Jua Tofauti kati ya Virus,trojan na Worm

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
115
Kosa ambalo watu wengi huwa tunalifanya katika topic ya Computer Virus ni kujumuisha Worm au trojan kama Virus,Haya maneno huwa yanatumika sana midomoni mwetu kana kwamba yote ni kitu kimoko,Sio kweli kwamba zote ni kitu kimoko bali ni Utitofa.Trojan,worn na virus zote ni malicious programu ambazo zinaweza kukuharibia Computer yako,lakini kuna tofauti kati ya hivi vitu na kuzijua zinaweza kukusaidia katika kulinda Computer yako kwani wahenga walisema "KUMJUA ADUI YAKO NI MOJAWAPO YA USHINDI" sasa iweje leo hii kipindi tunapambana na Mafisadi tutafanikisha vipi endapo hatujui hata tofauti kati ya Fisadi na Gaidi..haha Just Porojo...Twende kazi

Kirusi cha Computer(computer virus) huwa kinajiingiza kwenye program au faili chenyewe ili kiwe na uwezo wa kusafiri kutoka computer moja hadi nyingine.Na huwa kikiacha infection wakati kikisafiri,Wataalamu wa mambo ya Security huwa wanasema kuwa Computer virus huwa vinafanana sana na virusi katika mwili wa Bin Adam,Baadhi ya virusi huwa vinaathari ndogo tu wakati vingine athari zake huwa ni kubwa mno kwani vinauwezo wa kuharibu Software,hardware na vijiFile.Ukweli ni kwamba Virusi vyote huwa vinajiunganisha kwenye Excutable file yaani nina maana huwa vinajiingiza ndani ya mafaili ambayo wewe inabidi uje kujarun,kwa mfano kama unainstall program yoyote sasa firus huweza kupenya ndani ya hilo file na kujifanya nacho ni sehemu ya hilo file.Hii ina maana Kirusi kinaweza kuwa ndani ya Computer yako lakini hakiwezi kuwa na effect yoyote hadi uirun hiyo program,Kwa mfano wewe mwenyewe umedownload software yako ya kuangalizia Ip za watu,sasa kirusi kinaweza kikawa ndani,sasa hakitakuwa na tatizo,ila hiyo siku utayosema ahaa leo nataka Niinstall hii program yangu hapo sasaaa.
Jua kwamba Virusi haviwezi kusambaa bila ya mkono wa mwanadamu,kwa mfano kurun infected program ambayo kirusi kimo ndani..
nadhani umenipata kwenye maelezo yangu hapo juu..watu huendelea kusambaziana virusi either kama e mail attachment au mutu anakuja kwenyePC yako na ka USB kake then anakuambia muzee hii progam ni bomba muno kumbe haijapima italiga wapi(ina Ngoma) kaaaazi kwelikweli.

worm inafanana sana na kirusi katika muundo wake na wataalamu wa mambo ya Usalama wanasema kuwa Worm ni mutoto wa kirusi.Worm husafiri kutoka Computer moja hadi nyingine ila sio kama Kirusi,Worm haiitaji msaada wa mtu,chao chenyewe kinaweza kufanya mandingo..Worm huwa vinatumia msaada wa mafaili au transport mechanism ili kusafiri bila ya msaada wa mtu.Ubaya wa Worm ni kuwa vina uwezo wa kujiCOPY vyenyewe sasa kama kimekuja kimoja baada ya sekunde kumi unakuta vipo mia na vishasambaa Computer nzima.kuna siku kuna Mjinga mmoja alinitumia worm,basi kakawa kamchezo kazuri kwani nikawa naviona vikijidai kwenye Computer yangu kama kwao vle,Shenzi zao...sasa badala ya computer yako kutuma Worm mmoja inaweza kutuma mamia ya virusi,upo?? Mfano mzuri ni kuwa unaweza kushangaa kuna mtu akiingia online tu unakuta mimessage kibao anakutumia,kumbe yote ni miworm(sio Virusi),Worm anauwezo huu wa kutumia your address list contact katika e mail kujitumia miworm na ikifika kwa hao jamaa ambao wapo kwenye addreaa yako nao kama wapo online then hutuma kwa watu ambao wapo kwenye list zao na mziki unaendelea..kumbuka kuwa hapo sasa unaongelea mamia ya minyoo(Worm) kwakuwa hii minyoo ina uwezo wa kujicopy(Kwa kichina tunaiita fuyinzhen-复印真 just safari na muziki wakuu)Kutokana na kamtindo cha kujituma yenyewe hii minyoo huwa inatumia system memory nyingi na pia bandwidth kubwa kwani kama munavyojua kila kitu katika computer kinahitaji memory na kipindi unatuma kitu chechote online unatumia Bandwidth kwakuwa kama tunavyojua coputer huwa zinatumia kitu kinachoitwa Windowing katika TCP connection so kama kiasi cha Buffering chote kimechukuliwa na Minyoo ina maana wewe huwezi tuma kitu(Kuna kipindi watu wanalalamika mbona Internet ipo very slow kumbe minyoo imekaba Bandwidth yako yoooote wewe mwenyewe hujui na unaanza kumpigia simu ISP kumlaumu angalia net yenu ipo slow,ninyi mifisadi na mijizi waaapi wakuu) katika research zangu za hivi karibuni nimedokolea sehemu wanasema kuna minyoo inaitwa much-talked-about .Blaster Worm hii minyoo kama inakuwepo kwenye Computer yako basi yule mtumaji ana uwezo wa kucontrol computer yako nzima,Anaweza kuizima,kuiwasha,kufuta chochote hata kuuninstall your operating system..so kuwa makini na hii minyooo wakuuu.hapa ndio mahacker wanapoanzia kufanya kazi zao(Big Up kwa hawa jamaaa)..

