Wakati si milele

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,453
Reaction score
872,052
Wakati si milele bandugu siku hazigandi hata siku moja kwahiyo twapaswa kuwa na subra na uvumilivu kwenye kila jambo ,mambo mengi yanaharibika kwakuwa watu wanakosa uvumilivu ,subira .

UVUMILIVU KWENYE MAHUSIANO
Unapaswa kuwa mvumilivu na msukivu
kumbuka huyo mwenza wako mmetoka mazingira tofauti hamuwezi kufanana hata siku moja kwa mambo yote au kukubaliana
mmekutana mkiwa watu wazima !alikokulia yeye na ulikokulia wewe ni tofauti kabisa ,tabia binafsi mlizo nazo zimejengwa zaidi ya miaka 20 huwezi kuzibadilisha kwa mwaka mmoja au miwili
kinachotakiwa ni kuwa na subira busara na uvumilivu tuu !mahusiano yako yatakuwa ya furaha na yatadumu


SUBIRA KWENYE MATATIZO
Wengi wetu hushindwa kutatua matatizo yetu kwa sababu tu hatuna uvumilivu huwa tunafikiri ndio mwisho na hakuna ufumbuzi tena ikifikia hapa watu huchukua maamuzi ya hovyo ya kupombeka au hata kukatisha uhai kumbuka leo si jana kwa hiyo hata hili ulilonalo leo linalokuumiza sana na kukunyima raha litapita tu
Wakati si milele siku hazugandi na maisha yanaendelea ukishindwa kabisa kutatua tatizo ulilo nalo uwachie wakati utaamua kwakuwa wakati huwa haushindwi na lolote wakati hauna haraka wakati si milele

Jumapili njema wana MMU woote...!
 
Asante kwa kutukumbusha hayo...maana Uvumilivu sikuhizi limebaki neno tu
 
Safi mkuu,we ni mdogo wake mandela?unawosia mzuri inabidi tukushirikishe kwenye mgogoro wetu wa ziwa malawi.
 
^^
"... Me and Patience are old friends..." By Merlin
^^
 
Safi mkuu,we ni mdogo wake mandela?unawosia mzuri inabidi tukushirikishe kwenye mgogoro wetu wa ziwa malawi.

Mmh kule kwa Joy ana bifu lake binafsi na one of the boyz ll men..! Ziwa malawi ni kisingizio tuu...!
 
Mwallu kuna Novel moja ya James Hadley Chase inaitwa VULTURE IS A PATIENT BIRD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…