Wakati Acacia ikifungasha virago, tukumbushane mambo ya kijinga tuliyokuwa tunafanya mgodini

IMG_20171006_130502.jpg


APA ndipo
 
SURFACE/JUU KABLA YA KUZAMA SHIMONI
Unawahi kazini maana hesabu zako zinalipwa kwa masaa baada ya kugogesha kitambulisho chako getini. Unaingia kwenye vyumba vya kubadirishia nguo, Unatagi kitambulisho chako juu kwa ajili ya kutambuliwa wakati wa kulipua Chini ya ardhi, unachukua jagi la maji, unavaa nguo za kazi na vifaa vya kujiokoa mwenyewe then unaenda kuchukua chakula (kiloba). Unapewa kadi ya kusaini kuelewa sheria za kazini na sehemu utakayoenda kufanyia kazi pia aina ya mashine.

KWENYE CAGE/LIFT
Hapa ndipo mnakutana wote kusubiri kusafiri kwa winch inayotumia umeme. Story za hapa ndipo utafahamu akili za ma miner zilivyo. Mkiwa hapa ndipo utasikia mtu anajisifu kutembea na mademu na off days aliifanyia nini. Kwa kifupi maneno pointless utakutana nayo hapa.

NDANI YA CAGE
Hapa ndipo utavunjika mbavu kwa matani ya kila namna. Kwa kifupi hata ukiwa na umri wa waziri mkuu inabidi uazime akili za kijana wa kidato cha pili.
NB: Akili za ma miner zinafanana huenda ni nature ya kazi (kufanya kazi chini ya ardhini).

ENEO LA KAZI
Hapa kuna makundi mawili, kundi la kwanza ni lile la MAKAZI KUNOGA /wapenda sifa kwa mabossi na wachapa kazi hawa wakifika eneo la kazi ni kazi kazi kweli

Kundi la pili ni WAZUGAJI hili kundi ndilo nilikuwemo mimi, kuna siku tukiamua kazi ni kazi kweli na tukiamua kuzuga ni kuzuga kweli. Unazugaje na wakati uko kwenye mashine za mzungu!? Jibu hili hapa, tulikuwa tukifika eneo la kazi jambo la kwanza ni kuharibu mashine harafu baada ya lisaa limoja tunatoa taarifa kwa kupiga simu zilizoko Chini huko shimoni, mafundi hadi wafike na kugundua tatizo tayari tutakuwa tumepumzika vya kutosha

USHAWAHI KUJIULIZA WAFANYAKAZI MAMIA KWA MAMIA SHIMONI WANAJISAIDIA WAPI na AJALI ZIPI NI COMMON UNDERGROUND!? NI WAPI UTAKIMBILIA ENDAPO KUNA HALI YA HATALI SHIMONI, JE UKITOKA SHIMON NI MASHARTI YAPI UYAFANYE NA VITUKO VYA KUIBIANA SABUNI NA MAFUTA KWENYE MAROKA Usikose part II
Hiyo migodi akishapewa mchina ndipo akili itatukaa sawa. Maana technolojia ya mchina kwenye migodi kama hiyo anaijua mwenyewe
 
Wak wahawa jamaaaa kama wanataka kuindoka bongo nawanaanza kunchojonoa Aliko dangote ipo kaziiii
 
Back
Top Bottom