Wakati Acacia ikifungasha virago, tukumbushane mambo ya kijinga tuliyokuwa tunafanya mgodini

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,125
8,631
SURFACE/JUU KABLA YA KUZAMA SHIMONI
Unawahi kazini maana hesabu zako zinalipwa kwa masaa baada ya kugogesha kitambulisho chako getini. Unaingia kwenye vyumba vya kubadirishia nguo, Unatagi kitambulisho chako juu kwa ajili ya kutambuliwa wakati wa kulipua Chini ya ardhi, unachukua jagi la maji, unavaa nguo za kazi na vifaa vya kujiokoa mwenyewe then unaenda kuchukua chakula (kiloba). Unapewa kadi ya kusaini kuelewa sheria za kazini na sehemu utakayoenda kufanyia kazi pia aina ya mashine.

KWENYE CAGE/LIFT
Hapa ndipo mnakutana wote kusubiri kusafiri kwa winch inayotumia umeme. Story za hapa ndipo utafahamu akili za ma miner zilivyo. Mkiwa hapa ndipo utasikia mtu anajisifu kutembea na mademu na off days aliifanyia nini. Kwa kifupi maneno pointless utakutana nayo hapa.

NDANI YA CAGE
Hapa ndipo utavunjika mbavu kwa matani ya kila namna. Kwa kifupi hata ukiwa na umri wa waziri mkuu inabidi uazime akili za kijana wa kidato cha pili.
NB: Akili za ma miner zinafanana huenda ni nature ya kazi (kufanya kazi chini ya ardhini).

ENEO LA KAZI
Hapa kuna makundi mawili, kundi la kwanza ni lile la MAKAZI KUNOGA /wapenda sifa kwa mabossi na wachapa kazi hawa wakifika eneo la kazi ni kazi kazi kweli

Kundi la pili ni WAZUGAJI hili kundi ndilo nilikuwemo mimi, kuna siku tukiamua kazi ni kazi kweli na tukiamua kuzuga ni kuzuga kweli. Unazugaje na wakati uko kwenye mashine za mzungu!? Jibu hili hapa, tulikuwa tukifika eneo la kazi jambo la kwanza ni kuharibu mashine harafu baada ya lisaa limoja tunatoa taarifa kwa kupiga simu zilizoko Chini huko shimoni, mafundi hadi wafike na kugundua tatizo tayari tutakuwa tumepumzika vya kutosha

USHAWAHI KUJIULIZA WAFANYAKAZI MAMIA KWA MAMIA SHIMONI WANAJISAIDIA WAPI na AJALI ZIPI NI COMMON UNDERGROUND!? NI WAPI UTAKIMBILIA ENDAPO KUNA HALI YA HATARI SHIMONI, JE UKITOKA SHIMON NI MASHARTI YAPI UYAFANYE NA VITUKO VYA KUIBIANA SABUNI NA MAFUTA KWENYE MAROKA Usikose part II
4d8cdc830e68433782ce5643ab3309e7.jpg
65ae86679a5350527b48c6da32405485.jpg
a2afbb5e13f441e8c64c511e28d65f15.jpg

-------------------------------
-------------------------------

Soma part 2 >> PART II: Wakati Acacia ikifungasha virago tukumbushane mambo ya kijinga tuliyokuwa tunafanya mgodini

PART III: WAKATI ACACIA IKIFUNGASHA VILAGO TUKUMBUSHANE MAMBO YA KIJINGA TULIYOKUWA TUNAFANYA MGODINI

Katika sehemu ya tatu ya simulizi hii niliahidi kuwaletea maelezo ya kwa nini uchimbaji au uvunaji wa dhahabu huambatana na imani za kishirikina huku albino wakiwa ni wahanga wakuu wa hii imani

Pia nilidokeza inachukua muda gani hadi uwe approved kushuka chini lkn katika hili taelezea (kutokana na maswali ya wasomaji) ni wapi Mtanzania atajifunza kazi ya u miner ili awe professional!!

Pia tamalizia kwa kuzungumzia biashara ya ngono na maambukizi ya UKIMWI katika maeneo yote ya machimboni kwa mikoa ya Shinyanga na Geita pia tazungumzia faida ya uwepo wa mgodi na maendeleo yaliyopatika baada ya kuja kwa kampuni hizi za madini.

Mwisho tatoa shukrani kwa Watanzania waliofanikisha kuniwezesha kuwa miner hadi pale nilipo resign mwenyewe na baadae kutimiza ndoto zangu za kuzamia ng'ambo.

Kutokana na kuzidiwa na majukumu, sehemu hii itakuwa ya mwisho japo tajitahidi kujibu maswali yatakayoulizwa na ambayo nitakuwa na uwezo wa kuyajibu.