Trojan naweza kusema kuwa ni janja sana hizi jamaa kama walivyoiita mythological Trojan Horse,trojan inawezekana ikaonekana kana kwamba ni kitu kizuri mno lakini ikakuharibia kila kitu endapo utainstall,Chukua mfano murua...Umeenda sokoni kununua papai,umeliona papai limewiva kinomi lanjanooo,ukalinunu akuwa na imani kuwa litakuwa tamu,umerudi home,umeosha baada ya mlo si unajua tena matunda sio mpaka asema daktari ukaamua kulikata,vile unakata hamade ndani unaona kuna miparachichi,mipera nk yote imo ndani..je utalitupa au??? Jua kwamba trojan huwa zina muonekano wa kuvutia saaana ila ukishaintall tu umekwisha muzee,inaanza kazi mara leo ibadilishe Icon zako,mara kesho ikuwekee passwors wakati wa Kulog in,mara ibadilishe youe wallpaper na kuna kipindi zina uwezo hata wa kufuta mafaili yako,asume pale mzee kuna faili lako la vitafunwa limetulia na mipicha toka kwa mzee Brazaman then lao linayafutilia mbali...hahahahahaha utaumia...Vlevle trojan wana uwezo wa kumpa mtengeneza trojan Access ya Computer yako so akaitumia kama yake vle kwa kuchukua vtu anavyotaka..tofauti na Mivirusi na Minyoo ni kuwa hawa trojana hawana uwezo wa kujisambaza kwenye mafaili mengine pia hawana uwezo wa kujicopy so hapa inakuwa rahisi ukimkamata mmoja basi umemaliza kila kitu

Kukuchanginyi zaidi kuna hiki kitu kinaitwa blended threat,Hiki wakuu ni hatari kwani chao huwa kinakusanya Minyoo,virusi na Mitrojani na Code zenye walakini kwa pamoja na kuziweka kama kitu kimoja..Utakimbilia wapi??? Hii huwa inatumia Server na Internet kusafiri na kujisambaza so huwa inasambaa haraka sana na madhara yake ni makubwa mno,tabia ya hizi ni kuwa huwa inasambaa kwa njia nyingi si unajua ndani yake kuna madudu kibao na athari zake ni balaa so kazi kwako hapo,wataalam wanaamini kuwa hii ndio babayao kwani yao inauwezo wa kufanya collabo ya Worm na virus wakakushambulia,huyu anapiga huku huyu anabadilisha hiki..hapo sasa

Jinsi ya kupambana
haya tumeona maadui wetu sasa ni jinsi gani ya kupambana nao???
Njia ya kwanza ni kuweka Computer yako UP-2-date kwani katika kila update huwa kunakuja na kinga za haya majamaa,kwa mfano wa wale wanaotumia Microsoft windows internet explorer wapo kwenye risk kimtindo ukilinganisha na wanaotumia kitu kama Mozila kwani Mozila huwa inafilter madudu yaliyokaa kimashakashaka na uwezi weka ADDONs ovyo..kumbuka hapa sipigii debe Mozila wala sipondi Window kwani mimi sina masilahi nazo ila nina masilahi na Watanzania.
Njia ya pili ni kutumia Anti-virus software ambayo ina anti spayware,pia inakuja na Fiwewall yake kwani kuna muda hizi firewall za Vitu kama Window tayari watu wanazijua sana( Firewall ni Kama Ukuta ambao huwa na gate moja ambalo hupitisha tu Packets ambazo zimehakikiwa,chukulia mlinzi kakaa getini la Ubalozi wa Tanzania China ,so kashapewa amri kuwa hapa hapiti mtu zaidi ya mchina ambaye anaenda kuomba visa au mtanzania ambaye anaenda kumuona Mzee mapuri..sasa kama wewe mtanzania unakuja unaulizwa unaenda wapi unasema naenda kuonana na mr manongi basi yule mlinzi aongei na wewe ni kufunga geti lake tu ndio maana kuna kipindi unaweza ona unataka kuchatt kwa kutumia MSN messanger lakini haiconnect hii ni mamboya firewall kwani katika Luga za ufundi huwa tunatumia Mambo ya ports)
Kumbuka kuwa Firewall sio kama itakuzuia kupata Virusi ila kwa kushirikiana na Mi Antivirus itakuwezesha kujikinga au kukupa ulinzi tosha.
Kuweni makini na E mail au attachment toka kwa mtu usiyemjua au hata kama unamjua lakini imekaa kizushizushi au mtu anakutumia kitu bila ya uhusiano ingawa unamjua,,Kuna kipindi kuna Rafiki yangu alikuwa ananilalamikia kwanini huyu mtu kila akisignin tu attachment kibao inakuja?? so kuwa makini wazee..
Nimeandika sana so nadhani mutakuwa mumenipata..kama una utata kwenye mambo hayo au ya Networking basi usisite kuwasiliana nami kwa kutumia private e mail.
好好学习不如你去做生意吧-Kama masomo hayapandi nenda kafanye Biashara
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom