...Wakati nchi inalawitiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

...Wakati nchi inalawitiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BMW, Apr 23, 2012.

 1. B

  BMW Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Folks,


  Imagine wewe ni mwana familia. Familia inalia njaa. umekaa unafikra nzuri kabisa juu ya jinsi gani mkate unaweza kupatikana, lakini pamoja na fikra hiyo nzuri umekaa tu huchukui hatua mpaka familia yote inateketea kwa njaa. Is your thinking any useful??

  Wiki iliyopita Afisa Mipango wa wilaya ya kahama akiwasilisha revenues forecast kwa wilaya ya Kahama, alitanabaisha kuwa wanataraji kukusanya zaidi ya Billion 3 lakini CHAKUSHANGAZA alikaririwa akisema ZAO LA TUMBAKU ndilo linaloongoza kuchangia mapato kiasi cha mil 800+ huku migodi mikubwa miwili ya dhahabu ya Bulyankhuru na Buzwagi ikitarajiwa kuchangia dola laki 4 sawa na takribani mil 600+. HAYA JE SI MATUSI YA NGUONI KWA TAIFA???? HUKU SIO KULILAWITI TAIFA??? mwanangu wa miaka minne tu nimemsimulia hili haijamuingia akilini. How on earth, in a country with people claiming to be great thinkers is this allowed kwamba taifa linaendeshwa na tumbaku/TB pamoja na massive export ya GOLD??

  Point yangu ni nini dhidi ya Jamii forums na makundi mengine kama hili. Yes we are great thinkers But our thinking must liberate this country. Hapa jamii yapasa sasa kuanzia sasa tuache kupost tu details bali tuje na mikakati ya kuhamasisha wananchi kulikomboa taifa. Hii migodi inahitaji movement ya kumobilise wananchi waivamie waifunge, watupe nje kila mzungu, tuweke ulinzi potelea mbali ulaya wakituwekea vikwazo tutatrade na China na URUSI........otherwise huu ni upuuzi na our thinking is not helping this nation.
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Ukiwa na maana tuanzishe chama?au gazeti huru?au tuwapatie wananchi tabs au laptop na generator kijijini ili wate habari za kuwahamasisha??au kila atakayesoma uzi aingie mtaani kwa mapanga kule buzwagi?au au atakayesoma uzi hapa amwambie mwenzake kwamba wakutane ukumbifulani au??Mimi sijakuelewa kimsingi labda mimi ndo mvivu wakufikiri au?ngoja waje watakupa jibu.
   
 3. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  KK
  Majibu yote ni sawa Mkuu
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mku mwisho hapo umenena vizuri lakini mwanzo hapo maneno hayana nguo.

  Lakini kumbuka pia kwamba mapato ya migodi yanatawaliwa na Central Government, hizo Halmashauri huwa wanapewa kiasi kidogo sana. Ikianzishwa serikali za majimbo ndipo kila jimbo (Local Government) zitakuwa zinaweza kulinda na kufaidika na mali zilizoko kwenye maeneo yao.
   
 5. B

  BMW Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uko sahihi Kaka kwamba mapato yanatawaliwa na central Government lakini issue hapa ni kwamba kuna DISTRICT SERVICE LEVY ambayo inapaswa iwe 0.6% ya mapato yote ya kampuni ya mwaka........kwa ukubwa wa migodi hii inayozalisha trilions mil 600 ni utani uliokithiri
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Wengine tushakataa hiyo self-patting, almost religiously feel-good induced patronising label ya "Great Thinkers".

  The trouble with calling yourself a Great Thinker is that great thinkers seldom call themselves so. Ukimsoma Socrates aliyeitwa na oracle la Delphi "the wisest man alive", alipata tabu sana kuelewa oracle anamaanisha nini kwa maana yeye mwenyewe hakujiona kama mtu mwenye busara sana.

  Ukimsoma huyo Yesu/ nabii Issa anakwambia wanaojikweza watashushwa, na wanaojishusha watakwezwa. Yeye mwenyewe kaingia Yerusalem huku kapanda punda badala ya farasi mweupe.

  Ukimsoma Newton, wakati kila mtu anamu admire kwamba ni mwanasayansi aliyegundua formula za motion, yeye mwenyewe alisema hajui dunia inamuonaje, bali mwenyewe anajiona kama mtoto mdogo aliyesimama ufukweni na kuweza kukijua kijiwe kimoja, wakati bahari nzima inamsubiri.

  The trouble with true great thinkers is that they are humbled by knowledge. The more you know, the more you know you don't know and would never dare call yourself a "Great Thinker".

  Kwa hiyo, kwangu mimi at least, mtu mmoja anaweza kumuita mwingine "Great Thinker". Forum moja inaweza kuiita nyingine ya "Great Thinkers".

  Lakini ukisikia mtu anajiita "Great Thinker" au forum inajiita hivyo ujue kazi bado sana. Hii habari ndiyo waswahili wanaiita "kujivika kilemba cha ukoka".

  I don't know about you, but as for me I have declared myself a simpleton who not only doesn't know, but also doesn't even know that he doesn't know sometime ago.

  Samahani nimetoka nje ya mada ya kati.

  Kuhusu hiyo mada labda ni muda wa kujaribu decentralization kama wanavyotaka CHADEMA.
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Ni katika muktadha upi nchi inalawitiwa? Hii nchi ni ya kiume ama ya kike? Na kwa nini usiseme nchi inabakwa? Kwani lazima kusema kama ulivyosema?
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Anaweza kukwambia ingawa kubakwa ni kubaya, kulawitiwa kunaweza kuwa kubakwa kinyume na maumbile na kama unaelewa mfano wa kubakwa, basi anajaribu kukuonyesha mfano kwamba hali ni mbaya zaidi ya kubakwa.
   
 9. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Du...Punguza makali kidogo ya maneno.... Nchi kulaw....du?? Hii mupya.....

  Maoni yangu ni kuwa tumependa wenyewe hii hali kwa kuendelea kukumbatia watawala wanaofanikisha huo mpango wa nchi kupigwa nanilihiii... 2015 haipo mbali ni wakati wa kuamka... tutumie kura zetu kwa busara.
   
 10. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  Kubakwa ni Bila Ridhaa yako, Ila kulawitiwa inaweza kuwa umeridhia Mwenyewe. Mtu anaweza kubakwa kwa kulawitiwa.
   
 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Neno zuri lenye kuunganisha kitendo cha kufanywa kwa nguvu ni KUNAJISIWA.

  TANZANIAINANAJISIWA NA WAWEKEZAJI CHINI YA USIMAMIZI THABITI WA SERIKALI YA CCM
   
 12. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,293
  Likes Received: 2,107
  Trophy Points: 280
  uta trade na China wakati China wana Trade na US na UK? you are really a simple minded thinker!
   
 13. alberaps

  alberaps JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 804
  Trophy Points: 280
  Sometime U talk things with lots of sense.
   
 14. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  uko sawa muno jamani hamasisheni jamii zenu tukomboe taifa hili kama tunafikiri vizuri
   
 15. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Ni kweli tiafa limebakwa kama sio kulawitiwa. Lakini sio suala la kushika mapanga wala nini. Wenzako wameishaanza siku nyingi kuhamasisha umma na kuupa semina za ukombozi wa pili wa taifa. Jiunge na hamasisha wengine kujiunga kwa vitendo na M4C - ili ifikapo 2015 tuwaondoe madarakani wabakaji wa taifa hili.
   
Loading...