ANGALIZO: Mimi ni miners (sijasomea u miner) na wala sina elimu (elimu yangu ni O level tu), hivyo maswali kama gharama za kuendesha mgodi na mengine ukweli sitaweza hivyo namshkru [HASHTAG]#jiwedogo[/HASHTAG] kwa namna ambayo amekuwa msaada kwangu katika habari hii.

IMANI ZA KISHIRIKINA

Ushirikina katika uchimbaji wa madini nilianza kuushuhudia nikiwa bado mdogo (kipindi ambacho Bulyanhulu inamilikiwa na wachimbaji wadogo zamani yakiitwa machimbo ya "Bariadi", neno Bariadi lilitokana na wachimbaji wenye asili ya wilaya ya Bariadi (Wanantunzu) kubatiza jina kwa minajili ya kuweka kumbukumbu na kuendeleza dharau zao kwa wasukuma (watu wa Magharibi). Kumbuka Wanantunzu ni watani zetu na wasukuma hivyo hata wangeyaita machimbo ya Chenge wala tusingemind.

Iliaminika huwezi kupata dhahabu bila kwenda kwa waganga wa kienyeji kupewa "ndagu" na ndagu karibia zote zilikuwa na mashariti magumu likiwemo kutambikia na ikiwezekana kutoa kafara mtoto, mke au wazazi na ikiwezekana kumpa ndugu yako mpenzi uzezeta (Itonjo).
Ma Albino kanda ya ziwa walikuwa washaanza kutumika sana kwani hata mimi niliaminishwa kuwa Albino huwa hafi isipokuwa hupotea tu hadi namaliza Form four GESECO nilikuwa najua hivyo.

Wanantunzu ni moja ya makabila ya kipuuzi sana (Jamani nawatania watani zangu) ila ni ukweli ulio wazi kuwa kupitia kujikita kwenye dhahabu na ushirikina (mimi si muumini) Kwa kweli ni matajiri sana. Unaweza kufanya research ya matajiri wengi wenye asili ya kanda ya ziwa utawakuta Wanantunzu kibao na baadae watu wa Mara na Musoma.

Katika mgodi wa Bulyanhulu kuna imani karibia kwa ma miner wote kuwa kila inapokaribia kuisha kwa mwaka au mwanzo mwa mwaka lazima mgodi ule kichwa (Mtu atangulie kwenye haki) au itokee ajali itakayohusisha na kumwaga damu hata kama mtu huyo hatakufa. Upande wangu katika hili huwa niko neutral kwani ni kweli matukio hayo hutokea (kipindi nilipokuwa hapo).

WAPI UTAJIFUNZIA KAZI YA UCHIMBAJI NA KUWA MINER!!

Katika Tanzania hakuna chuo kinachofundisha kuwa miner isipokuwa utapata tu elimu ya kwenye makaratasi (madaftari) na sio vitendo.
Wote maboss wa Kitanzania unaowasikia kuwa wako wanasimamia migodi, wako nje ya nchi kama ma expert hawa wote waliingia mgodini wakiwa mambumbumbu tu. Mgodi wa Bulyanhulu hutoa mafunzo ya kuwa miner juu na baadae mnapelekwa eneo maalumu chini kufanya kwa vitendo kwa muda wa wiki kadhaa kama miner trainee. Hapo ndipo niliwakuta Sosteness Mnoku, Gibu na Carlos (Watanzania) wakitoa mafunzo na ujanja wote wa shimoni.

Kwa kifupi ukitaka kuwa miner (professional) hakikisha unapitia mgodi wa Bulyanhulu iwe kwa vyeti au njia za panya.

Hata ukiwa tayari umeshaiva na unafanya kazi mgodini (chini) bado mgodi huo hutoa mafunzo tena kwa awamu ili kukukomaza na baadae kupanda daraja kama jeshini huku na mshahara wako ukizidi kuwa juu. Baada ya kupanda madaraja kazaa hapo ndipo utawagundua Watanzania walivyo na roho mbaya kama makaburu. Ukipanda daraja mara nyingi huchaguliwa kuwa msimamizi na hapo ndipo unyanyasaji kwa walio chini huanza mara moja (si wote ila kwenye kumi utakuta aidha wawili tu ndio wanakumbuka walikotoka)

MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Katika hili halihitaji maelezo mengi. Biashara ya ngono Bulyanhulu na maeneo ya kanda hiyo (GEITA na KAHAMA) yalisababishwa na ma miner kuwa wanahonga pesa ndefu kwa dada zetu wauzaji na wakiwa wamelewa chakali!! Ilipelekea wadada kila tarehe 14 na mwisho wa mwezi wanakodi Hiece kutoka mijini kuja kuwashughulikia miner kwa kuwapa joto na ngoma huku baadhi ya miners wakitelekeza familia zao hadi wanashitakiwa mgodini na kuanza kukatwa mshahara kwa ajili ya kuzilinda familia zao (mwanamke wako anafuata pesa ya matumizi mgodini baada ya wewe miner kupokea mshahara na kupotea nyumbani). Nakumbuka kuna miner walikuwa wakipata off na mshahara wanaenda hadi Zanzibar ku spend. Wote tunakumbuka basi la Nyehunge likiwa linatoka stand ya mabasi Nyegezi Mwanza tulikuwa tunataniwa na makondakta kuwa.... "Peleka waathirika hao" huku basi likiwa limejaa mahandsome boys na mademu wakali

FAIDA ZA KUWEPO KWA MGODI

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kuwepo kwa huu mgodi ndiko kumeifanya Kahama izidi kuwa juu kimaendeleo. Mgodi umewekeza sana katika jamii hasa katika suala la elimu, Afya na huduma mbali mbali. Ni mgodi huu hutoa huduma ya ndege kwa mgojwa iwapo atakuwa hawezi kutibiwa katika hospital yao ya mgodini na ile ya kisasa iliyopo Bugarama. Ndege huletwa endapo mgojwa huyo atakuwa amepata ajali mbaya kazini au uraiani na hapa huwa hakuna ubaguzi.

Nikianza kutaja uwekezaji walioufanya mgodi wa Bulyanhulu kwa kweli itachukua msururu wa maandishi. Kutokuwepo kwa lami ni Serikali yetu. Mgodi uliomba kuweka lami barabara ya kutoka mgodini hadi ile ya Manzese Kahama lkn waliomba wapewe hizo pesa wajenge wenyewe na zikapingwa.

Bila Bulyanhulu (Barrick) pasingekuwa na Kakola ya sasa, Bugarama ya sasa, Ilogi ya sasa pia hata Umeme usingekuwepo ukiachia huduma ya maji kwani kila kijiji lilikopita bomba la maji ya ziwa Victoria kuja mgodini wameweka chanzo cha maji na wananchi wanachota bure.

SHUKRANI ZANGU

Nawashukru sana miner wote wa kitengo cha Narrow Vein kipindi hicho, namshukuru sana Andy Mwakibete, Kaka Emanuel Mbise, Kaka Kitiku, Kaka Zagalo king Mario mzee wa faka, kaka Emanuel Masuwe, Walimu wote wa kitengo cha Mafunzo, dada Sarah wa Community na kampuni ya Sodexho na AKO kwa kutupatia msosi wa haja mwisho ni Wazugaji wote na utunzaji wa siri tuliokuwa tunatunziana kuepuka kufukuzwa kwa style ya uzugaji wa aina yake.

Mgodi wa Bulyanhulu una dhahabu nyingi sana, tumuunge mkono raisi katika vita hii ya kiuchumi.

Mwisho nakuombea mapumziko mema huko ahera rafiki yangu KADELEMA kwa ajali iliyochukua uhai wako mgodini shift ya usiku tukiingia pamoja getini na nikitoka peke yangu getini.
 
Hahahahahhaaaaa, hayo maisha ni karibia ma miner wote duniani hata wazungu tulikuwa tunaona wakizuga kama sie
Tena wazungu ndo wazugaji wazuri. Kuna mmoja aliletwa kutoka SA akawapewa uboss kwenye Shaft ni full kuzuga muda wote anacheza game tu hadi wenzake wakawa wanammind maana alikua hajui lolote zaidi ya kubebwa.
UG alikua anaenda mara moja kwa week.
 
Hewa ya huko chini haina shida kuivuta? Kuna kina ukifika hewa itakua sumu?

Joto vipi?
Mgodini (underground) ni kama nyumba ya ghorofa, sehemu zingine hewa ni nyingi, sehemu nyingine hewa ni kidogo sana hasa narrow vein mining, sumu huwezi kuikwepa kwani milipuko ile huwa ni sumu, kuna sehemu ukikuta blasting imefanyika unahisi hadi ngozi ya mwili inawasha sababu ya sumu (fumes). Kuna sehemu hapo Bulyanhulu wanaita development (mwisho wa mgodi unakoendelezwa), huko jasho linatililika hadi kujaza gabuti. Ndiyo sababu miner wote wale wanaochimba kitaalamu na wale locally hutumia pesa ovyo sababu ya mazingira hatarishi ya kazi. Hakuna sehemu ambayo unafikia na kukuta sumu tu hapana. Mgodi wa Bulyanhulu ni kati ya migodi ya kisasa kiteknolojia, wamesambaza njia za hewa kote japo huwezi kulinganisha na hewa Natura ya mungu
 
Back
Top Bottom