kwa sababu tu mzazi mmoja sio mtanzania halisi.

Hili suala la uraia pacha linafaa kuwekewa msisitizo maalum na serikali ili tusiendelee kuwadhulumu watanzania wenzetu kwa sababu kisiasa ambazo zinazidi kupitwa na wakati kadri miaka inavyopita.
 
Hivi ni lazima uwe na dual citizenship ili uwekeze Tz au umletee mzazi wako fedha toka diaspora? Labda kama mnafanya biashara haramu huko. Mbona akina Mengi wametajirika na wanasafiri nje na kurudi watakavyo! Ina maana ninyi mna hela ndefu kupindukia na pengine mnaogopa kuulizwa mmezipataje? Tusijilinganishe na USA au kuwaiga tu, ile nchi ilijengwa na watumwa, ambao mpaka leo bado wanabaguliwa! Sembuse wewe unaejulikana ulikotoka na ulichofuata huko? Kwenu ni kwenu tu, halafu mkipewa dual citizenship mtadai triple citizenship, na kuendelea mpaka multi citizenship! Finally, don't stand outside there thinking you know better than your faulks back home. If you are so patriotic and not a coward yourself, stop complaining, come back and join the liberation struggle.
 
Ukiangalia nchi ambazo raia wake wamesambaa sehemu mbalimbali Duniani ambazo kama zingekubali Dual citizenship zingefaidika sana kama Uraia pacha unafaida kubwa ni INDIA na CHINA lakini nchi hz zimekataa uraia pacha kwa nini au sababu gani wanajua wenyewe

Mfano India hawaruhusu uraia pacha lakini watu wenye asili ya kihindi waliopo sehemu mbalimbali Duniani wanatuma kiasi cha dola billion 69 kwa mwaka kutoka kwa watu waliopo sehemu mbalimbali Duniani wenye asili ya India tu na kufanya India kuongoza

Mkuu, bora hata tungefanya hilo la India, ambapo wao wana kitu kinaitwa "Oversees Cizitenship of India".

Lakini India na China si walewale wenye mawazo mgando kama sisi? Kwa nini hutolei mfano jirani, Kenya, Burundi, South Africa etc. Hata Zimbabwe wanao!
 
Hivi ni lazima uwe na dual citizenship ili uwekeze Tz au umletee mzazi wako fedha toka diaspora? Labda kama mnafanya biashara haramu huko. Mbona akina Mengi wametajirika na wanasafiri nje na kurudi watakavyo! Ina maana ninyi mna hela ndefu kupindukia na pengine mnaogopa kuulizwa mmezipataje? Tusijilinganishe na USA au kuwaiga tu, ile nchi ilijengwa na watumwa, ambao mpaka leo bado wanabaguliwa! Sembuse wewe unaejulikana ulikotoka na ulichofuata huko? Kwenu ni kwenu tu, halafu mkipewa dual citizenship mtadai triple citizenship, na kuendelea mpaka multi citizenship! Finally, don't stand outside there thinking you know better than your faulks back home. If you are so patriotic and not a coward yourself, stop complaining, come back and join the liberation struggle.

Mkuu, suala sio kuwa citizen wa Tanzania, bali ni fursa zinazopatikana ukiwa raia wa nchi hizo nyingine ambazo huwezi kuzipata kama huna uraia wa nchi hizo. Sasa ili niwekeze kwa kiasi kikubwa Tanzania nahitaji kwanza kuwa raia wa hizo nchi nyingine. Ninachotaka ni kufanya hivyo bila kupoteza uraia wa Tanzania.

Ni kweli kwetu ni kwetu, ndio maana tunataka fursa ya nchi hizo nyingine bila kupoteza kwetu. Kama tusineona kwetu ni kwetu tungekubali kupata hizo fursa na kupoteza kwetu.

Sema tatizo la uraia specifically ni nini katika issue za uzalendo na usalama, sio kubwabwaja tu kama broken record uzalendo usalama.

