Wajue virus(trojan) (chizicomputer) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajue virus(trojan) (chizicomputer)

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by edjizzo, Dec 25, 2010.

 1. edjizzo

  edjizzo Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TROJAN
  ni mfumo wa recomand key ambao mafaili yana weza kuya fanya mafaili mengine kufanya yanavyo taka.
  FAIDA
  utumika kwenye crank vitu ambavyo vimelock
  urecommand computer
  uwa kama akimu
  HASARA
  usababisha kufuta mafaili na kufanya shughuli zisizo takiwa
  u crash computer
  uwa ni mwizi na mwaribifu
   
 2. MKURABITA

  MKURABITA JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Una mawzo mazuri, ila lugha yako sijaielewe, au unajifunza kiswahili? Tumia English tukuelewe vizuri mkuu.
   
 3. WIRELESS

  WIRELESS Senior Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umechemka kuelezea, I know more about all types of viruses. Goo deep man. use english if possible.
   
 4. edjizzo

  edjizzo Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sio kijana lugha yetu masikini ukianza kusema lugha ya kisomi watu vile vile watashindwa kunielewa asante
   
 5. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Acha dharau kijana; Great Thinkers hapa, ain't it?
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Virusi za kompyuta

  Virusi za Kompyuta ni programu haramu yenye uwezo wa kujisambaa ndani ya kompyuta na kujiingiza ndani ya programu halali zinazotakiwa kufanya kazi mle. Ikisambaa inaathiri programu halali na kusababisha hasara. Virusi zinasambaa kwa njia ya intaneti lakini pia kwa njia ya sidii au diski yoyote ya kubebea data kati ya kompyuta. Virusi vinaweza kuharibu mafaili na kupunguza uwezo wa ufanyaji kazi wa kompyuta yako.

  Historia

  Programu za virusi zilianzishwa tangu vyanzo vya kompyuta vyenyewe. Wanahisabati maarufu kama John von Neumann walikadiria nadharia ya programu zenye uwezo wa kujiendeleza na hata kujisambaa peke zao tangi miaka ya 1950. Tangu kupatikana kwa kompyuta ndogo za nyumbani imeonekana ya kwamba programu za aina hii zinaweza kuleta hasara mbalimbali. Mara nyingi programu (c)Brain hutajwa kama virusi  ya kwanza iliyosambaa kwenye kompyuta ndogo tangu mwaka 1986. Usambazaji wake ulikuwa kosa la watungaji wake waliotaka kukinga diski za programu halali waliyouza dhidi ya kopi haramu; waliandika namba ya simu yao ndani ya virus.


  Tangu kupatikana kwa intaneti kuna watu maelfu ambao wametunga programu za virusi kwa kusudi mbalimbali; mara nyingi ni vijana wanaotaka kujaribu uwezo wao wa kuandika programu za aina hii. Wengine wanakusudia mzaha tu wakitaka kuona mafanikio yao kwenye kompyuta za dunia yote. Kuna wengine wenye hasira dhidi ya kampuni kubwa kama Microsoft, dhidi ya benki, dhidi ya serikali au dhidi ya  binadamu kwa jumla. Hao ni hatari zaidi wakijitahidi kusababisha hasara kubwa. Wengine hufuata kusudi za kisiasa wakilenga kwa kompyuta za lugha au nchi fulani hasa. Virusi nyingi zina malengo ya kijinai kwa sababu watungaji wao wanajaribu kupata faida ya kifedha kwa njia ya utapeli wakijaribu kuiba maneno ya siri kutoka kompyuta ya watu yanayomruhusu mtumiaji kuwasiliana na benki na kutuma fedha kwa akaunti yningine.

  Hatari za kutumia makompyuta mengi-mengi

  Mtandao wa intaneti unaruhusu mamilioni ya watumiaji wa kompyuta duniani kuungana pamoja kibiashara na hata kwa kujifurahisha. Watu wengi tofauti hutumia intaneti. Yeyote anayetumia Intaneti anaweza kupata habari nyingi kuhusu mada tofauti, tena kwa lugha tofauti, yaani, katika kipindi kidogo sana.


