Wakamatwa kwa ukwepaji wa kodi

Wakamatwa kwa ukwepaji wa kodi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
WATU wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kwa makosa mbalimbali akiwamo kuingiza uyoga aina ya Soya Gold na mifuko laini ya plastiki kutoka nchini Malawi bila kulipia kodi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei
Katika tukio hilo, Musa Maulidi (23), ambaye anatuhumiwa kuingiza bidhaa hizo bila kulipa ushuru.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa na paketi 750 na marobota matatu ya karatasi ambavyo vyote havikuwa na nyaraka zinazoonyesha kuwa amelipa kodi.

Alisema alikamatwa katika eneo la kizuizi cha barabara kilichoko eneo la Kayuki barabara kuu ya Tanzania na Malawi wilayani humo, majira ya saa 12 :45 asubuhi akisafirisha bidhaa hizo kutoka Kyela kuelekea Mbeya.

“Mtuhumiwa kwa sasa yupo mahabusu na tunakusudia kumpeleka mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria, ili kukomesha vitendo hivi ambavyo vimekithiri katika barabara hiyo,” alisema Kamanda Matei.

Katika tukio la pili Kamanda Matei alisema kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Bahati Kasungula (35), alikamatwa akisafirisha vitenge kutoka nchini Malawi kuingiza katika Mkoa wa Mbeya.

Alisema mtuhumiwa huyo pia alikamatwa katika kizuizi cha barabara cha Kayuki ambacho kimekuwa maarufu kwa kukamata wakwepa kodi wanaoingiza bidhaa kutoka nchini Malawi kwa kupitia njia za panya na hivyo kukwepa kodi.

Katika tukio la tatu Kamanda Matei alisema kijana mwingine, Juhudi Kasyupa (25), mkazi wa Majengo katika Wilaya ya Chunya, alikamatwa na jeshi hilo akiwa anamiliki mali mbalimbali za wizi.

Alizitaja baadhi ya mali ambazo kijana huyo alinaswa nazo kuwa ni pamoja na boksi moja la daftari, deki, kompyuta, betri za solar, runinga, kopo la rangi na solar panel.

Alisema baada ya mtuhumiwa kupekuliwa alikutwa na vifaa mbalimbali vya kuvunjia nyumba zikiwamo nondo, bisi bisi na kwamba vitu hivyo vilikutwa nyumbani kwa mtuhumiwa na kwamba alipohojiwa hakuwa na maelezo ya kujitosheleza.

Katika tukio la mwisho, Kamanda Matei alimtaja kijana mwingine kuwa ni Juma Adamu (23) mkazi wa Mbozi mkoani Songwe ambaye alikutwa na mali za wizi.

Alisema kijana huyo alikamatwa katika eneo la Mlima Reli lililoko kwenye Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi akiwa na mali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi ikiwamo ‘Copper Plate’ tatu.

IPP
 
watu wanatafuta maisha nyie mnwarudisha nyuma, matajiri wakubwa wote michezo hiyo wamecheza walikuwa stable wakaacha, wakaanza kwenda kihalali
 
Back
Top Bottom