Hebu sema, ni athari gani za usalama na uzalendo Uganda wamepata kwa kuruhusu uraia pacha, ambazo zimesababishwa na Waganda wenye uraia pacha?

Eti come back home. Come back home kwa kuwa wewe umeshindwa kutoka hivyo unaona bora wote tuwe malofa tu, kifo cha wengi harusi? Nyie ndio watu mnagoma kutengeneza barabara za mtaani kwenu eti kwa kuwa huna gari. Unasingizia uzalendo lakini ndani ya moyo wako unajua wivu tu umekujaa ukijua hata ufanyeje hutakaa uwe na uraia pacha asilani. Very simple minds watu kama wewe.
 
Last edited:
Wakati mwingine kuna mambo ya kuchekesha yanayoendelea. Tulipinga apartheid ya kina Botha tukiita ubaguzi halafu wakaiti huo huo tunawakataa watanzania wenzetu kwa sababu tu mzazi mmoja sio mtanzania halisi.

Hili suala la uraia pacha linafaa kuwekewa msisitizo maalum na serikali ili tusiendelee kuwadhulumu watanzania wenzetu kwa sababu kisiasa ambazo zinazidi kupitwa na wakati kadri miaka inavyopita.
Ukisikiliza maoni ya watu ambao hawajui hata maana ya uzalendo lakini kila siku wanaimba uzalendo, utajua watu wengine ni kiasi gani ni watupu kichwani katika masuala kama haya.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayepinga uraia pacha hapa Tanzania ambae yuko katika nafasi ya kupata uraia pacha wa Tanzania na nchi nyingine yeyote ile duniani. Hakuna. Wote wanaopinga wanajua wazi kwamba wao ni local people, and will always be local people.

Eti ni kukosa uzalendo. Kama mnajali uzalendo kweli mgekubali kufungua ofisi za ubalozi na mataifa yenye kutawala nchi nyingine na kukandamiza watu katika nchi zao? Yaani huo uzalendo unaishia midomoni tu, hata kama watu ni mafisadi wa kutupwa. Ovyo!
 
Last edited:
Mkuu, bora hata tungefanya hilo la India, ambapo wao wana kitu kinaitwa "Oversees Cizitenship of India".

Lakini India na China si walewale wenye mawazo mgando kama sisi? Kwa nini hutolei mfano jirani, Kenya, Burundi, South Africa etc. Hata Zimbabwe wanao!
Mkuu unajua nikwambie kitu Africa kwa mwaka wanapoteza zaidi ya dola billion 148 sawa na 25% ya GDP ya Africa nzima kwa Ufisadi na utoroshaji wa fedha nje ya Africa fedha zote hz zinakwenda kufichwa nje ya Africa haya pato linaloingia Africa tukoka kwa Diaspora ni dola billion 35.2 kwa mwaka huku kwa mwaka zaidi ya $581.6 billion. zinatumwa kwa nchi mbalimbali na Diaspora kuelekea nchi za Asia, hii inatufundisha nini? ni kwamba watu wenye asili ya Africa hawatumi fedha nyumbani kwao Africa na waafrika wa nyumbani Africa ni mabingwa wa kutorosha fedha zaidi ya $ 148 billion kwa mwaka hii ina maana gani hawa wanaoiba na kuficha nje ni wale wenye passport moja je hawa wakipata passport mbili coz uwezo wa kununua uraia wanao zipo nchi nying ukiwekeza dola laki mbili tu unapata uraia je hawa wakipata hyo fursa ya dual citizenship unadhani watafanya nini?

