Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,669
- 119,293
Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) kuisaidia serikali kutekeleza kwa vitendo, azma ya kubana matumizi kwa kupunguza safari, ambapo Wakala hio, inayatoa mafunzo hayo humu humu nchini kupia mtandao wa Video.
Mkurugenzi wa TaGLA, Bw. Charles Senkondo, amezitaka Wizara, Idara, Wakala na Mashirika ya Umma nchini kuitekeleza azma hiyo, kwa kutumia Wakala kuendesha mafunzo yoyote yatakayohitajika, ambapo Wakala itendesha mafunzo hayo humu humu nchi, kwa kuwatumia wakufunzi wa kimataifa waliobobea katika fani zao walioko nje ya nchi, hivyo kuokoa mamilioni ya fedha ambayo yangetumika kuwapeleka maofisa hao nje ya nchi.
Senkondo, ametoa wito huo, wakati wa kufunga mafunzo ya kimataifa ya Menejimenti ya Miradi: Uratibu, Tathmini na Ufuatiliaji, “Project / Program Management: Planning, Monitoring and Controlling” , yaliyokuwa yakiendeshwa na mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Utumishi wa Umma nchini Canada, ENAP huku wahsirikiwakiwa nchini Tanzania, kwa kuunganishwa kwa mtandao wa video kwenye ukumbi wa TaGLA, uliopo chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam.
Senkondo, amesema, mafunzo hayo ni muendelezo wa juhudi za Wakala kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo Watanzania wengi zaidi na kwa gharama nafuu wakiwa hapa hapa nchini wakiwa na wigo mpana wa uchaguzi wa taaluma na wakufunzi, muda wa kupata mafunzo na muendelezo wa kutoa huduma kwa wananchi
Akizungumzia faida za Elimu kwa Mtandao wa Video, Bw. Senkondo amesema Elimu kwa Mtandao inapunguza gharama (posho, usafiri) za uendeshaji wa mafunzo na kuwezesha watu wengi kupata elimu/ mafunzo na kwa gharama nafuu ikilinganishwa na kama watu hao wangesafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo hayo.
Pia amesema Elimu kwa Mtandao, inawezesha wataalamu/wakufunzi kutoka duniani kote kutoa mafunzo kwa Watanzania bila wao kuja nchini Tanzania hivyo kuokoa muda na kupunguza adha mbalimbali zikiwemo hatari za kusafiri, ajali, uchovu, kukabidhi ofisi/kazi, kutengana na familia/jamii na usumbufu.
Naye Mratibu wa Mafunzo wa Wakala hio ya TaGLA, Bw. Dickson Mwanyika, amesema Wakala hiyo, inaendesha kozi mbalimbali za mtandao kwa kushiikiana na vyuo na taasisi mbalimbali zinazotoa mafunzo duniani.Mbali na kozi ya kimataifa ya Menejimenti ya Miradi: Uratibu, Tathmini na Ufuatiliaji, “Project / Program Management: Planning, Monitoring and Controlling” , Wakala kwa kushirikiana na chuo kikuu cha ENAP, itaendesha kozi ya utendaji unaotegemea matokeo, “Result Based Management” inatarajiwa kufanyika tar 9 – 13 Mei 2016.
Nae Mkufunzi Mzalendo wa Kozi hiyo ya Project Management, Bi. Rukia Wadoudi, amesema kozi hiyo ya “Project / Program Management: Planning, Monitoring and Controlling” ni muhimu kwa wasimamizi wa miradi wa wizara zote, idea zote na wakala za serikali na hata taasisi zote za umma na binafsi.
Baadhi ya washiriki wa kozi hiyo, wameisifu Wakala ya Elimu kwa Njia Mtandao kwa kuendesha kozi za kimataifa bila wanafunzi kulazimika kwenda kwenye nchi husika, hivyo wamewawezesha wafanyakazi waliomakazini, kuweza kuhudhuria masomo wakati wa jioni, hivyo kutolazimika kuchukua likizo za masomo.
Architect Amina Mgaza kutoka Wakala wa Majengo Tanzania, TBA, amesema kozi hiyo itamsia kuongoza vizuri miradi anayoisimamia.
QS Peter Saliem kutoka Wakala wa Majengo, amesema kozi hiyo itaisaidia serikali kupata value for money , amesema wamepata kwa kawaida kozi hiyo ingechukua muda mrefu, lakini wameweza kupata mambo makubwa katika muda mfupi.
Eng. Abubakar Ahamed, hii ni njia nzuri ya kuweza kupata mafunzo kwa kufunza na wabobezi kutoka nchi za nje.Eng. Mtapuli Juma, ni mtaalamu wa mazingira, “tumeweza kujifunza toka kwa wataalamu wan je waliobobea kwa ghaa nafuu kama azma ya rais ya kubana matumizi na Nachinana Mgimwa kutoka chuo kikuu cha Muhimbili, amesema kwa kuhudhuria kozi hii, amejifunza mengi katika usimamizi wa miradi, kila mtu anayeshughulika na usimamizi wa miradi, angepaswa kuhudhuria kozi hii.
Wakala wa Elimu kwa Mtandao, TAGLA, ni Wakala ya Serikali ilio chini ya Ofisi ya Rais Menejmenti ya Utumishi wa Umma. Ofisi za Wakala zinapatikana Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Block A, Ghorafa ya saba. na uko kwenye Chuo cha IFM jijini Dar es Salaam.
Paskali.
Salaam.