Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,116
- 8,662
Ukiwa mwenyeji ama mzaliwa wa maeneo ya Shinyanga ama Geita na kama ni mdau wa madini katika uchimbaji mdogo basi neno "manyani" utakuwa umeshalisikia mara kibao.
KWA NINI WANAITWA MANYANI
Tafasiri yangu binafsi ni kuwa: Manyani ni kundi la vijana wachimbaji wadogo (umri wao ni rika la vijana na wanaweza kuwepo watu wazima wachache sana). Vijana hawa hufanya uvamizi wa gafla na haraka pale wewe unayemiliki shampo (shimo) kihalali na imejulikana linatoa dhahabu hasa (pure gold) maarufu usukumani kama "shikole". Vijana hawa huvamia wakiwa wamejihami kwa siraha zao hatari za kiuchimbaji wakiwa wengi wakishuka kwa kasi bila utaratibu wa kiusalama na mara nyingi hutumia kamba (mikono) badala ya miguu. Wengine hubaki juu baada ya kukufukuza kwa kukupiga mmiliki kwa ajili ya kupokea vifusi vya mchanga unaosadikiwa kuwa na dhahabu kutoka chini. Ieleweke kuwa wanapovamia wanakuwa tayari kufa na kupona kwani baadhi yao huja na mapanga tayari kwa lolote.
NYUMA YA PAZIA LA MANYANI
Manyani imekuja kubainika hivi karibuni kuwa baadhi yao hukodishwa na matajiri (wanunua dhahabu) kwa mkakati ulioratibiwa kwa ufanisi sana. Nilishawahi kushuhudia tajiri mmoja Nyagalata akipiga risasi juu ili kuwasaidia Manyani kuiba dhahabu. (Sitamtaja)
MAISHA YASIYOKWEPEKA KWA MANYANI
Mara nyingi manyani katika harakati zao za kufanikisha maisha kwa kuiba ama kuvamia huishia kufa aidha kwa kulipukiwa na baruti chini ya ardhi na muda mwingine hufariki kwa kuangukiwa kifusi ardhini kwa sababu wanapoingia kuiba huwa hawajali kuchimba ukuta hata ule unaolinda shimo lisishuke maarufu kama "ngunzo za shimo".
KIAPO CHAO
Manyani ni watunza siri sana na lengo ni kutotoa siri nje za ajali zinazotokea chini ya ardhi ili kulinda eneo lililo na dhahabu serikali isilifunge. Manyani /nyani anapopata ajali na kufa shimoni wewe uliyekuwa nae unatakiwa uweke mwili wake pembeni,vuna dhahabu na kaa kimya. Huwa wanapeleka taarifa za kufa mwezao pale wanapokuwa wamesafisha eneo lote.