Haya umesema Kenya, Burundi, South Africa wanafaidika sana na hii ya Uraia pacha wanafaidika nini wote tunategemea wawe wanafaidika kiuchumi haya linapokuja swala la Usalama wa Taifa unadhani mwenye Passport mbili akifanya tukio aidha la kuiba nyaraka za siri za serikali au akifanya Ufisadi then akafanikiwa kukimbia je Nchi za Africa zinauwezo wa kumpata wakat ana uraia wa nchi nyingine? unadhani nchi za Ulaya na Amerca ni nyepesi kwa kukubali raia wao kuhukumiwa nje ya mataifa yao? leo America akimtaka hata raia wa Tanganyika rabda kafanya kosa alipokuwa US na akafanikiwa kutoroka wanauwezo wa kumpata lakini je Tanganyika ikimtaka mtu aliyefanya kosa Tanganyika na kukimbilia US kwa nini ni vigumu kumpata? why vije vigezo vya hili si kosa kwa nchi hii ?
 
Acha drama Mkuu. Watu wa diaspora wataiba pesa kutoka wapi? Au unasahau kama wakipeleka fedha kwenda nje ni kwa kuwa wamezizalisha wenyewe? Kumbuka kwamba huko sio "kutorosha" katika context unayoisema wewe, kama vile wanaiba. Hiyo inaitwa "repatriation of income" ambayo inaruhusiwa kisheria. Haina tofauti na jinsi kampuni zinazo-invest toka nje zinavyofanya. Unafikiri kwa mfano, kampuni ya mafuta BP wakigundua mafuta Tanzania, wakawa wanazalisha, ile fedha wanayopata itaenda wapi? Watatakiwa kuitumia Tanzania? Hapana, wanaruhusiwa ku-repatriate hizo revenues. Sasa huko utaita kutorosha? Na kwa nini iwe sawa kwa BP na Acasia kufanya hivyo na sio diaspora mwenye uraia pacha?

Kumbuka kwamba hata ukipata kazi nchi kama Botswana, kuwa na uraia wa Tanzania kunafanya uruhusiwe ku-repatriate income unayopata Botswana kuja Tanzania, sasa huko sio kutorosha wala kosa. Ni wazi kwamba nikiwa nina uraia pacha say between Botswana na Tanzania, nikipata faida sana Tanzania nitataka nipeleke sehemu ya faida hiyo Botswana ili kuwekeza huko pia kama vile kununua nyumba, kwa kuwa mimi ni raia pia wa Botswana. Bottomline ni kwamba nimefanya shughuli ambayo zimezinufaisha Tanzania na Botswana.

Na kumbuka the opposite is true. Kama mimi nimechukua uraia wa Botswana, siruhusiwi ku-repatriate income kuja Tanzania kwa kuwa sina sababu ya msingi ya kufanya hivyo, maana inaonwa kwamba ni uondoaji wa forex ya Botswana. Lakini Botswana wakijua nina uraia wa Tanzania basi nitaruhusiwa kirahisi sana, na hilo ndilo watu waliochukua uraia nchi nyingine wanataka. Bila Tanzania kuruhusu uraia pacha, wanabanwa ku-repatriate income kutoka nchi walizo kuleta Tanzania.

Halafu haya mambo ya kusema wataiba nyaraka za siri ni kwamba nyie mnaangalia movie za kitoto za kipelelezi halafu mnaleta mambo yenu hapa. That is just drama. Wizi wa nyaraka sio kwamba ni lazima ufanywe na mtu wa uraia pacha. Na kuwa raia pacha kunakupaje access kwenye hizo nyaraka za siri hadi uone kila mwenye uraia pacha analeta hatari ya kuiba nyaraka za siri? Nyaraka zipi za siri ambazo ni raia pacha tu wanaoweza kuzipata?

Suala la kusema tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa mtu akiwa na uraia pacha na Marekani haitaruhusu ahukumiwe Tanzania akifanya kosa hapa inaonyesha tu ni jinsi gani watu wengi mnaokataa uraia pacha mna wigo wa kitoto sana wa kufikiri kuhusu hili suala.

Ndio maana nikasema wengi mnaobisha juu ya hili la uraia pacha wala hamlielewi. Mnabisha tu kwa katika ignorance yenu. Mnakera sana.
 
Back
Top Bottom