Wakandarasi wasiolipa mishahara, wanaoomba rushwa kwa wateja kutopewa kazi REA 3

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Wakandarasi wenye tuhuma za kutolipa mishahara wafanyakazi wao, kuomba rushwa kwa wateja wanaotaka kuunganishiwa umeme na kutolipa fedha za watoa huduma waliokuwa wakifanya nao kazi katika usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili, hawatapewa kazi husika katika miradi ya REA Awamu ya Tatu.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na kampuni mbalimbali zinazotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili inayotarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.
 
Back
Top Bottom