  Intaneti inawezesha mtu mmoja kuharibu au kupunguza uwezo wa mamilioni ya kompyuta ambazo zimeunganishwa nazo. Wanaweza kufanya hivi kwa kuandika program za kompyuta. Au, wanaweza kuzifanya kompyuta zijiweke taarifa za kipuuzi ambazo zinasabisha kompyuta iache kufanya kazi. Iwapo sio mwangalifu, basi unaweza kusababisha kompyuta iache kufanya kazi.  Hasara kubwa zilizosababishwa na "worm"

  Mnamo tar. 24 Januari, 2003, aina ya kirusi cha kompyuta kiitwacho "worm" kilitolewa ili kuathiri Intaneti. Worm ni mfululizo wa maelekezo ya kompyuta ambayo yanajiweka nakala nyingi-nyingi yenyewe na kuzituma kwa kompyuta nyingine.


  Huyu worm ametuma nakala kibao zake mwenyewe kwenye kompyuta nyingine kupitia Intaneti. Huyo worm ameharibu mamilioni kadhaa ya kompyuta duniani. Imepunguza uwezo wa makompyuta kibao kupitia mitandao ya kompyuta.


  Kampuni za kupiga vita virusi

  Sophos P-L-C ni kampuni ya kompyuta ya huko Britania ambayo inatengeneza program za kuilinda kompyuta dhidi ya virusi. Hii ni kampuni ya nne kwa ukubwa ya kutengeneza program za kuzuia virusi.


  Hivi karibuni, kampuni ya Sophos imetangaza onyo rasmi watumiaji wa kimpyuta kujikinga dhidi virusi vipya vingi na worms. Tangaza lilitoa maelezo juu ya baadhi ya watu wanaofanya kazi kwa juhudi kutengeneza bidhaa pepe haramu za kompyuta. Kampuni ya Sophos ilisema ya kwamba hizi ni ripoti kutoka katika gazeti lililochapishwa nchini Singapore mnamo tar. 14 Januari, siku tu kable ya shambulio la worm lililofanywa katika Slammer.


  Graham Cluley ni mtalaamu wa kompyuta katika kampuni ya Sophos. Alisema kwamba kampuni za utengenezaji wa programu za kulinda kmpyuta zinategemea virusi vingi kwa mwaka huu. Alisema watunzi wa virusi wanataka kubuni virusi vingine vyenye nguvu kupita hata hivi vya worm. Hii itaweza kusambazwa kupitia ujumbe elektronikia au njia ya mawasiliano ya kompyuta iitwayo Instant Messaging (Ujumbe wa Haraka  kama vile Yahoo Messenger, Google Talk, Windows Live Messenger, na kadhalika). Bwana Cluley aliendelea kusema kwamba aina hii ya virusi husababisha matatizo makubwa sana.
  Wataalamu wa kompyuta wa Kampuni ya Sophos walisema kuna virusi vya kompyuta takriban 40,000 ambavyo kwa sasa vinafahamika kama v


  ipo. Wataalamui hao waliendelea kusema kwamba takriban virusi vipya 200 hutolewa kila mwezi kupitia Internet.
  Bwana Cluley alisema miaka kumi au tisa iliyopita kompyuta nyingi zilizoharibiwa na virusi ni zile ambazo zinatumia Microsoft Windows kama ndiyo mfumo wake wa uendeshaji, yaani, operating system.
   
 7. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Virus!= Trojan
  Please eddy slow down! Post zako zinaanza kuniboa. Hazioneshi unavyoji advertise. Please slow down utajikwaa mdogo wangu!
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Akieleweshwa anasema anapondwa nadhani anataka watu wawe wanafiki wamcheke kwa pembeni
   
 9. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni mbaya kwa mtaalamu yeyote! Kukosoana ndio kusaidiana ndio kukua kitaaluma
   
 10. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  EDJIZZO, mimi nakuaminia. Umenipa ushauri mwingi na umenifaa
   
Loading...